Quantcast
Channel: PolitiksiFactTrack ''ARUSHA255''
Viewing all 1899 articles
Browse latest View live

Utata dhamana ya Lwakatere wa Chadema

$
0
0

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare akipelekwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana, Picha na Venance Nestory


HATMA ya dhamana ya Mkurugenzi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare, na Joseph Ludovick, imebaki kuwa kitendawili baada ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo kuwa na udhuru.

Lwakatare na Ludovick Joseph, wanakabiliwa na kosa la kula njama baada ya Mahakama Kuu kuwafutia mashtaka ya ugaidi.

Kesi hiyo ilitajwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo, baada ya Hakimu Mkazi Alocye Katema anayeisikiliza kesi hiyo kutokuwapo mahakamani.

Kabla ya kuahirishwa kwa kesi hiyo, wakili wa utetezi, Peter Kibatara, aliomba mteja wake apatiwe dhamana kwa kuwa kosa hilo lina dhamana kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Prudence Rweyongeza, aliomba ombi hilo litupwe kwa kuwa mahakama haiwezi kutoa dhamana kwa kesi isiyokuwepo.

Alidai kilichopo mahakamani ni jalada la tuhuma zinazowakabili washtakiwa ambazo ziko hatua ya uchunguzi na kwamba mwisho wa siku itafunguliwa kesi rasmi Mahakama Kuu ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kuisikiliza.

“Shauri liko katika hatua za uchunguzi na bado DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini) hajafungua kesi rasmi Mahakama Kuu, sasa tunashangaa mawakili wa washtakiwa wanawasilisha ombi la dhamana leo,” alidai.

Hivyo aliiomba mahakama itupilie mbali maombi hayo kwa kuwa hakuna kesi rasmi iliyofunguliwa na DPP Mahakama Kuu.

Baada ya kuwasilishwa kwa hoja hizo, Hakimu Fimbo aliahirisha kesi hadi Mei 27 mwaka huu na kusema Hakimu Katemana ndiye atakayetolea uamuzi maombi hayo.

Washtakiwa hao wanadaiwa kuwa Desemba 28 mwaka jana, huko Kimara King’ong’o Stop Over, walikula njama kwa kutaka kumdhuru Denis Msaki ambaye ni mhariri wa habari wa gazeti la Mwananchi kwa kutumia sumu.

Mei 8, mwaka huu, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, iliwafutia mashtaka matatu washtakiwa hao likiwemo la ugaidi.

Chanzo: Happiness Katabazi, Tanzania Daima


IKULU YAMJIBU DR. SLAA KUHUSU KASHFA YA UDINI WA RAISI KIKWETE ALIZOZITOA

$
0
0

Taarifa kwa media Ikulu

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mheshimiwa Wilbroad Slaa, leo, Jumatatu, Mei 13, 2013, amekaririwa na gazeti moja akidai kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na timu yake ya kampeni, “ilikuwa ikisaka kura kwenye nyumba za ibada na kumwaga sumu mbaya ya udini ambayo sasa inaitesa Serikali nataifa” kwenye Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010.

Aidha, katika habari hiyo iliyoandikwa chini ya kichwa cha habari, “Dk. Slaa amlipua JK” kwenye gazeti linalounga mkono CHADEMA la Tanzania Daima,Mheshimiwa Slaa anadai kuwa migogoro ya sasa ya kidini “inajengwa au kutengenezwa na Serikali iliyojikita kusambaza sumu ya udini katika misikiti wakati wa kampeni za Urais mwaka 2010”.

Kwa hakika, hakuna namna nyingine ama namna bora zaidi ya kuielezea kauli hii ya Mheshimiwa Slaa isipokuwa kwamba kauli hiyo ni riwaya nyingine isiyokuwa na mshiko. Ni uongo mtupu. Yake Mheshimiwa Slaa ni maneno yasiyokuwa na ukweli wowote.

Ni uzushi na santuri ambayo imezoeleka sasa kwa wananchi. Kauli ya Mheshimiwa Slaa ni mwendelezo wa mtiririko usiokuwa na mwisho wa ghiriba ambazo kamwe hazitafanikiwa za Mheshimiwa Slaa kuwahadaa wananchi ukweli wa mambo ulivyo katika nchi yetu.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na timu yake ya kampeni kamwe hawakufanya kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010, ama wa mwaka mwingine wowote, katika nyumba yoyote ya ibada iwe msikitini ama kanisani ama hekaluni ama nyumba nyingine yoyote ya ibada mahali popote katika nchi yetu.

Mheshimiwa Rais Kikwete hajawahi hata kufikiria kuchanganya dini na siasa. Hana sababu ya kufanya hivyo. Anaelewa fika madhara ya udini kwa mustakabali wa nchi yetu, kwa umoja wa taifa letu na kwa mshikamno wa wananchi wake.

Yoyote anayejaribu kumbebesha Rais Kikwete msalaba wa udini ana lake jambo na ni vyema atuambie fika Rais alitumia Msikiti upi, ama Kanisa lipi, mahali gani na kwa nyakati gani kufanya kampeni.

Vinginevyo, kauli ya Mheshimiwa Slaa itabakia ni kauli tu inayostahili kupuuzwa na wananchi, itabakia ni kauli ya mtu mzima anayetapatapa na kufanya jitihada kubwa kujivunjia mwenye heshima kwa kutunga na kusambaza uongo.

