Quantcast
Channel: PolitiksiFactTrack ''ARUSHA255''
Viewing all 1899 articles
Browse latest View live

Dr Ndesamburo afariki ghafla, Daktari aeleza kilichomuua

$
0
0


MSHTUKO.
Ndivyo unavyoweza kusema baada ya aliyekuwa Mbunge wa Moshi Mjini kwa miaka 15, Philemon Ndesamburo, kufariki dunia ghafla jana.

Vilio, huzuni na simanzi vimetanda ndani ya mji wa Moshi na vitongoji vyake, baada ya kusambaa taarifa za kifo cha Ndesamburo maarufu ‘Ndesapesa’.

Ndesamburo ambaye pia ni Mweneyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Kilimanjaro, alifariki dunia baada ya kuanguka ofisini kwake akitekeleza majukumu yake ya kila siku.

Akizungumza na MTANZANIA, mtoto mkubwa wa marehemu, Sindato Ndesamburo, alithibitisha baba yake kufariki dunia.

Sindato alisema baba yake alianguka ghafla ofisini kwake akiwa anatekeleza majukumu yake ya kila siku, japo hakujua mara moja tatizo lililomsibu.

Alisema wamepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa, ikizingatiwa baba yake aliondoka nyumbani asubuhi akiwa mzima wa afya.

 “Kifo hiki kimekuwa pigo kubwa kwa familia nzima, baba yetu alikuwa mzima, asubuhi alitoka nyumbani vizuri kama kawaida yake kuelekea ofisini kwake Keys, baadae tuliambiwa ameanguka ghafla akiwa ameketi kwenye kiti,  inasemekana alifariki dunia papo hapo,” alisema

UCHUNGUZI WA KIFO 

Akizungumzia taarifa za awali za uchunguzi wa kifo hicho, Profesa Elisante Massenga wa HospItali ya Rufaa ya KCMC, alisema walimpokea Ndesamburo akiwa tayari amefariki dunia.

Alisema baada ya mwili wake kufanyiwa uchunguzi wa awali, ilibainika alikuwa na tatizo kubwa kwenye moyo.

“Uchunguzi wa vipimo vingine bado, ila kwa taarifa za awali, kama wataalamu tumebaini alikuwa na shida kubwa kwenye moyo, vipimo vingine vikikamilika tutatoa taarifa rasmi,” alisema.

MBOWE

Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, alielezea namna Ndesamburo alivyofariki dunia.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Mbowe alisema kabla ya kufariki, Ndesamburo alikuwa anajiandaa kusaini hundi ya fedha za rambirambi za wanafunzi waliofariki katika ajali ya basi la Shule ya Lucky Vincent mwanzoni mwa mwezi huu, wilayani Karatu, Mkoa wa Arusha.

“Nimewaita hapa kuwathibitishia juu ya taarifa za kifo cha mwasisi wa chama chetu, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, mjumbe wa Kamati Kuu na mbunge wa vipindi vitatu katika Jimbo la Moshi Mjini, mzee wetu, Philemon Ndesamburo, kilichotokea leo (jana) saa 4.45 asubuhi.

“Chadema tumepokea taarifa za kifo hicho kwa mshtuko mkubwa kwa sababu mzee Ndesamburo alikuwa ni nguzo, alikuwa msaada kwa chama chetu na alikuwa msaada kwa wabunge pia.

“Juzi, alikuwa hapa Dodoma kwenye kikao cha Baraza Kuu, tulipomaliza alirudi nyumbani kwake Moshi ambako jana jioni alimpigia simu Meya wa Jiji la Arusha, Lazaro na kumuuliza waliofariki kwenye ajali ya basi la Lucky Vincent ni wangapi.

“Meya akamwambia ni watu 35, kwa hiyo, akamwambia leo saa tatu asubuhi (jana), meya aende Moshi Mjini ili amkabidhi fedha za rambirambi Sh milioni 3.5 kwa sababu alisema angechanga shilingi laki moja kwa kila familia ya mfiwa.

