Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha Mh Amani Golugwa akihutubia wananchi wa Namanga Wilaya ni Longido jana baada ya kumpokea aliyekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Arusha ambaye alihamia rasmi Chadema na kupokelwa katika kikao cha ndani kabla ya mkutano huo wa hadhara.
Mbunge wa Viti Maalumu CHADEMA, Mh Cecilia Paresso akizungumza na wananchi wa Namanga Wilayani Longido wakati wa Mkutano wa hadhara wa chama chake Wilayani humo kushukuru wananchi kuichagua Chadema katika uchaguzi wa vitongoji na Mitaa mwishoni mwa mwaka jana ambpo pia walitumia nafasi hiyo kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura wakati zamu yao itakapofika.
Kutoka kushoto; Diwani wa Kata ya Levolosi Mh Ephata Nanyaro Mbunge Viti Maalumu Arusha Mh Joyce Mukya wote wa CHADEMA na Mwandishi wa Tanzania Daima Ausha Bi Grace Macha wakifuatilia jambo katika kikao cha ndani kabla ya mkutano wa hadhara wa shukrani baada ya Wilaya ya Longido kuchagua viongozi wengi wa Vijiji na Vitongoji watokanao na Chadema. Wilaya hii ya Longido ndio iliyochagua viongozi wao wengi kupitia Chadema kuliko Wilaya nyingine zenye wakaazi wengi jamii ya Maasai.
Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini Bw Amani Golugwa (katikati)akimpokea kamanda mpya kutoka Longido Bw Thomas ambaye awali alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Arusha. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Arumeru Magharibi Bw Gibson Meseiyaki ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Olturoto kupitia CHADEMA.
Bw Thomas ameeleza sababu za kujiengua kwake kutoka CCM na kujiunga Chadema kuwa ni msukumo aliokuwa nao kwa miaka mingi kuona mabadiliko ya kiuchumi na kijamii Wilayani Londigo. Akifafanua zaidi anasema ameamua kujiunga Chadema kwasababu Longido kuna changamoto nyingi ikiwemo ya ardhi ya malisho, makazi, kilimo, maji n.k ambapo imefikia hadi wananchi kuchomewa nyumba zao na CCM imeshindwa kuitatua na hivyo kuja kwake Chadema atapata jukwaa la kuwasemea wananchi wa Longido tofauti na akiwa CCM ambako sio rahisi kupata jukwaa la kuwasemea walalahoi.
Diwani wa Levolosi, Ephata Nanyaro (kushoto) akifuatilia kwa karibu yanayoendelea kweye kikao cha ndani
Wananchi wa Longido eneo la Namanga wakiwa wamejipanga barababrani kuulaki msafara wa viongozi wa Chadema waliokuwa wageni maalumu kwa mkutano wa shukrani baada ya Chadema kushinda vijiji na vitongoji katika uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana. Katika Mkutano huo viongozi mbalimbali wa chama na wabunge na madiwani wa chama hicho walishiriki kwa pamoja miongoni mwao akiwemo Mwenyekiti Chadema Arusha Amani Golugwa, Diwani Ephata Nanyaro, Diwani Gibson Meseiyaki, Wabunge Viti Maalumu Cecilia Paresso na Joyce Mukya, Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari na James Ole Millya mtia nia Simanjiro
Kamanda wa CHADEMA anayetazamia kupambana na Ole Sendeka Jimbo la Simanjiro, Kamanda James Ole Millya akizungumza na wananchi wa Namanga jana
Joshua Nassari na viongozi wengine wa CHADEMA katika picha ya pamoja na viongozi wa kimila wa jamii ya Maasai waishio Wilayani Longido
PICHA ZOTE NA YEGELLA