Tunanapenda kumshauri Mheshimiwa Slaa kuwa kama  hana jambo la maana lakuwaambia wananchi ama ameishiwa na hoja ni vyema  anyamaze, awaachie wananchi waendelee na shughuli zao za maendeleo, kuliko kuendeleza riwaya zake zisizokuwa na mshiko.Yake ni santuri iliyowachosha wananchi.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya

Raisi Ikulu.

Dar es Salaam.

13 Mei, 2013

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe Amtembelea Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa Nchini Tanzania Francisco Montecillo Padilla na kumpa pole

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Mhe. Francisco Montecillo Padilla, Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa hapa nchini mara baada ya kuwasili Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumsalimia na kumpa pole kufuatia shambulio la bomu  lililotokea Jijini Arusha tarehe 5 Mei, 2013  na kupelekea watu watatu kufariki dunia na wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa. Balozi Padilla alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa  katika hafla ya ufunguzi rasmi wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, Jimbo Kuu la Arusha wakati tukio hilo linatokea.

Mhe. Balozi Padilla akiwa katika  mazungumzo na Mhe. Membe kuhusu tukio hilo  ambapo pamoja na mambo mengine alisema kuwa anaamini suala hilo litapita na wahusika kupatikana na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Mhe. Membe akiagana na Mhe. Balozi Padilla mara baada ya kuzungumza naye.Picha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa

Leo Mei 14 ni Siku ya Kuzaliwa Mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg

$
0
0

Leo Mark Zuckerberg anasherehekea B'day yake,alizaliwa 14 May mwaka 1984. Arusha255 Blog tunamtakia maisha mema yanye afya tela hadi mwisho wa uzee wake miaka mingi ijayo.

Credit: annapita.com

CRDB YAFANYA MKUTANO MKUU WA 18 WA WANAHISA JIJINI ARUSHA

$
0
0

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akitoa mada wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wanahisa wa benki hiyo uliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha, mwishoni mwa wiki. 

Mmoja wa wajumbe wa mkutano Mkuu wa 18 wa Wanahisa wa CRDB akiwa katika maandalizia ya kuingia katika ukumbi wa  mikutano wa AICC jijini Arusha.

Mtangazaji Mkongwe, Salim Mbonde (kulia) akifuatilia Mkutano Mkuu wa  18 wa Wanahisa wa CRDB uliofanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki.

Wanahisa wa mkutano huo.

Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye akifuatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (katikati) wakati wa Mkutano Mkuu wa 18 wa Wanahisa wa benki hiyo jijini Arusha.

Mwanahisa akitoa mada.

Mwenyekiti wa Mkutano huo akisoma majina ya wajumbe waliochaguliwa kuingia katika Bodi ya Wakurugenzi.

Naibu Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kushoto) akiwa na baadhi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo pamoja na mmoja wa wanahisa (wa pili kulia). 

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyadhiyay akiwa na mke wake pamoja na mjumbe wa bodi ya CRDB, Kai. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano huo.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei.

Wanahisa.

Charles Itembe akitoa mada kuhusu fursa za uwekezaji na upatikanaji mitaji katika masoko ya fedha wakati wa semina ya wanahisa wa benki ya CRDB iliyofanyika mjini Arusha.

CHANZO: MROKI MROKI

MBIO ZA UCHAGUZI WA UDIWANI ARUSHA: MWENYEKITI CCM KATA YA THEMI ATIMKIA CUF

$
0
0

Pichani ni aliyekuwa mwenyekiti wa CCM kata ya Themi Petro Ndarivoi (Kulia) akirudisha kadi ya chama cha mapinduzi kwa mwenyekiti wa chama cha CUF halmashauri ya jiji la Arusha Hamza Mustaph kwenye makao makuu ya chama hicho jana jioni

Wakati kipenga cha uchaguzi wa udiwani kikitarajiwa kupilizwa wiki ijayo pichani ni mwenyekiti wa CUF halmashauri ya jiji la Arusha Hamza mustaph akimpatia kadi ya chama hicho Aliyekuwa mwenyekiti wa CCM kata ya Themi Petro Ndarivoi aliyejiunga na chama hicho jana jioni na kupewa fomu ya kugombea udiwani wa chama hicho kata ya Themi.

Mgombea udiwani kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF kata ya Themi kwenye uchaguzi utakaoanza wiki ijayo Petro Ndarivoi akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya CUF halmashauri ya jiji la Arusha jana jioni wakati aliporudisha rasmi kadi ya CCM na kuchukuwa kadi ya CUF mbele ya mgombea udiwani kwenye kata ya ELERAI John Bayo na mwenyekiti wa CUF wilaya ya Arusha Hamza Mustapha.Picha na Mahmoud Ahmad-Arusha

WAKENYA WAANDAMANA KUPIGA ONGEZEKO LA MISHARA YA WABUNGE

$
0
0

Wanaharakati wa mashirika ya kiraia wakipinga hatua ya wabunge kujiongezea mishahara Nchini Kenya hii leo tarehe 14.05.2013 kunafanyika maandamano ya amani ya kupinga nyongeza ya mishahara ya wabunge.

Wabunge nchini humo wanataka tume inayoshughulikia mishahara ya watumishi wa umma iongeze mishahara yao kutoka elfu 532,000 hadi 850,000. Wabunge hao wa Kenya wanasema kima walichoekewa ni kidogo sana kukidhi mahitaji yao.
Hata hivyo tume hiyo imesema haitabadilisha msimamo wake huku ikitupilia mbali vitisho kutoka kwa wabunge hao waliosema wataifuta kazi tume hiyo iwapo matakwa yao hayataridhiwa.