“Kwa bahati mbaya, meya hakufika saa tatu kama walivyokubaliana na badala yake alifika saa nne. Hivyo basi, waliingia ofisini kwake na mazungumzo yakaanza. Wakati mazungumzo yakiendelea, mzee Ndesamburo alichukua kalamu ili aandike cheki ya rambirambi hizo na kabla hajaijaza, kalamu ikamdondoka mkononi, na hapo akaanza kulegea.

“Meya alipoona hivyo, akamuuliza ‘mzee uko salama’, naye akajibu ‘niko salama’. Pamoja na kusema yuko salama, mzee alizidi kulegea. Kwa hiyo, meya alinyanyuka na kumfuata na alipoona hali inazidi kuwa mbaya, akawaita wahudumu wa pale hotelini kwa mzee, Keys Hotel maana ndiko walikokuwa.

“Wahudumu walipofika, walishirikiana na meya kumchukua na kumkimbiza Hospitali ya KCMC kwa matibabu, ambako aliwekewa mashine ya oxygen kumsaidia kupumua. Lakini baada ya nusu saa tangu alipopokewa, madaktari walitoa taarifa kwamba mzee amefariki dunia,” alisema.

MWENYEKITI WA BUNGE

Wakati Mbowe akisema hayo, Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, aliliambia Bunge jinsi alivyopata taarifa za msiba huo, muda mfupi kabla ya mtoto wa marehemu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Owenya (Chadema), hajachangia bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa fedha 2017/18.

“Waheshimiwa wabunge, nina tangazo hapa la tanzia ambalo nimelipata muda si mrefu kutoka kwa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, mheshimiwa Freeman Mbowe.

“Aliyekuwa Mbunge wa Moshi Mjini kwa vipindi vitatu kuanzia mwaka 2000 hadi 2015, Philemon Ndesamburo, amefariki dunia leo asubuhi saa 4.45.

“Wakati napata taarifa hizi, binti wa marehemu alikuwa ameomba kuchangia, lakini nikaruka jina lake makusudi na mmesikia alivyolalamika hapa, ndipo nikalazimika kumruhusu achangie.

“Kwa hiyo, mipango ya mazishi tutaendelea kujulishana kwa sababu huyo mzee tulikuwa naye hapa kwa miaka mingi,” alisema Chenge.

IKULU

Naye Rais Magufuli amesema amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Ndesamburo.

Taarifa ya Ikulu iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana, ilisema Rais Magufuli alieleza namna alivyomfahamu Ndesamburo kutokana na kufanya naye kazi wakati wote wakiwa wabunge.

Alisema kuwa walishirikiana, kutaniana na anamkumbuka kwa namna ambavyo alitumia muda wake bungeni kupigania mambo yenye masilahi kwa wananchi wa jimbo lake.

Rais ameitaka familia ya marehemu Ndesamburo na wote walioguswa na msiba kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu.

CHADEMA KILIMANJARO

Akizungumzia kifo hicho, Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro, Basili Lema, alisema chama kimepokea kwa masikitiko makubwa kifo hicho na ni pigo ambalo kamwe halitazibika.

Alisema Ndesamburo amekuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa zaidi ya miaka 20, alikilea kwa nguvu na mali zake kama baba.

“Chadema tumepata pigo kubwa, Ndesamburo alikuwa baba kwetu, alilea chama vema na siasa zake zilikuwa si kutetea masilahi yake binafsi, bali masilahi ya wananchi wa Jimbo la Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro na taifa kwa ujumla,” alisema Lema.

MEYA WA MOSHI

Meya wa Mji wa Moshi, Raymond Mboya, alisema Ndesamburo alianguka ghafla akiwa ofisini kwake, wakati akiandika hundi ya Sh milioni 3.5 kutoa rambirambi yake kwa vifo vya wanafunzi 32 wa Shule ya Lucky Vincent ya mkoani Arusha iliyotokea hivi karibuni.

“Akiwa ofisini kwake na Meya wa Jiji la Arusha, Calisti Lazaro akisaini hundi ya rambirambi, ghafla alianguka, alipokimbizwa Hospitali ya KCMC alikutwa tayari amefariki dunia. Hili ni pigo kwetu, alitulea vijana kwenye maadili mema ya kisiasa,” alisema.

