“Serikali huwezi kutibu Malaria kwa kumpa Mgonjwa Panadol” - G. Lema
MUHIMU!! MUHIMU!! TANGAZO KWA WANAFUNZI WOTE WA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA
CHUO CHA UHASIBU ARUSHA
Kutokana na Chuo kufungwa, Baraza la Uongozi wa Chuo katika kikao chake cha dharura cha tarehe 03 Mei 2013 kimeagiza wanafunzi wote kuanzia ngazi ya Cheti mpaka Stashahada ya Uzamili kuzingatia yafuatayo:
1. Kila Mwanafunzi anatakiwa kutuma maombi mapya ya kujiunga na Chuo.
2. Barua ya maombi hayo ipitishwe kwa Mkuu wa Wilaya anapoishi mwanafunzi. Kwa mwanafunzi wa Stashahada ya Uzamili ya Uhasibu barua yake ya maombi ipitie kwa Mhasibu Mkuu wa Serikali.
3. Katika maombi hayo mwanafunzi anaagizwa kueleza namna alivyoshiriki katika vurugu za tarehe 24 Aprili 2013.
4. Mwanafunzi awe amekamilisha malipo ya ada iliyobaki wakati anatuma maombi yake.
5. Mwisho wa maombi ni tarehe 16 Mei 2013.
Maombi yapelekwe kwa anwani ifuatayo:
Mkuu wa Chuo,
Chuo cha Uhasibu Arusha
S. L. P. 2798
Arusha.
08 Mei 2013

BREAKING NEWS: SIR ALEX FERGUSON ATANGAZA KUSTAAFU KUIFUNDISHA MANCHESTER UNITED
SHAFFIH DAUDA anaripoti
Sir Alex Ferguson ametangaza kustaafu kuifundisha Manchester United baada ya miaka 27 ndani ya Old Trafford.
Taarifa za Fergie kutaka kustaafu zilianza kuzagaa tangu jana mchana na usiku zikazidi lakini hakuna habari yoyote rasmi iliyotoka United mpaka leo asubuhi.
Ferguson aliwasili kazini kama kawaida asubuhi akiendesha gari lake katika uwanja wa mazoezi wa United wa Carrington mnamo saa kumi na mbili.
Akitangaza uamuzi wake wa kustaafu alisema: "Uamuzi huu nimeufikiria sana na sikukurupuka. Ni muda sahihi.
'Ilikuwa ni muhimu kuiacha taasisi hii ikiwa katika hali nzuri na imara na ninaamini nimefanya kazi nzuri sana. Ubora wa kikosi hiki kilichoshinda ligi, na uwiano wa umri wa wachezaji unaonyesha kutaendelea kuwepo na mafanikio katika hatua ya juu - mfumo mzuri wa kukuza vipaji unatoa picha nzuri ya mafanikio ya siku zijazo ya klabu.
'Kutokea hapa, nina furaha kuchukua majukumu ya ukurugenzi na ubalozi wa klabu hii. Sasa naangalia mbele kuzitendea haki kazi zangu.
'Lazima niipe shukrani familia yangu, mapenzi yao na sapoti imekuwa muhimu sana kwangu. Mke wangu Cathy amekuwa mtu muhimu katika maisha yangu yote, kunipa moyo pale mambo yalipokuwa hayaendi sawa na kunisapoti. Maneno hayatoshi kuelezea namna gani wakati huu ulivyo kwangu.
'Kwa wachezaji wangu na wafanyakazi wengine wa klabu, wa sasa na zamani, ningependa kuwashukuru kwa kazi nzuri tuliyofanya pamoja iliyonisaidia kuleta kumbukumbu nyingi za ushindi zisizosahaulika. Bila mchango wao historia ya klabu hii kubwa isingekuwa tajiri kiasi hiki.
'Katika miaka yangu ya mwanzo hapa, utetezi wa bodi kwangu, na Sir Bobby Charlton zaidi, ulinipa hali ya kujiamini na muda wa kujenga timu ya soka.
'Katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, familia ya Glazer imenipa kila kitu nilichohitaji katika kuiongoza Manchester United kwa ubora wote na nimekuwa nina bahati sana kuweza kufanya kazi na mtu mwenye kipaji na mwaminifu kama CEO David Gill, Nina washukuru sana.