MAADHIMISHO YA SIKU YA WAUGUZI ARUSHA LEO YAFANA,WATAKIWA KUACHA KAULI ZISIZOFAA KWA WAGONJWA

$
0
0

Wauguzi kutoka hospitali mbalimbali jijini Arusha wakiserebuka wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wauguzi duniani ilifanyika leo katika hospitali ya Selian(ALMC)

Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre(ALMC)akisoma hotuma yake.

Muuguzi Mkuu wa Jiji la Arusha,Jane Barakururiza alisema maadhimisho hayo ni muhimu sana kwao kutokana na wajibu wao wa kuwahudumia wagonjwa na kuwasaidia madaktari koukoa maisha ya wagonjwa.

Maadhimisho yaho yalianzia kweny hospitali ya AICC kwa maandamano na kupitia barabara ya Sokoine,Makongoro hadi hospitali ya Selian

Wauguzi wakiwasha mishumaa yao wakati maadhimisho hayo

Sanaa ya maigizo ilipamba maadhimisho hayo

Wauguzi waliamua kukumbukia enzi zile kuimba mashairi

Wauguzi wakila kiapo cha utii na uaminifu wakutokutoa siri za wagonjwa na kutokufanya vitendo viovu leo

PICHA NA FILBERT RWEYEMAMU


YALIYOJIRI KATIKA MAGAZETI YA LEO JUMATANO MEI 15, 2013

Makala: Ujio wa FBI, Usalama wa Taifa Utakuwaje salama?

$
0
0
 

UJIO wa wapelelezi kutoka Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) kusaidia uchunguzi au upelelezi katika tukio la shambulio la bomu katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Olasiti, jijini Arusha, pamoja na matukio ya kigaidi Zanzibar, kwa upande wangu, ni wa kutafakari upya mwelekeo wetu kiusalama nchini.

Msaada wa kiusalama ni muhimu, lakini hata hivyo suala muhimu zaidi ni kwa namna gani unadhibiti nafasi yako ndani ya msaada husika. Kwa lugha nyingine, unachukua hadhari gani wakati wa operesheni za msaada husika wa kiusalama?

Historia ya FBI ni ndefu, tangu kuanzishwa kwake mwaka 1908 (miaka 105 sasa) kwa wakati huo kikiitwa kitengo cha uchunguzi (Bureau of Investigation - BOI) na baadaye mwaka 1935 kubadilishwa jina na kuitwa FBI – Federal Bureau of Investigation.

Hata hivyo, ingawa historia ndefu na uwezo ni mambo mawili tofauti lakini ukweli ni kwamba, uwezo wa FBI katika kazi za kipelelezi ni mkubwa na wakati wote unatanguliza maslahi ya taifa lao na kwa hiyo, ingawa si vibaya kwa FBI kusaidiana na vikosi vya usalama nchini katika upelelezi wa matukio ya kihalifu, hasa yenye sura za kigaidi lakini suala la hadhari dhidi yao ni muhimu pia.

Tatizo hapa si msaada wa FBI nchini bali ni kwa namna gani, vikosi vyetu vya upelelezi na usalama vimejipanga (wakati wote wa msaada wa ki-operesheni kutoka FBI) kuhakikisha hawajianiki moja kwa moja au kujisalimisha mikononi mwa FBI katika mazingira ambayo yanathibitisha viashiria vya udhaifu katika maeneo kadhaa kwa upande wetu.

Eneo la kwanza lenye viashiria vya udhaifu kwa upande wa vikosi vyetu hivyo nadhani ni uwezo binafsi wa kutathmini vitisho dhidi ya nchi (threats assessment).

Katika eneo hili (threats assessment) mazingira yanadhihirisha kwamba kuna wakati vikosi vyetu vimepata kuonyesha udhaifu. Kama ambavyo wamekuwa wakilalamika viongozi mbalimbali wa dini kwamba kumekuwa na uenezaji wa wazi wa chuki za kidini, kuanzia uuzaji wa kanda za video na machapisho mbalimbali, hali hiyo haikufanyiwa uchambuzi wa kina na kwa sasa chuki imeenea nchini wakati ingeweza kudhibitiwa kama kungefanyika tathmini ya kina ya vitisho hivyo na namna ya kuvikabili mapema.

Eneo jingine la pili ni dalili za udhaifu wa vikosi vyetu hivyo katika kukusanya na kutumia (kwa wakati) taarifa za kijasusi kutoka sekta na taasisi mbalimbali nchini au hata nje ya nchi (counterintelligence) ili kudhibiti viashiria vyote vya hatari dhidi ya usalama wa nchi.

Katika eneo hili la pili, nadhani kuna uwezo mkubwa wa kukusanya taarifa lakini pia nina shaka kama taarifa hizo zinazokusanywa zinatumika ipasavyo na kwa wakati. Inawezekana pengine wakubwa wenye kuamua taarifa gani zitumike au la na kwa wakati gani, ndiyo wenye matatizo.

Kwamba inawezekana kuna maofisa waandamizi wasiomudu majukumu yao, wameshikilia madaraka wasioyamudu. Inawezekana katika vikosi vyetu wapo maofisa wabobezi katika masuala ya counterintelligence lakini si waamuzi wa mwisho katika eneo hili.

Mambo kadhaa yamekuwa yakithibitisha kuwapo kwa tatizo hili na kati ya hayo, vurugu za hivi karibuni, miezi kadhaa iliyopita katika mikoa ya kusini, hususan mkoani Mtwara, wakati wa kelele kuhusu gesi asilia ziliposikika na kusababisha vurugu kubwa za uvunjifu wa amani, upotevu wa mali na tishio dhidi ya uhai wa raia.