NATSE

Aliyekuwa Mbunge wa Karatu, Mchungaji Israel Natse (Chadema), alisema kifo hicho kimekishtua chama na taifa zima.

Aliwataka wana familia na jamii nzima kutafakari kwa kina juu ya kifo hicho na kuiga mfano wa mambo yote aliyofanya Ndesamburo, ikiwa ni pamoja na kuishi vema na jamii.

ZITTO KABWE

Naye Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, ametuma salamu za rambirambi kutokana na kifo hicho.

“Ni msiba mzito kwa watu wa Kilimanjaro, hasa Moshi Mjini. Ndesapesa alikuwa mwakilishi wao bungeni kuanzia mwaka 2000 hadi 2015, Kilimanjaro imepoteza mtu ambaye aliweka masilahi ya mkoa wake mbele kuliko kitu kingine chochote,” aliandika Zitto katika ukurasa wa Facebook.

WANANCHI

Nao baadhi ya wananchi wa mjini hapa,  wakizungumza kwa nyakati tofauti, walisema Ndesamburo alikuwa miongoni mwa wanasiasa wanaopaswa kuigwa kutokana na namna alivyoendesha siasa zake bila kuwa na chuki wala kinyongo na mtu au chama kingine.

Teresia Urio, alisema enzi la utawala wake, Ndesamburo alijitahidi kuhakikisha jimbo lake linakuwa tofauti na majimbo mengi.

Aliweza kuwafundisha wananchi wake kuendesha siasa kwa hali ya amani na utulivu.

“Kwa namna alivyotulea Ndesamburo, ni vigumu kuona Moshi kuna maandamano au uvunjifu wa namna yoyote ile wa amani zinazotokana na siasa, licha ya jimbo hili kuwa la upinzani tangu mfumo wa vyama vingi ulipoingia nchini mwaka 1992,” alisema Wilson Kusekwa.

WASIFU WAKE

 Ndesamburo alizaliwa Februari 19, 1935.

Alikuwa Mbunge wa Moshi Mjini tangu mwaka 2000 na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro.

 Desemba mwaka jana, alitunukiwa PhD ya heshima ya utu (Doctor of Humanity na chuo Kikuu cha Biblia cha Japan, ambacho kilitambua mchango wake katika medani ya uongozi, hasa kujitolea na kuhudumia wengine pamoja na jitihada zake za kuhubiri amani wakati wote.


YANGA YATUA ARUSHA KWA KISHINDO HUKU IKIWA NA KOMBE LAKE

$
0
0


picha na maktaba
Na Woinde Shizza,Arusha

Kikosi cha Afc Arusha kimejinasibu kuwa kitawafunga mabigwa wa ligi kuu bara msimu uliomalizika  Timu ya  Yanga Afrika,katika mchezo wao wa kirafiki unaotajarajiwa kupichezwa Jumapili hii  May 28 katika kiwanja cha kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini hapa


Akiongea na gazeti hili kocha wa kikosi hichi kipya cha timu ya AFC Fikiri Elias  alisema kuwa vijana wake wapo tayari kuwapatia burudani wapenzi wa ke wa soka mkoani hapa huku akiwapa sifa viongozi wa serikali kwa kuwa begakwa bega katika kuhakikisha soka la mkoa wa Arusha linarudi katika ramani yake

Alisema kuwa japo hii ni mechi yao ya kirafiki baina yao na timu ya Yanga lakini watatumia mchezo huu pia kuangalia kikosi bora ambacho kitakaa kambini kwa ajili ya kuandaa timu ya kikosi kitakacho unda AFC mpya itayoshiriki ligi daraja la kwanza .