'Kwa mashabiki, shukrani sana. Mapenzi na sapoti mliyonipa miaka yote siwezi kuielezea. Imekuwa ni heshima kubwa sana kuweza kuiongoza klabu yenu na nimekuwa na ufahari wa muda wangu kama kocha wa Manchester United." alimaliza Ferguson.
HAYA NDIO MAFANIKIO YA FERGUSON KAMA KOCHA
ST MIRREN
Scottish First Division (1): 1976-77.
ABERDEEN
Scottish Premier Division (3): 1979-80, 1983-84, 1984-85.
Scottish Cup (4): 1981-82, 1982-83, 1983-84, 1985-86.
Scottish League Cup (1): 1985-86.
European Cup Winners' Cup (1): 1982-83.
European Super Cup (1): 1983.
MANCHESTER UNITED
Premier League (13): 1992-93, 1993-94, 1995-96, 1996-97, 1998-99, 1999-2000, 2000-01, 2002-03, 2006-07, 2007-08, 2008-09, 2010-11, 2012-13.
FA Cup (5): 1989-90, 1993-94, 1995-96, 1998-99, 2003-04.
League Cup (4): 1991-92, 2005-06, 2008-09, 2009-10.
Charity/Community Shield (10): 1990 (shared), 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011.
Champions League (2): 1998-99, 2007-08.
European Cup Winners' Cup (1): 1990-91.
European Super Cup (1): 1991.
Intercontinental Cup (1): 1999.
FIFA Club World Cup (1): 2008
.
TASWIRA: LWAKATARE AKIWA MAHAKANINI LEO AMBAPO KAFUTIWA MASHITAKA YOTE YA UGAIDI
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo imemfutia mashitaka mawili ya ugaidi, Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Bw. Wilfred Lwakatare.
Jaji aliyekuwa akiendesha shauri hilo, Lawrence Kiduri, amemfutia Lwakatare mashitaka hayo na kumbakizia kosa la kujaribu kumwekea sumu, Mhariri wa gazeti la Mwananchi, Dennis Msaki, ambalo dhamana yake iko wazi.
Akizungumza na GPL, wakili wa mshitakiwa huyo, Peter Kibatara, amesema wanatarajia kumtoa kwa dhamana mteja wake huyo siku ya Jumatatu ambayo anaamini kuwa taratibu zote zitakuwa zimekamilishwa.
CHANZO PICHA&MAELEZO: GLOBAL PUBLISHERS
Lwakatare akimkumbatia kwa furaha wakili wake, Peter Kibatara, baada ya kufutiwa mashitaka ya ugaidi.
Askari wakimuamuru Lwakatare kuondoka kizimbani kwa ajili ya safari ya gerezani.
Akiwaonyesha wafuasi wake alama ya ushindi wa chama chao.
Ndugu, jamaa na wafuasi wa Chadema wakikumbatiana kwa furaha.
Mmoja wa wanachama wa Chadema akiwapigia simu wenzake kuwapasha kilichojiri mahakamani.
Ulinzi nje ya jengo la mahakama.
Wafuasi wa Chadema wakitoka mahakamani kwa furaha.
Kibatara akifafanua jambo kutoka kwenye makabrasha yake
Lwakatare akirudishwa rumande kwa kosa moja la kutaka kumwekea sumu, Dennis Msaki.
TASWIRA: ZIARA YA MBOWE JIJINI ARUSHA KUNANI WAFIWA NA KUFARIJI WAHANGA WA TUKIO LA BOMU KATIKA KANISA KATOLIKI ARUSHA
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, ambae pia ni Mbunge wa Hai na kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzania Bungeni Mh Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari jana jioni katika uwanja wa hospitali ya Mt Meru mara baada ya kutembelea kuwapa pole majeruhi wote waliolazwa katika hospitali hiyo kutokana na majeraha ya yaliyosababishwa na mlipuko wa bomu la kurushwa kwa mkono katika kanisa la Mt Joseph Mfanyakazi-Olasiti lililotokea jumapili iliypoita.