Kwamba mambo yalifikia hatua ya kulipuka na kusababisha madhara, pengine kutokana na udhaifu wa ama maofisa wa ngazi za chini au viongozi waandamizi ambao inawezekana, licha ya kuwa na taarifa, hawakuwa wepesi kufanya uamuzi katika maeneo mawili niliyoyabainisha hapo awali, yaani tathmini ya vitisho vya hatari dhidi ya nchi (threat assessment) na counterintelligence.

Na hapa ni lazima tuwakane wazi, Tanzania itachafuliwa kimataifa kama mchezo huu wa kushindwa kutumia taarifa za kiintelinjensia kwa wakati utaendelezwa (kwa kuzingatia mifano ya uenezaji chuki za kidini).

Matukio ya vurugu yatakuwa yakitokea na kusababisha vifo na maafa mengine, licha ya ukweli kwamba matukio hayo yanaweza kudhibitiwa baada ya maafa hayo kutokea na kisha eti kuendeleza upelelezi kwa kuwashirikisha FBI.

Jambo la msingi ni kufanyia kazi taarifa muhimu kwa wakati na si kutafakari namna ya kudhibiti fujo. Ingawa matukio ya maafa yanayotokana na vurugu wakati mwingine hutokea popote duniani licha ya uimara wa vyombo vya ulinzi na upelelezi (rejea shambulio la jijini Boston – Marekani wanakotoka FBI) lakini ni busara zaidi kwa vikosi vyetu kujielekeza katika kuwekeza zaidi kwenye kuzuia (prevention) na si kukabili (combating), na hasa kuzuia matukio ambayo msingi wake ni vitisho vya wazi.

Ni hatari kuwa na vikosi vya upelelezi na usalama vyenye kutenda kazi yake katika mwelekeo wa kukabili matukio hatari badala ya kuyazuia.

Tutafakari, kama vikosi vyetu vya usalama na upelelezi mara kwa mara vinayumba katika kujiendesha kwenye mazingira ya hapa nchini, hasa katika kuzima matukio mabaya ya ndani (domestic counterintelligence) hali inakuwaje pale vikosi hivyo vinaposhirikiana na vikosi vya mataifa makubwa, kama FBI? Je, mianya ya FBI kunufaika na ulegevu wowote wa vikosi vyetu imezibwa?

Tanzania inao watalaamu wa usalama wenye mafunzo kutoka nchi mbalimbali duniani lakini swali la msingi; je, utaalamu wao unatumika katika misingi ya weledi? Nahoji hivyo kwa sababu, inawezekana nchi inao watalaamu wa kutosha na makini, tena waliofuzu vizuri zaidi katika mafunzo yao lakini kuwa na utaalamu ni jambo moja na fursa ya kutumia utaalamu husika, kwa weledi, ni jambo jingine.

Ni kweli katika ushirikiano huo na vyombo vya kimataifa vya nchi nyingine kama FBI, mafanikio yanaweza kujitokeza kwa mfano kuwakamata wahusika wa matukio ya uhalifu, lakini hata hivyo, bado tatizo ni lile lie ni kwamba, ni kwa namna gani FBI na vikosi vyetu wataheshimu mipaka yao kikazi, na kwa namna gani hali ya kutazamana kwa ‘jicho’ la kufanyiana ujasusi wa kujihami (defensive counterintelligence) itakuwa ya kujiridhisha kwa upande wa Tanzania?

Binafsi nadhani, ushirikiano wetu na FBI ni muhimu lakini nafasi yetu katika ushirikiano huo kwenye matukio haya inaweza kuwanufaisha zaidi wao kuliko angalau kupata manufaa nusu kwa nusu kati yetu na wao hasa katika zama hizi za uwekezaji wa mashirika makubwa ya kimataifa hapa nchini, kuanzia kampuni za uchimbaji gesi hadi uzalishaji umeme bila kusahau kile kinachoitwa mashirika au taasisi za kimataifa za misaada na maendeleo.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika


Na Godfrey Dilunga,Raia Mwema

Soma hapa Ya Kinana kumkacha DK Slaa na Kisa cha Nape ITV

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa akisalimiana na kufurahia jambo na Katibu Mwenezi wa CCM Nape Moses Nnauye walipokutana katika Studio za ITV.Picha na Chadema

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amemkacha Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa.

Wawili hao walitarajiwa kukutana kwenye kipindi kipya kiitwacho ‘Uzalendo’, kinachotarajiwa kuanza kurushwa wakati wowote kuanzia mwezi ujao katika kituo cha televisheni cha ITV.

Taarifa za Kinana kumkimbia Dk. Slaa katika mdahalo huo zilisambazwa jana katika mitandao mbalimbali ya kijamii nchini.

Taarifa hiyo na vyanzo vyetu vingine vya habari, vilieleza kuwa viongozi hao walialikwa na ITV kwa ajili ya mdahalo ambao ungerekodiwa na baadaye kurushwa na kituo hicho.

Kwa mujibu wa habari hizo, viongozi hao walipewa mwaliko wa kuhudhuria kipindi hicho siku kumi zilizopita na wote kuthibitisha ushiriki wao, lakini Dk. Slaa jana alifika katika studio za kituo hicho na kukutana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, badala ya Kinana.