,, pamoja ya kuwa timu ya yanga inawachezaji wazoefu wengi na pia ndio wametoka tu kutwaa ubigwa mara ya tatu lakini napenda kusema hivi japo mechi hii ni ya kirafiki lakini nimeaada kikosi kizuri nanauhakika lazima tutaifunga timu hii ili tuweke historia japo ni mechi ya kirafiki ,,alisema Fikiri



Kwa upande wake kocha msaidizi  timu ya  Yanga ambao wameshikilia ubigwa  kwa mara ya tatu mfulukizo ligi kuu bara  Juma Mwambusi alisema kuwa mchezo huu ni muhimu  kwao kwani ni moja  ya program zao katika kujiandaa kuelekea katika michuzano inayowakabili  ikiwemo mashindano ya Sport Pesa


Kikosi hichi cha yanga kipo katika ziara ya kutembeza kombe lake kwa mashabiki wa mikoani ambapo mkoa wa Arusha umekuwa wa kwanza kuona kombe hilo na wakitoka mkoani hapa wanampango wa kulipeleka mkoani Dodoma ,ambapo pia wanajangwan hawa wamekuwa ni timu ya tatu kuoka ligi kuu bara msimu ulioisha kutoa katika aridhi ya jiji la Arusha iliyokuwa na ukame wa timu za ligi kuu mara baada ya timu za Ruvu shooting na Simba  zilizowaikutua hapa katika mtanange wake ulioisha



Akizungumzia mchezo huo wa kirafiki  mmoja wawaandaaji wa mechi hiyo ambayo katibu wa timu ya AFC  Charles Mwaimu alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika timu zote zipo tayari wanaisubiri tu siku ya mechi ifike.



Aliwasihi wananchi wa mkoa wa Arusha na pembezoni kujitokeza kwa wingi kuishabikia timuyao ya AFC ikiwa ni ujio mpya wa timu hii mara baada ya kupotea kwa muda ,na aliwasihi wananchi wa mkoa wa Arusha kujitokeza kuwapa morali wachezaji wao .



Aidha alisema kuwa pia mbali na mechi hii ya yanga kucheza na AFC pia wanampango wa timu hii kwenda mkoani manyara kucheza mechi baida yao na timui ya Merirani.


MAZISHI YA NDESAMBURO KUFANYIKA KWA SIKU MBILI MFULULIZO

$
0
0

Kikao cha Wanafamilia,Viongozi wa siasa na Viongozi wa Dini kikifanyika nyumbani kwa marehemu Ndesamburo kwa ajili ya maandalizi ya mazishi yake.
Ndugu na Baadhi ya watoto wa marehemu Philemoni Ndesamburo wakiwa katika kikao hicho.
Baadhi ya Viongozi wa Chadema wakishiriki katika kikao hicho.
Baadhi ya watoto wa marehemu Philemoni Ndesamburo.
Baadhi ya Wabunge wakishiriki katika kikao hicho.
Baadhi ya wanandugu wa familia ya marehemu Ndesamburo.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini

MAZISHI ya Mbunge mstaafu wa jmbo la Moshi mjini na Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro Philemon Ndesamburo Kiwelu (82) yanataraji kufanyika kwa siku mbili mfululilizo huku watu zaidi ya laki 2 wakitaraji kushiriki katika mazishi hayo.

Shughuli nzima za mazisihi zinataraji kufanyika June 5 na sita katika uwanja wa mashujaa mjini Moshi kabla ya kuhitimishwa siku ya Jumanne kwa ibada itakayoanzia kanisani na kumalizikia nyumbani kwa marehemu. 

Hatua ya maziko ya Ndesamburo kufanyika kwa siku mbili inatokana na uwepo wa idadi kubwa ya marafiki wa familia kushiriki katika maziko hayo ya kihistoria yatakayotanguliwa na kutoa heshima za mwisho ,shughuli zilizopangwa kufanyika katika uwanja wa mashujaa mjini Moshi.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichodumu kwa zaidi ya saa nne ,Msemaji wa Chadema katika maandalizi ya mazishi hayo Amani Golugwa amesema uamuzi huo unatokana na kutoa nafasi kwa watu mbalimbali kutoa heshima za mwisho kwa Ndesamburo.