Katika mazungumzo yake Mh Mbowe aliwapa pole wote waliofikwa na janga hilo na kuwataka watanzania wote wawe watulivu huku vyombo vya dola vikifanya kazi yake lengo likiwa ni kuwapata wahusika na ijulikane hasa lengo lao kulipua bomu kanisani lilikuwa ni nini. Baada ya kutoka hopsitalini hapo Mbowe na msafara wake walielekea Elerai kuhani msiba mmojawapo.
Waumini wa Kikatoliki wakimsikiliza Mh Mbowe (haonekani pichani) wakati alipofika kanisani hapo kuwapa pole.
Mh Mbowe akihutubia waumini wa Kanisa Katoliki Mt Joseph – Olasiti jana. Aliyemshikia kipaza sauti ni Mbunge wa Arumeru Mashariki, Mh Joshua Nassari.
Mb Mbowe akipatiwa maelekezo namna siku ya shambulio hali ilivyokuwa na Padri Festus Mangwangi wa Kanisa la Mt Josephat Mfanyakazi.Olasiti Arusha
Mh Mbowe akiwa ndani ya kanisa hilo
Padri Festus Mangwangi akielekeza mahali bomu lilipoangukia na namna watuwalivyojiokoa. Mbowe katika msafara wake aliambatana na wabunge wa chama hicho kwa majimbo ya Arusha Mjini na Arumeru Mashariki, pamoja na viongozi wa juu wa chama na Kanda ya Kaskazini.
Mh Mbowe akiondoka eneo la kanisa mara baada ya kuzungumza na mapadri na waumini
Mbowe na viongozi wengine wa chama na wabunge wakisubiri kuruhusiwa kuingia eneo la kansia ambalo muda huo kulikuwa na ulinzi mkali kusubiri ujio wa Rais Kikwete
Wafuasi na viongozi wa Chadema Arusha wakimsubiria Mwenyekiti wao Mbowe katika geti la wanaowasili uwanja mdogo wa ndege Arusha.
Mbowe akiwasili uwanja mdogo wa ndege Arusha mchana wa jana na kulakiwa na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Mbunge wa Arumeru Mashariki, Mh Joshua Nassari, Katibu wa Chadema Arusha na Kanda ya Kaskazini, Mh Amani Golugwa na Mwenyekiti wa Chadema Arusha Mh Samson Mwigamba.
Chritopher Mbajo, wa Chadema Same anayefanya shughjuli zake Arusha akimtambulisha Mh Mbowe kwa makamanda waliokusanyika nje ya uwanja mdogo wa ndege Arusha kwa ajili ya kumpokea
Mh Mbowe akimjulia hali Apolinary Malamsha aliyelazwa hospitali ya St Elizabeth. Hospitali hiyo ina majeruhi 20 na baadhi yao bado wana vyuma vya bomu mwilini.
Mbowe akizungumza na daktari wa hospitali ya St Elizabeth ya jijini Arusha
Mbowe akimjulia hali mtoto aliyejeruhiwa na bomu na kulazwa hospitali ya Mt Meru.
Mbowe akimfariji majeruhi Samwel Pius aliyelazwa hospitali ya St Elizabeth
Mjeruhi mwingine hopitali ya Mt Meru
Mh Mbowe akisalimiana na wauguzi wa hospitali ya St Elizabeth
Mh Mbowe akisaini kitabu cha wageni hospitali ya St Elizabeth
Mh Mbowe katika ukumbi wa VIP uwanja mdogo wa ndege Arusha
Mh Mbowe akizongwa na kina mama waliokuwa na shuku ya kumshika tu mkono alipozuru hopitali ya Mt Meru
Kamanda wa Chadema Jijini Arusha maarufu kama Omar Matelephone akiwa na wenzake uwanja wa ndege Arusha. Mh Mbowe alipokelewa na msafara wa magari 30 chini ya usimamizi wa Omary na mtu mwingine aliyetambulishwa kama Magoma Derick Magoma
Mh Mbowe na viongozi wa chama (CHADEMA) katika ofisi ya chama hicho.
TAMKO LA BAKWATA JUU YA MLIPUKO KANISANI ARUSHA
Assalaam alaykum warahmatullahi wabarakaatuh.
Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania BAKWATA, limepokea kwa masikitiko makubwa tukio la kurushwa bomu Kanisani na kusababisha upotevu wa maisha na majeraha kwa watu wengi wakati wa sherehe ya uzinduzi wa jengo la Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Orasiti, Arusha.
Kimsingi hili ni jambo la kusikitisha, kukera na kufadhaisha sana kutokea hapa nchini. Watanzania kwa miaka mingi, tumezoea hali ya utulivu na amani na tukio kama hili ni changamoto kwa usalama wa Watanzania wote nchi nzima Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania BAKWATA linalaani kitendo hicho cha kikatili na inaviomba vyombo vya dola kufanya jitihada zote kuhakikisha wahusika wanakamatwa na wanachukuliwa hatua, kwani msiba huu ni wetu sote, Waislamu, Wakristo na Watanzania wote.
Kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania mimi Sheikh Issa Bin Shaaban Simba Mufti wa Tanzania nawapa pole wafiwa wote katika tukio hilo na kuwaombea dua majeruhi na Mwenyezi Mungu (SW) awape tahfif na wapone haraka na kurudi katika shughuli zao za kila siku.
Wabillahi Tawfiiq.
SHEIKH ISSA BIN SHAABAN SIMBA.
MUFTI NA SHEIKH MKUU WA TANZANIA BARA.
AICC YATOA MSAADA WA MAGODORO 30 YENYE THAMANI YA TSH.3.7 MILIONI KATIKA HOSPITALI YA MOUNT MERU ILI KUWAHUDUMIA VEMA MAJERUHI WA BOMU KANISANI
Afisa Itifaki Mwandamizi wa Arusha International Conference Center(AICC)Catherine Kilinda(katikati)akimkabidhi moja ya magodoro 30, Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa wa Arusha,Josiah Mlay leo ikiwa ni sehemu ya kusaidia huduma bora za matibabu kwa walioathirika na mabomu
Afisa Itifaki Mwandamizi wa Arusha International Conference Center(AICC)Catherine Kilinda(wa pili kulia)akipongezwa na muuguzi Mkuu wa hospitali ya mkoa wa Arusha,Mwamini Nyakwela baada ya kukabidhi moja ya magodoro 30,kwa Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa wa Arusha,Josiah Mlay leo ikiwa ni sehemu ya kusaidia huduma bora za matibabu kwa walioathirika na mabomu,kulia ni Matron wa hospitali hiyo,Getrude Andarson
Afisa Itifaki Mwandamizi wa Arusha International Conference Center(AICC)Catherine Kilinda akimsikiliza Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya mkoa wa Arusha,Josiah Mlay leo baada kukabidhi msaada wa magodoro ikiwa ni sehemu ya kusaidia huduma bora za matibabu kwa walioathirika na mabomu
PICHA NA MAELEZO: FILBERT RWEYEMAMU
VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO ALHAMISI MEI 9, 2013
NEWS UPDATES: SHEIKH PONDA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA NJE, DR KAFUMU ARUDISHIWA UBUNGE WAKE WA IGUNGA
Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar Es Salaam, imemfunga kifungo cha nje cha mwaka mmoja Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda, huku washtakiwa wengine wote 49 wakiachiwa huru. Chanzo: Jamii Forums
Mahakama ya Rufaa imemrudishia Ubunge DK. DALALY PETER KAFUMU (kulia pichani)
Awali Mahakama Kuu Kanda ya Tabora ilimvua Ubunge Dk. Kafumu baada ya madai ya kukiuka utaratibu wa Uchaguzi wakati wa Kampeni katika Kesi iliyofunguliwa na Mwl. Joseph Kashindye aliyekuwa Mgombea kwa tiketi ya Chadema.