Akizungumza kwa simu na gazeti hili jana, Dk. Slaa alisema: “Ni kweli tulikuwa tumealikwa kwenye mdahalo pale ITV (leo) jana saa 3, nilipofika nilikutana na Nape, nikamsalimu nikajua kuwa alikuwa amemsindikiza Kinana, lakini nilipomuuliza mwendesha kipindi kwamba Kinana yuko wapi, alisema amepata udhuru hivyo hajafika.

“Nilimwambia Nape wewe si saizi yangu, sitaweza kuongea katika kipindi hiki kama Kinana hayupo, hivyo kipindi hiki kiahirishwe hadi Kinana atakapokuwa na nafasi ya kuja,” alisema Dk. Slaa.

“Haiwezekani mwenzangu akaahirisha ghafla kuja kwenye kipindui halafu nisipewe taarifa na badala yake nikatumiwa Nape, Nape si saizi yangu,” alisisitiza Dk. Slaa.

Taarifa zaidi zinasema kuwa baada ya kuahirishwa kipindi hicho, Nape na Dk. Slaa walisalimiana na kuagana. “Naamini siasa si uadui, niliongea na Nape nikamuuliza Kinana yuko wapi, alisema alikuwa amepata udhuru, akanipigia simu nije,” alisema.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu suala hilo, Nape alisema alikwenda ITV badala ya Kinana, kuangalia maudhui ya kipindi hicho ili aweze kushauriana na Kinana na kuamua kuja au la.

“Mimi ndiyo msemaji wa chama, katibu mkuu hawezi kualikwa mimi nisiwe na taarifa, mimi ndiyo napaswa kwenda na nilikwenda nilipokutana na Dk. Slaa tukaelezwa, Dk. Slaa alishauri kuwa inafaa kualika watu wenye hadhi zinazofanana, yaani makatibu, hivyo mimi niliondoka nikamwacha Dk. Slaa, nadhani alirekodiwa kwa kuwa walisema wanaweza kurekodi mtu mmoja mmoja na katibu mkuu wetu anaweza kwenda siku nyingine kurekodi,” alisema Nape.

Kinana mwenyewe alipotafutwa kwa simu yake ya mkononi kuzungumzia suala hilo, hakuweza kupatikana kwani simu yake iliita bila kupokewa.

Chanzo: Tanzania Daima Mei 16, 2013

DONDOO ZA MAGAZETI YA LE ALHAMISI MEI 16, 2013 NA MJENGWA BLOG

Barua ya Zitto kwa Waziri Kigoda la kuzuia wasanii kunyonywa katika RBT

$
0
0
PENDEKEZO BINAFSI LA MBUNGE KUHUSU KUZUIA UNYONYAJI DHIDI YA WASANII WA TANZANIA KATIKA BIASHARA YA MIITO (RING BACK TONES)

Kwenda kwa:           DR ABDALLAH KIGODA, Waziri wa Viwanda na Biashara

Kuhusu:                    BIASHARA YA MIITO YA SIMU (RINGBACK TONES)

Kumekuwa na malalamiko makubwa sana kuhusu biashara ya mauzo ya nyimbo kama miito kwenye simu. Malalamiko haya yalianzia kwa wasanii wenyewe na baadaye mimi binafsi niliwasilisha hoja zao Bungeni mwaka 2012. Hata hivyo, hadi sasa malalamiko haya bado hayajapatiwa ufumbuzi na hivyo wasanii kuendelea kunyonywa. Tatizo kubwa katika biashara hii ni USIRI na UNYONYAJI kwa wasanii wa Tanzania.  Suala la USIRI lipo Wizara  ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.  Suala la Unyonyaji lipo Wizara ya Viwanda na Biashara.

USIRI

Biashara hii ya “Ring Back Tones” (RBT)  hufanywa na Kampuni za simu (Network providers) kwa kununua maudhui kutoka wachuuzi (Content Providers) ambao  nao huingia mikataba na Wasanii (Content Creators). Hakuna sheria yoyote au Kanuni hapa nchini inayoongoza biashara hii na hivyo “Network providers” na “Content  Providers” kuwa watu pekee wenye taarifa zote za biashara hii.  Kampuni za simu hujumuisha mapato ya biashara hii na mapato yake mengine (Not Ringfenced), hawatoi taarifa za manunuzi ya nyimbo (au ‘content’ nyingine yeyote) kwa wadau na hasa wasanii.  Wachuuzi (Content Providers) nao  hawatoi taarifa za  mauzo kwa wasanii na wanatumia uelewa mdogo wa  wasanii kuwasainisha mikataba inayowanyonya.  Matokeo yake ni kwamba msanii hupata kiasi cha

asilimia mbili tu (2.5%) ya mapato ghafi ya kazi yake.  Hivi sasa biashara hii inathamani (turnover) ya takribani shilingi 44 bilioni kwa mwaka.

Suluhisho:

Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano iandike kanuni (regulations) zitakazolazimisha makampuni ya simu kuweka wazi mapato yatokanayo na biashara ya RBT (Miito ya simu) kila baada ya miezi 4 (disclosure rules).  Kanuni hizi zielekeze makampuni kutoa taarifa za mauzo kwa kila kazi (nyimbo/vichekesho etc.)

UNYONYAJI

Kutokana na usiri ulioelezwa hapo juu, wasanii  wamekuwa wakinyonywa kimapato.  Kwa mfano Msanii hulipwa mapato yatokanayo na ununuzi wa awali wa kazi yake (wimbo) katika mwezi (downloads).

