Halmashauri ya Mji wa Babati imetoa mikopo zaidi ya sh milioni 150 kwa vijana na kina mama wajasiriamali ili waweze kujikwamua kimaendeleo.
Akisimulia Blogu hii namna zoezi hilo lilivyoanikiwa, Mbunge wa Viti Maalum Babati kupitia CHADEMA, Mh Pauline Gekul, amesema zoezi hilo la utoaji mikopo limefanyika jana katika uwanja wa Qwaraa, Banati Mjini.
Hii niawamu ya pili ya utoaji mikopo ambapo awamu ya kwanza ilikuwa Machi 19 mwaka huu na zaidi ya shilingi milioni 100 zilitolewa kama mikopo kwa vijana na kina mama wajasiriamali ndani ya Halmashauri hiyo.
![]() |