SPIKA ANNA MAKINDA AONGOZA WABUNGE KUWATEMBELEA WAHANGA WA MABOMU,WAGONJWA NANE WAKIMBIZWA MUHIMBILI NA NDEGE YA TANAPA
Spika Ana Makinda akiwa na Mbunge Urambo mkoani Tabora,Profesa Juma Kapuya leo wakiwasalimia wagonjwa waliopatwa na janga la mabomu kanisani jumapili
Wabunge James Mbatia(mwenye tai)na Mh.Arfi wakijulia hali mgonjwa katika hospitali ya Mount Meru
Mmoja wa wagonjwa nane waliosafirishwa leo kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi
PICHA NA MAELEZO: FILBERT RWEYEMAMU
Rais Kikwete awatkaa wanajeshi wanaokwenda DRC,kuilinda heshima ya Tanzania
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi bendera kiongozi wa batalioni ya wanajeshi wa JWTZ wanaokwenda kujiunga na jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
katika sherehe za kuwaaga zilizofanyika Msangani, Kibaha, Mkoa wa Pwani leo Mei 8, 2013.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wanashuhudia.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtakia kila la heri kiongozi wa batalioni ya wanajeshi wa JWTZ wanaokwenda kujiunga na jeshi la Umoja wa Mataifa kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,katika sherehe za kuwaaga zilizofanyika Msangani, Kibaha, Mkoa wa Pwani leo Mei 8, 2013.Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange wanashuhudia.
PICHA NA IKULU.
Wanajeshi wa Tanzania wanaokwenda kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wametakiwa kudumisha utamaduni wa askari wa kulinda amani wa Tanzania katika maeneo mbali mbali duniani kwa kuifanya kazi hiyo kwa heshima, nidhamu na utii ili kulinda heshima yao wenyewe na ile ya Tanzania.
Askari hao wamekumbushwa utamaduni huo wa askari wa kulinda amani wa Tanzania katika maeneo mbali mbali duniani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais na Amiri Jeshi Mkuu alikuwa akiwaaga wanajeshi wa Tanzania wanaokwenda kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa katika DRC katika hafla iliyofanyika leo, Jumatano, Mei 8, 2012, kwenye Makao Makuu ya Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu la Tanzania yaliyoko Msangani, Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani.
Akizungumza na askari hao, Rais Kikwete amewaambia kuwa hana wasiwasi kuhusu uwezo wao wa kutelekeza majukumu yao yanayowapeleka DRC isipokuwa tu kwamba waifanye kazi hiyo vizuri na kulingana na utamaduni wa majeshi ya kulinda amani ya Tanzania katika sehemu mbali mbali duniani.
“Tunakwenda kutelekeza majukumu ya Umoja wa Mataifa, sina shaka kuwa majukumu yenu mnayaelewa vizuri. Kazi yetu ni kulinda amani na wala hatuendi kupigana na yoyote. Kazi ya kijeshi mnaijua vizuri vile vile na kwa hili pia sina wasiwasi hata kidogo,” amesema Amiri Jeshi Mkuu na kuongeza:
“Kubwa ambalo lazima tulikumbuke ni kwamba nchi yetu kila ilikopeleka majeshi ya kulinda amani imejenga utamaduni wa pekee. Imejenga utamaduni wa askari wetu kuifanya kazi ya kulinda amani kwa heshima, kwa nidhamu na kwa utii wa kiwango cha juu. Hii ni heshima kwetu binafsi na heshima kwa taifa letu. Nawashukuruni na nawatakie kila la heri”
Kama ishara ya kuagana na askari hao, Rais na Amiri Jeshi Mkuu amemkabidhi Bendera ya Taifa Luteni Kanali Orestess Cassian Komba, Kamanda wa Kikosi cha Tanzania katika DRC ambacho kitajulikana kwa jina la TANZBATT 1-DRC, akimwambia “Bendera na Ikapepee”.
Katika jukumu la kulinda amani Mashariki mwa DRC, Kikosi cha Tanzania chenye askari 1281, kitajiunga na vikosi vya Malawi na Afrika Kusini ambavyo vyote vitakuwa chini ya Kamanda wa Brigedi hiyo, Brigedia Jenerali James Mwakibolwa wa Tanzania pia. Kundi la kwanza la askari hao Tanzania linaondoka nchini kesho.
Majeshi hayo ya Tanzania yatalinda amani katika DRC chini ya Azimio Nambari 2098 (2013) la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
8 Mei, 2013
MAJINA YA WATUHUMIWA WANAOHOJIWA JUU TUHUMA ZA KULIPUA BOMU KANISANI ARUSHA HAYA HAPA!
Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha,Liberatus Sabas. PIcha na Filbert Rweyemamu
Arusha
Jeshi la Polisi linawashikilia na kuwahoji watuhumiwa 12 wanaodhaniwa kuhusika na tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olasiti jijini Arusha jumapili iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari leo,Kamanda wa Polisi mkoani hapa,Liberatus Sabas amesema upelelezi wa awali umekamilika na majalada ya watuhumiwa yamepelekwa kwa Mwanasheria wa serikali kwa hatua zaidi.
Amewataja wanaoshikiliwa na jeshi hilo kuwa ni Victor Ambrose Calist(20),Jeseph Yusuph Lomayani(18)waendesha Bodaboda wakazi wa Kwa Mrombo jijini Arusha, George Batholomeo Silayo(23)mfanyabishara na mkazi wa Olasiti,Arusha,Mohamed Sulemani Said(38)Mkazi wa Ilala,Dar es Salaam,Said Abdallah Said(28)raia wa Falme za Kiarabu.
Sabas aliwataja wengine kuwa ni Abdulaziz Mubarak(30)mkazi wa Abudhabi,raia wa Saudi Arabia,Jassini Mbaraka(29)mkazi wa Bondeni jijini Arusha,Foud Saleem Ahmed(28)mkazi wa Falme za kiarabu na Said Mohsen mkazi wa Najran,Falme za Kiarabu ambao bado wanaendelea kuhojiwa.
Wakati huo huo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ameahidi kutoa kiasi cha Sh 50 milioni kwa atakayetoa taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa waliofanya kitendo hicho cha kigaidi.
VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO IJUMAA MEI 10, 2013
CHANZO: MJENGWA.COM
Taswira: Tukio lililowakutanisha ‘mahasimu’ Lema na Mulongo
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh Lazaro Nyalandu (mwenye shati jeupe) akiwa na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema, na Mkuu wa mkoa wa Arusha Maggesa Mulongo wakati wakikabidhi misaada ya kibinadamu kwa wahanga wa bomu kwa Daktari wa hospitali ya St.Elizabeth jijini Arusha juzi Mei 8, 2013 hospitalini hapo. Picha na Mitandao
SHANGWE ZA KUACHIWA KWA SHEIKH PONDA JANA
Katibu wa Jumuia za Taasisi za Kiisalamu Tanznania, Sheikh Ponda Issa Ponda akifanya mahubiri katika Msikitini wa Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam, alipokwenda leo baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kumwachia huru jana, yeye na wenzake 49 waliokuwa wanakabiliwa na shitaka la uchochezi.
Askari wa Magereza akimfungua pingu Katibu wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu Tanzania leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu., ambapo leo yeye na wenzie 49 wameachiwa huru ila watatumikia kifungo cha nje cha mwaka mmoja. PICHA ZOTE NA KHAMIS MUSSA
Askari wakiwa kwenye msafara wa kumsindikiza Sheikh Ponda baada ya kuachiwa.
Sheikh Ponda akiswali katika Msikitini wa Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam.
Wafuasi wa Sheik Ponda wakimshangilia alipokuwa akihutubia ndani ya Msikiti wa Mtambani.
Sheikh Ponda akiswali katika Msikitini wa Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam.
PICHA ZOTE: RICHARD MWAIKENDA
UFAFANUZI KUHUSU KUPITIWA UPYA KWA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012
DR. SHUKURU KAWAMBWA
Mnamo tarehe 03 Mei, 2013 Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Wiliam Lukuvi (Mb) ilitoa Kauli ya Serikali Bungeni Kuhusu Taarifa ya Awali ya Tume ya Taifa ya Kuchunguza Sababu za kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa Kidato cha Nne Mwaka 2012. Kauli ya Serikali ilielekeza kuwa matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2012 yafutwe na yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011 ili Wanafunzi hao wawe katika mazingira yanayofanana na ya wenzao wa miaka iliyopita kwa kuwa mfumo uliotumika mwaka 2012 katika kupanga matokeo na madaraja ni tofauti na ule uliotumika mwaka 2011 na miaka iliyotangulia.