Lakini mapato yatokanayo na “subscriptions” ambapo mlaji hukatwa shilingi 30 kila siku msanii hapati chochote.  Hivyo katika mapato ya sh. 1,300 kila mwezi kwa kila mteja kwa kila wimbo, msanii hupata mgawo wake kutoka shilingi 400 tu za ‘downloads’ na ndio maana wasanii wote nchini hupata 2.5% ya shilingi 44 bilioni zinazokusanywa na Kampuni za Simu.

Nchini Marekani biashara ya miito ya simu (RBT) imetafsiriwa kama maonyesho (Public Performances)  na hivyo “copyright Association”  ya Marekani imeweka kiwango cha chini cha mrahaba (royalty) ambacho msanii hulipwa.  Marekani msanii hulipwa asilimia 10 ya patoghafi linalozalishwa na kazi yake kama muito wa simu.

SULUHISHO

Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara iandike kanuni kwamba mauzo ya kazi za wasanii kama miito ya simu inachukuliwa kama ‘performance’ na kwamba Kampuni za simu zitalipa sio chini ya asilimia 12 (12%) ya  mapato ghafi, ambapo asimilia 10% itakwenda kwa msanii na asilimia 2% COSOTA kwa ajili ya usimamizi  na Ulinzi wa kazi za Wasanii.

HITIMISHO

Kanuni za Uwazi (disclosure rules) katika biashara hii ya ‘Ring Back Tones’ na mgawo wa haki wa mapato (fair and just revenue share) ndio suluhisho endelevu na litakaloleta tija kwa wasanii wa Tanzania na hata Serikali kukusanya mapato stahili. Kanuni (Regulations) zinazopendekezwa zianze kutumika kuanzia tarehe 1/7/2013

Kabwe Z. Zitto, Mb

Kigoma Kaskazini

Dodoma, 13 Mei 2013.

CPwaa ateuliwa kuwa msimamizi mkuu na MC wa michuano ya Mpira wa Meza (Foosball)

$
0
0

Sharon Mariwa Meneja Muenezi Biashara Brainstormusic, Caroline Kakwezi, Meneja Masoko wa Heineken Tanzania na Uche Unigwe – Mkurugenzi Mkuu na Cpwaa msanii maarufu wakishikana mikono na Mkurugenzi wa Heineken Tanzania baada ya kusaini mkataba wa kuteuliwa kuwa msimamizi na MC wa michuano ya mpira wa mezani (Foosball) kulia ni Ronald Louis Meneja Opereshini wa Brainstormusic.

Msanii maarufu wa kimataifa wa muziki wa kizazi kipya CPwaa ateuliwa na kampuni ya bia Heineken Tanzania kusimamia michuano ya mpira wa mezani (Foosball) pamoja na kutangaza na kuhamasisha mchezo huo wakati wa mashindano ambayo ni endelevu.Mpango huo ulikamilishwa kati ya kampuni ya Brainstormmusic & Media Co. Ltd na Heineken Tanzania Limited

Cpwaa, msanii maarufu na wakimataifa wa Bongoflava akisaini mkataba wa kuteuliwa kuwa  msimamizi na MC wa michuano ya mpira wa mezani (Foosball) nchini Tanzania, pamoja naye ni Caroline Kakwezi meneja masoko wa Heineken Tanzania na Uche Unigwe Mkurugenzi wa Heineken Tanzania

Sharon Mariwa Meneja Muenezi Biashara Brainstormusic, Caroline Kakwezi, Meneja Masoko wa Heineken Tanzania, Uche Unigwe – Mkurugenzi Mkuu wa Heineken Tanzania, kulia Cpwaa na Ronald Louis Meneja Opereshini wa Brainstormusic.

--

Credit: HakiNgowi

Taswira: Rais Jakaya Kkwete Atembelea Kiwanda Cha Kuzalisha Unga Cha AZAM na kiwanda cha BIDCO Oil and Soap Jijini Dar es Salaam

$
0
0

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na wadau wa lishe bora kutoka mashirika mbalimbali ya kimataifa  wakizindua mpango wa kuweka virutubisho vya lishe bora katika bidhaa za unga na mafuta nchini uliofanyika katika kiwanda cha BIDCO Oil and Soap kilichopo katika eneo la viwanda la Mikocheni jijini Dar es Salaam  jana

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mafuta yaliyowekwa virutubisho vya lishe bora wakati alipokitembelea kiwanda cha BIDC Oil and Soap kilichopo eneo la viwanda la Mikocheni jijini Dar es Salaam  Jana

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mafuta yaliyowekwa virutubisho vya lishe bora wakati alipokitembelea kiwanda cha BIDC Oil and Soap kilichopo eneo la viwanda la Mikocheni jijini Dar es Salaam jana

Rais Dkt.Jakaya kikwete akiangalia ukaguzi wa uwepo wa virutubisho vya lishe bora katika bidhaa zinazozalishwa katika kiwanda cha kuzalisha unga AZAM ukifanyika katika maabara ya kiwanda hicho Buruguruni jijini Dar es Salaam  jana

Akihakiki jambo katika moja ya Kompyuta ya ofisi ya Kiwanda hicho.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha BIDCO Oil and Soap muda mfupi baada ya kuzindua mpango wa kuweka virutubisho bora vya lishe katika bidhaa za unga na mafuta uliofanyika jijini Dar es Salaam  jana.Picha na  Freddy Maro-IKULU


Mhariri wa Mtanzania Jumatano, Charles Mulinda asimamishwa na Jukwaa la Wahariri kwa kukiuka maadili

$
0
0

Katibu wa Jukwaa la Wahariri Nevil Meena (mwenyekipaza sauti) Picha ya Maktaba


JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF) limemsimamisha uanachama kwa muda usiojulikana, Mhariri wa Mtanzania Jumatano, Charles Mulinda, kwa sababu za kukiuka maadili ya uandishi wa habari. Taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu wa Jukwaa hilo, Nevil Meena, alisema TEF imechukua uamuzi huo baada ya kupokea na kujadili kwa kina taarifa ya kamati ndogo ya wahariri watatu ambayo iliongozwa na Mhariri wa Nipashe, Jesse Kwayu, kwa ajili ya kuchunguza habari iliyochapishwa na gazeti la Mtanzania, Jumatano Aprili 17, mwaka huu ikiwa na kichwa kisemacho ‘Mtandao Hatari’.