“Tumekua na kikao na wanafamilia viongozi wa chama na mashaurizano kuhusiana na msiba huu ,tumekuwa na watoto wa marehemu ,walikuwepo wachungaji na viongozi wa chama ,kimsini tumekubaliana mazishi ya mze wetu Ndesamburo yatafanyika kwa siku mbili mfululizo”alisema Golugwa.

Kutakuwa na siku mbili za maombolezi,siku ya jumatatu mwezi huu tutakuwa na state funeral (mazishi ya kitaifa) siku ambayo tutafanya kumbukizi ya maisha yake na tunataraji kuwa na idadi kubwa sana ya watu”alisema Golugwa.

Kwa upande wake msemaji wa familia ambaye pia ni motto mkubwa wa marehemu Ndesamburo,Sindato Ndesambur o alisema vikao mbalimbali vinaendelea kwa ajili ya maandalzi ya mazishi na kwamba yanataraji kutanguliwa na maandamano.

“Kama unavyoonabado tunaendelea na vikao kwa sasa ,kuona namna gani tunaweza kumuaga mzee wetu kwa heshima aliyojijengea kwa wakazi wa Moshi na taifa kwa ujumla “alisema Sindato.

Alisema wanatazamia kupokea wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi zikiwemo taasisi mbalimbali za kidini,kiserikali pamoja na wafanyabiashara watakao shiriki katika shughuli nzima ya mazishi .

Mapema jana vilio na Simanzi vilitawala chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ,wakati familia ya Marehemu  Ndesamburo  ikiongozwa na mtoto wake wa  Pili ,Lucy Owenya kushudia mwili wa mpendwa wao ukiwa umehifadhiwa.

Wakati kifo cha Mzee Ndesamburo kinatokea ,Lucy Owenya alikuwa akihudhuria vikao vya  Bunge la 11 ,vikao vya  Bajeti  ambapo alipata nafasi ya kuchangia mjadala wa bajeti ya wizara ya fedha kabla ya kupokea taarifa rasmi ya kifo cha Ndesamburo ambaye pia ni mfanyabiashara mashuhuri.

Majira ya saa 11:45 familia ilifika katika hospitali ya rufaa ya KCMC huku Mbunge wa jimbo la Rombo ,Joseph Selasini akisimamia zoezi la kuomba kuona mwili wa marehemu Mzee Ndesamburo ili kujiridhisha kama kweli baba yao amelala mauti.

Michuzi Blog ililifika KDC nyumbani kwa marehemu Ndesamburo na kushuhudia maandalizi ya shughuli za maziko yakiendelea huku waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali ya pembe ya nchi wakifika kutoa pole kwa familia ya marehemu.

Philemoni Ndesamburo atakumbukwa na mengi hasa katika siasa za mageuzi ambapo katika uchaguzi wa mwaka 2015 akiwa ni mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro alisaidia kupatikana kwa madiwani wengi katika baraza la madiwani wa manispaa ya Moshi.

Ndesamburo maarufu kama Ndesa Pesa ametumia muda wake mwingi katka siasa na biashara ,amefariki dunia wakati akitaka kukabidhi mchango wake kwa meya wa jiji la ARUSHA ,Kalist Lazaro kwa ajili ya familia za watoto wa shule ya msingi ya Lacky Vicent waliofariki katika ajali ya gari Wilayani  Karatu mkoani Arusha.

Mwisho.