Kwa kuzingatia mapendekezo ya Tume na Maelekezo ya Baraza la Mawaziri, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Baraza la Mitihani Tanzania, kifungu cha 20, sura 107 ameliagiza Baraza la Mitihani la Taifa kupitia upya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012. Aidha, imeagizwa kwamba matokeo hayo yaandaliwe kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011. Serikali haikuagiza kufanyika upya kwa mitihani hiyo na wala haikuagiza kusahihishwa upya.
Hivyo, Serikali inapenda kuwahakikishia wananchi kwamba hapatakuwa na zoezi la kurudia usahihishaji wa mtihani huo kwa sababu hakuna dosari zilizobainishwa kwenye usahihishaji wa mitihani hiyo. Alama za watahiniwa ambazo zimehakikiwa zipo tayari, kitakachofanyika ni kwa Baraza la Mitihani kutumia alama hizo kuchakata matokeo upya kwa kutumia viwango vya ufaulu vilivyotumika mwaka 2011. Utaratibu ambao umekuwa ukitumika tangu mwaka 1973 wakati Baraza lilipoanzishwa, ni wa kuweka viwango vya ufaulu kila mwaka kwa kuzingatia ufaulu wa somo husika na ufaulu katika mwaka uliotangulia.
Kutokana na maelezo hayo, ni dhahiri kuwa zoezi la kupitia upya matokeo ya Kidato cha Nne 2012 litachukua muda mfupi na matokeo yatatangazwa hivi karibuni.
Selestine Gesimba
KAIMU KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
10/05/2013
YALIYOANDIKWA NA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MEI 11, 2013
Taswira: CHADEMA Wakiendesha mafunzo kwa wanachama wake 81 ambao wanatoka katika Majimbo 27 ya Uchaguzi katika Kanda ya Nyanda za Juu kusini, Jijini Mbeya jana
Chama Cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA) kimeendesha mafunzo kwa wanachama wake 81 ambao wanatoka katika Majimbo 27 ya Uchaguzi katika Kanda ya Nyanda za Juu kusini Mafunzo yanayofanyika Katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden City ya Jijini Mbeya.
Mkurugenzi wa Mafunzo na Organaizesheni wa Chadema Taifa Singo Bensoni alisema Lengo la Mafunzo hayo ni kuhakikisha wanapata wakufunzi 30606 nchi nzima ambao watatawanyika katika kila kitongoji nchi nzima kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi na kuunda matawi ya Chama hicho ikiwa ni pamoja na kukifikishama hadi ngazi ya Chini.
Alisema mafunzo hayo yalianza kutolewa kwa kuchukua wakilishi watatu kila Jimbo la Uchaguzi ambao baada ya kumaliza watafanya mitihani na kufuzu kuwa wakufunzi wa chama na kuongeza kuwa mbinu itakayotumika ni kuendesha mafunzo ya chini kwa chini bila kuvaa sare za chama wa kutumia magari ya matangazo na vipaza sauti.
Aliongeza kuwa katika mafunzo hayo yanahusisha wawakilishi wawili kila kanda ambao waliungana na wanachama wengine 10 wa Kitaifa ambao jumla walikuwa 30 ambao baada ya kufuzu mafunzo walirudi kufundisha katika kanda zao ambapo katika Kanda ya Mbeya ina wanafunzi 81,Arusha 96, Mwanza 72 na Shinyanga 60 ambao wanawakilishwa na watu watatu kila Jimbo la Uchaguzi.
Aidha alisema mafunzo hayo yanatolewa kutokana na ufadhili wa watu wa Ujerumani na kwamba wakufunzi hao watapewa Miezi miwili kuhakikisha wameyafikia maeneo yote nchini na kufanikiwa kuwapa elimu wananchi wapatao 30 kwa Mtu mmoja na kuunda Msingi tayari kwa maandalizi ya Uchaguzi mkuu ujao.