Katika habari hiyo, Meena alidai kuwa iliwataja wahariri wawili, Ansbert Ngurumo wa Tanzania Daima na Deodatus Balile wa Jamhuri kuwa ni washirika wa Joseph Ludovick, mshitakiwa katika kesi ambayo ilikuwa ikihusishwa na ugaidi (kabla ya kubadilishwa na mahakama) lakini ikiwahusisha kwa namna moja au nyingine na tukio la kuumizwa kwa Mwenyekiti wa TEF, Absalom Kibanda.

“Yalikuwa ni maoni ya wahariri wengi katika mkutano wa Aprili 18, 2013, kwamba habari hiyo ilikuwa na upungufu mkubwa kitaaluma, hivyo kuamua kuchunguza habari hiyo na kubaini iwapo kulikuwa na ukiukwaji wa maadili na misingi ya kitaaluma ya habari. “Pamoja na mambo mengine ilipaswa kuchunguza mazingira ya kuchapishwa kwa habari hiyo na kama kulikuwa na msukumo wowote nyuma ya kuandikwa kisha kuchapishwa kwakwe,” alisema...

Meena alisema kamati hiyo ilipaswa kuchunguza ushahidi wa tuhuma zilizotolewa dhidi ya Deodatus Balile na Ansbert Ngurumo (kama Mullinda) alivyokiambia kikao cha Aprili 18 kwamba alikuwa na ushahidi wa yale aliyoyaandika. Aliongeza kuwa TEF ilibaini kulikuwa na ukiukwaji wa maadili ya kitaaluma katika mchakato mzima uliowezesha kuandikwa na kuchapwa kwa habari husika na kwamba habari hiyo haikuwa na sifa wala vigezo vya kihabari. Hata hivyo, Meena alisema Mulinda alipotakiwa kutoa ushahidi wa tuhuma dhidi ya wahariri aliowataja, alishindwa kuthibitisha usahihi wa taarifa hiyo.

Kwa kuzingatia matokeo hayo TEF inaushauri uongozi wa New Habari (2006) Ltd na vyumba vingine vya habari kuboresha mfumo wake wa usimamizi wa uhariri ili kuziba mianya kwa habari tata kama hiyo ya ‘Mtandao Hatari’ kupenya na kuwaumiza baadhi ya watu bila kuwapo kwa uthibitisho wa tuhuma husika.

TEF inaendelea kuchukua hatua nyingine za ndani kuimarisha usimamizi wa nidhamu na maadili kwa wahariri, na itaendelea kuchukua hatua dhidi ya ukiukwaji wowote ule wa kitaaluma utakaofanywa katika vyombo vya habari.

Chanzo: Tanzania Daima

ECOBANK,MAWALLA ADVOCATE, MARCAS KUFIKISHWA MAHAKAMNI NA “SHANA BOY”KWA MADAI YA KUIBA MABILIONI YA FEDHA

$
0
0

Wakili Albert Msando akifungua mlango wa duka la Shana Boy walilolifunga kwa madai ya kudaiwa na ECOBANK baada ya kuamriwa na mahakama kuu kanda ya Dar es salaam kufanya hivyo , katikati mwenye kofia mkurugenzi wa Shana enterprises

Mwandishi Pamella Mollel akipiga picha wakati duka la mfanyabiashara Abdallah Mshana lilipokuwa likifunguliwa na wakili Albert Msando

Mkurugenzi wa Shana Entreprises, Abdallah Mshana aliyevaa kofia akijibu maswali ya waandishi wa habari walipokuwa wakishuhudia kufunguliwa kwa duka lake baada ya kufungwa na kampuni ya udalali ya Marcas, mwenye suti nyeusi ni Albert Msando anayeitetea Ecobank ambaye anadaiwa ndie aliyehusika kufunga duka hilo

Credit:  Pamela Mollel

WATUMISHI 10 WA JIJI LA ARUSHA WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA KUJIPATIA MAMILIONI YA KIFISADI

$
0
0

Aliyekuwa Afisa Elimu wa Manispaa ya Arusha (Sasa Jiji), Fatma Laizer akiingia katika viwanja vya mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha akisubiri kupandishwa mahakamani akituhumiwa kujipatia mamilioni ya fedha kupitia mishahara ya watumishi hewa pindi akiwa Afisa elimu.