UPDATES: MSIBA WA MBUNGE MSTAAFU WA JIMBO LA MOSHI MJINI PHILEMONI NDESAMBURO

$
0
0

Nyumbani kwa Marehemu Mzee Philemoni Ndesamburo aliyefariki dunia jana katika Hosptali ya Rufaa ya KCMC mjini Moshi.
Baadhi ya waombolezaji wakiwemo ndugu wakijiandaa kwenda kutizama mwili wa Mzee Ndesamburo katika HospItali ya Rufaa ya KCMC.
Baadhi ya Waombolezaji wakiwemo Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wakia nyumbani kwa Mzee Ndesamburo.
Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini ,Godbless Lema pamoja na mkewe Neema Lema wakiwasili nyumbani  kwa marehemu Mzee Ndesamburo.
Mbunge wa jimbo la Arusha mjini ,Godbless Lema akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Rombo ,Joseph Selasini mara baada ya kukutana nyumbani kwa marehemu Mzee Ndesamburo .
Mtoto wa Marehemu Ndesamburo ,Ndohorio Ndesamburo akiwaeleza jambo waombolezaji waliofika nyumbani kutoa pole kwa familia.
Mwenyekiti wa Chadema kanda ya Kaskazini,Aman Golugwa akitia saini katika kitabu cha waombolezaji nyumbani kwa marehemu Ndesamburo.
Baadhi ya viongozi wa Chadema wakiwa katika kikao kifupi nyumbani kwa mareheu Ndesamburo.
Familia ya marehemu Ndesamburo wakiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa ajili ya kutizama mwili wa mpendwa wao.
Mkurugenzi wa kampuni ya World Frontier,John Hudson akimfariji ,mtoto wa marehemu Ndesamburo,Lucy Owenya nyumbani kwao eneo la Mbokomu mjini Moshi.
Baadhi ya waombolezaji wakiwafariji wafiwa.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

VIONGOZI WAMIMINIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU DKT PHILEMONI NDESAMBURO KUTOA POLE KWA FAMILIA

$
0
0

Maandalizo ya Mazishi ya marehemu Dkt ,Philemoni Ndesamburo yakiendelea nyumbani kwake KDC mjini Moshi.
Kwaya ikihudumu kwa nyimbo kwa ajili ya kuwafariji wafiwa nyumbani kwa marehemu Dkt Philemoni Ndesamburo.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson akitoa mkono wa pole kwa mama Mjane wa Marehemu Dkt Philemoni Ndesamburo ,Ndehorio Ndesamburo alipotembelea nyumbani kwa marehemu kuifariji familia. 
Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni ,Freeman Mbowe akitoa mkono wa Pole kwa mjane wa marehemu Dkt Ndesamburo ,Ndehorio Ndesamburo nyumbani kwake KDC mjini Moshi.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni ,Freeman Mbowe akitoa mkono wa Pole kwa mtoto wa marehemu Dkt Ndesamburo ,Filomena Ndesamburo nyumbani kwao  KDC mjini Moshi.
Waziri wa Malisili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akitoa pole kwa mama mjane wa marehemu Ndesamburo nyumbani kwake KDC mjini Moshi.
Baadhi ya watoto wa marehemu Philemoni Ndesamburo wakiwa nyumbani kwao.
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi ,David Mathayo David akitia saini katika kitabu cha waombolezaji nyumbani kwa marehemu Dkt Philemoni Ndesamburo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro,Idd Juma akitia saini katika kitabu cha waombolezaji nyumbani kwa marehemu Ndesamburo KDC Mjini Moshi.
Mkurugenzi wa Halmashauri wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) John Mrema akitia saini katika kitabu cha waombolezaji nyumbani kwa marehemu Dkt Ndesamburo KDC mjini Moshi.
Baadhi ya Madiwani wakitia saini katika kitabu cha waombolezaji .
Baadhi ya viongozi waliofika kutoa pole kwa familia ya marehemu Dkt Ndesamburo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mstaafu ,Saidi Meck Sadiki akisalimiana na Mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe walipokutana nyumbani kwa marehemu Dkt Ndesamburo.
Saidi Meck Sadiki akitoa mkono wa pole kwa watoto wa marehemu Dkt Ndesamburo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akisalimiana na mume wa Mbunge wa viti maalumu Lucy Owenya,Dkt Fidelis Owenya alipofika nyumbani wa marehemu Dkt Ndesamburo kutoa salamu za pole.
Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Rombo Joseph Selasini walipokutana nyumbani kwa marehemu Ndesamburo.
Mjane wa marehemu Ndeamburo ,Bi Ndehorio Ndesamburo (mwenye nguo za rangi nyeusi ) akionekana ni mwenye huzuni.
Baadhi ya waombolezaji .
Mwenyekiti wa Chadema Taifa  na Kiongozi  wa kambi rasmi Bungeni ,Freeman Ndesamburo akisalimiana na Askofu wa KKKT Dkt Martin Shoo alipofika nyumbani kwa marehemu Dkt Ndesamburo .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