Mkurugenzi wa Mafunzo na Organaizesheni wa Chadema Taifa Singo Bensoni alisema Lengo la Mafunzo hayo ni kuhakikisha wanapata wakufunzi 30606 nchi nzima ambao watatawanyika katika kila kitongoji nchi nzima kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi na kuunda matawi ya Chama hicho ikiwa ni pamoja na kukifikishama hadi ngazi ya Chini
CHANZO: MBEYA YETU BLOG
TASWIRA: MAZISHI YA WATU WALIOLIPULIWA NA BOMU KANISANI ARUSHA
Maaskofu wakiombea miili ya marehemu Regina Loning'o Laizer ,James Gabriel Kessy na patricia Assey kabla ya kuingizwa kanisani tayari kwa ibada ya mazishi iliyofanyika katika kanisa la mtakatifu josephy mfanyakazi lililopo katika kata ya olasiti mjini hapa ambapo marehemu hawa ambao walifariki dunia may 5 wakati wakisali katika ibada ya uzinduzi wa kanisa ambapo mtu asiyejulikana alirusha bomu wamezikwa nje ya kanisa hilo. Picha hii imepigwa na Woinde Shizza
Majeneza yakiwa kanisani kabla ya ibada ya mazishi
Mapadri wakiwa wamebeba moja ya majeneza
Watawa wakiwa kanisani wakati wa ibada
Viongozi wa Kanisa wakitoa salamu za mwisho
Kilio kilio kilio anamlilia mama yake mzazi
Wananchi wakitoa salamu zao za mwisho kwenye kanisa katoliki
Majonzi na uchungu
Wahudumu wakishusha mwili wa marehemu kaburini kwenye viwanja vya Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olasiti jijini Arusha
Wahudumu wakishusha mwili wa marehemu kaburini kwenye viwanja vya Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olasiti jijini Arusha
Baadhi ya maaskofu kutoka majimbo mbalimbali waliohudhuria ibada ya mazishi leo
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania(KKKT)Dk Alex Malasusa(kushoto)akiwa na viongozi wengine wa Kanis a hilo wakiwa kwenye ibada ya mazishi
Umati wa watu waliohudhuria maziko hayo
Waziri Mkuu mstaafu,Edward Lowassa(kulia)akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani,Dk Emmanuel Nchimbi kabla ya ibada kuanza. Kuanzia picha ya pili: Filbert Rweyemamu
Waziri wa Mambo ya ndani, Dk Emmanuel Nchimbi akiweka shada la maua kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliyeondoka kabla ya zoezi hilo kufanyika, katika ibada ya mazishi ya waumini waliokufa baada ya kulipuliwa na blomu katika Kanisa la Katoliki la Mt Josephat Mfanyakazi – Parokia ya Olasiti, Arusha.
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho kwa moja ya miili hiyo.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe akiweka shada la maua katika moja ya makaburi hayo.
Majeneza yenye miili ya marehemu ikiwa kanisani tayari kuombewa. Marehemu hawa walifariki katika mlipuko wa bomu katika Kanisa la Mt Josephat Mfanyakazi – Parokia ya Olasiti, Arusha wakati ibada ikiwa ineendelea.
PICHA NA SEIF MANGWANGI, FILBERT RWEYEMAMU NA WOINDE SHIZZA
SHAFFIH DAUDA MATATANI BAADA YA MTANDAO WAKE KUTOA BARUA HALISI YA FIFA KWENDA TFF
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtaka Shaffih Dauda ambaye ni mmiliki wa tovuti ya www.shaffihdauda.com kutoa maelezo kuhusiana na barua ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) aliyoiweka kwenye mtandao wake huo.
FIFA ambayo ilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa TFF baada ya baadhi ya wagombea kuulalamikia, baadaye ilitoa maelekezo kuhusu mchakato huo kwa barua ambayo iliituma kwa Rais wa TFF, Leodegar Lenga.
Rais wa TFF katika mkutano wake na waandishi wa habari ambao Dauda alihudhuria alibainisha kuwa barua hiyo ya FIFA hawezi kupewa kila mtu, na kuruhusu waandishi kuisoma kwa Ofisa Habari wa TFF bila kuondoka nayo.
Wakati Rais Tenga anazungumza na waandishi wa habari (Mei 2 mwaka huu), nakala ya barua hiyo ya FIFA ilikuwa kwa viongozi wakuu wa TFF pekee, na viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Hivyo TFF imemtaka Dauda kutoa maelezo ya mahali alipoipata barua hiyo ndani ya siku saba.
SOURCE: SHAFFIHDAUDA.COM