Mmoja wa watumishi wa idara ya Afsa wakati ikiitwa Manispaa ya Arusha(sasa jiji), ambae jina lake halikupatikana akiingia kwenye viwanja vya mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha akisubiri kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za kujipatia mamilioni ya fedha kupitia mishahara hewa ya watumishi. kushoto ni Afisa mwingine wa Manispaa hiyo

Mmoja wa Maofisa wa Manispaa ya Arusha akiteremka kutoka kwenye gari la TAKUKURU kuelekea kwenye viwanja vya mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Arusha akisubiri kusomewa mashitaka kuhusu kujipatia mamilioni ya fedha kupitia mishahara ya watumishi hewa. hata hivyo walishindwa kupandishwa kizimbani leo kufuatia hati iliyowasilishwa mahakamani hapo kuonekana kuwa na makosa ya kisheria

Ofisa wa takukuru akimsubiri mmoja wa watuhumiwa wa kujipatia mamilioni ya fedha kupitia mishahara ya watumishi hewa akiwa mtumishi katika manispaa ya Arusha baada ya kumfikisha mahakamani hapo

Mmoja wa watuhumiwa akiingia mahakamani hapo baada ya kuteremka kutoka kwenye gari la Takukuru

Published  by Pamela Mollel on May 16, 2013

Mke wa waziri Mkuu Pinda afungua kongamano la Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA) jijini Arusha leo.

$
0
0
 

Mgeni rasmi Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda (wa tano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi viongozi wakuu wa TAPSEA pamoja na waratibu wa Kongamano hilo la Makatibu Muhtasi  Tanzania lililofanyika leo kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Uwezeshaji na Uwekezaji,ambaye pia ni mlezi wa TAPSEA.Dkt Mary Naguakimkabidhi zawadi ya kinyago mgeni rasmi,Mke wa Waziri Mkuu,Mh.Mama Tunu Pinda ,shoto kwake ni Mwenyekiti wa TAPSEA,Bibi Pili Mpenda wakati wa Kongamano la tatu la Makatibu Muhtasi Tanzania.

 

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Uwezeshaji na Uwekezaji,ambaye pia ni mlezi wa TAPSEA.Dkt Mary Nagu akizungumza jambo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye kongamano tatu la Makatibu Muhtasi Tanzania,lililofanyika kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC .

Waziri wa  Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mh.Sofia Simba akizungumza jambo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali kwenye
mkutano wa Kongamano  la  tatu la Makatibu Muhtasi  Tanzania,uliofanyika mapema leo  kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC .

Sehemu ya meza kuu ndani ya mkutano wa kongamano la tatu la Makatibu Muhtasi  Tanzania lililofanyika leo kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC,kutoka kushoto ni  Waziri wa  Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mh.Sofia Simba,Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Uwezeshaji na Uwekezaji,ambaye pia ni mlezi wa TAPSEA.Dkt Mary Nagu,Mgeni rasmi wa Kongamano hilo la TAPSEA,Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda,Mwenyekiti wa TAPSEA,Bibi Pili Mpenda pamoja naNaibu Waziri wa katiba na sheria ambaye pia ni Mshauri wa masuala ya sheria na kazi waTAPSEA,Bi.Angella Kairuki.

Pichani ni sehemu ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye kongamano la tatu la Makatibu Muhtasi  Tanzania lililofanyika leo kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC.

 

 

 

Pichani juu ni sehemu ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye kongamano la tatu la Makatibu Muhtasi  Tanzania lililofanyika leo kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC.

Baadhi ya wageni waalikwa kutoka sehemu mbalimbali wakijiandikisha tayari kwa kushiriki kwenye kongamano la tatu la Makatibu Muhtasi  Tanzania lililofanyika leo kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC.

Mwenyekiti wa TAPSEA,Bibi Pili Mpenda akimkaribisha mmoja wa wageni maalum wa kongamano hilo,Naibu Waziri wa katiba na sheria ambaye pia ni Mshauri wa masuala ya sheria na kazi waTAPSEA,Bi.Angella Kairuki alipokuwa akiwasili kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC .

Mwenyekiti wa TAPSEA,Bibi Pili Mpenda akimkaribisha Mgeni rasmi,Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda alipokuwa akiwasili mapema leo kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC .

Wakielekea kwenye  ukumbi wa mikutano ambao Kongamano la  kwenye kituo cha mikutano cha kongamano la tatu la Makatibu Muhtasi  Tanzania (TAPSEA), lililofanyika leo kwenye kituo cha mikutano cha Kimataifa  jijini Arusha-AICC .

 

Mgeni rasmi,Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda  (wa pili kushoto) pamoja na wageni waalikwa wengine wakitazama ngoma ya kimasai iliyokuwa ikitumbuiza nje ya jengo la mikutano la AICC kabla ya mkutano wa Kongamano  la  tatu la Makatibu Muhtasi  Tanzania kuanza.

PICHA ZOTE NA MICHUZI OTHMAN

LOWASSA AZINDUA KITABU CHA MTIKISIKO WA UCHUMI

$
0
0

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (kushoto), akizindua kitabu kipya kinachoelezea mtikisiko wa uchumi karne ya 2000 na kuendelea, kiitwacho 'The Economic Crisis of the 2000s and Beyond', Dar es Salaam LEO. Katikati ni Mtunzi wa kitabu hicho Dk. Prosper Ngowi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni iliyochapisha kitabu hicho ya Matokeo Publishers &Printers, Rosemary Sokile

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (katikati), akizindua kitabu kipya kinachoelezea mtikisiko wa uchumi karne ya 2000 na kuendelea, kiitwacho 'The Economic Crisis of the 2000s and Beyond', Dar es Salaam leo. Kulia ni Mtunzi wa kitabu hicho Dk. Prosper Ngowi na Mchapishaji, Dk. Charles Sokile.

Baadhi ya wadau waloshiriki kwenye uzinduzi huo

Dk. Ngowi akisaini moja ya vitabu vilivyonunuliwa leo. (PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA)

Viewing all 1899 articles
Browse latest View live