WAONGOZA UTALII WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KATIKA KUWAPENDEKEZA WATAKOINGIA KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA KUMPATA MUONGOZAJI BORA WA MWAKA 2017

$
0
0

Wa kwanza kushoto ni Muasisi wa Tanzania Tour Guide Awards Sadock Mugetta, aliyepo kushot kwake ni Katibu wa Freelance Guides Society of Tanzania(FGST )anayefuata ni mjumbe wa  wakiwa katika maonyesho ya (3)Utalii ya Kilifair  katika uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro.



Na.Vero Ignatus Kilimanjaro.

 Wito umetolewa kwa waongoza watalii nchini kutoa ushirikiano ,kuwapendekeza watakaoingia katika kinyang'anyiro cha kumtafuta mshindi wa Tuzo ambayo imeandaliwa kwaajili ya kumpata Balozi atakaewawakilisha waongoza utalii nchini Tanzania,Afrika ya Mashariki na Kati .

Akizungumza na blog hii Muasisi na mwenyekiti wa Tuzo hiyo Sadock Mugetta amesema kuwa tuzo  inafahamika kama  TANZANIA TOURGUIDE AWARDS   ambapo mwaka jana ilikuwa imegawanyika   katika vipengele vya kumtafuta muongoza watalii bora wa Mlima,Safari pamoja na Wapagazi,ila mwaka huu wameongeza vipengele viwili ambavyo ni Muongoza utalii wa Utamaduni pamoja na Mpishi bora.

Sadock amesema kuwa wameamua kuwepo kwa Tuzo hiyo kutokana hali halisi iliyopo ya ugumu wa kazi wanayoifanya waongoza watalii (Mabalozi) ili mshindi atakayepatikana atawawakilisha katika mambo yao ambayo wanataka Serikali iyafahamu,pamoja na wageni mbalimbali waitambue Tanzania pamoja na vivutio vya Utalii vilivyopo.

 Ameongeza kuwa tangia kuanzishwa kwa huduma ya  utalii hapa nchini waongoza Watalii  hawajawahi kupewa kipaumbele, hivyo ni vyema Serikali ikatambua kuwa muongozaji watalii huwa  anatumumia 99% ya muda wao  kukaa na mgeni awapo nchini na anapewa taarifa zote sahihi na muhimu  hadi anaondoka nchini. 

"Ikumbukwe kuwa tangia kuanzishwa kwa huduma hii ya utalii waongozaji hawajawahi kupewa kipaumbele wakati anatumia 99%ya muda wake na mgeni akiwa hapa nchini ,anahakikisha mgeni yupo salama,anahakikisha mgeni anapata taarifa zote sahihi hadi anaondoka nchini,muongozaji huyu anafanya kazi yake kama mwalimu,Daktari pale mgeni anapopata taizo anampatia huduma ya kwanza,mpishi,mpatanishi na Balozi mwaminifu".alisema Sadock.

Kwa upande wake Katibu wa Waongoza watalii wa kujitegemea Ally Mtemvu amesema kuwa hakuna mgeni anayekuja nchini kufanya utalii pasipokuwa na muongozajiamesema tuzo hiyo inawashirikishwa makampuni yote ya utalii ,wadau wa utalii KIATO,TATO, pamoja KGA,TTGA,FGST,KTAS,TTG,KILIMERU,TPO,MMPA,NCPG na NMPA

" Hivyo tunaiomba Wizara ya Utalii na Maliasili watuunge mkono kuhakikisha kuwa tuzo hii ya Afrika Mashariki na Kati zinakuwa bora zaidi kwakuwa tumewatangulia na imeasisiwa nchini Tanzania "alisema Ally.

Aidha Tuzo hii ilizinduliwa rasmi mwaka 2016 mkoani Arusha ambapo mgeni rasmi alikuwa Naibu katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Anjelina Madete,ambapo mwaka huu 2017 itafanyika jijini Dar es salaam kwenye maonyesho ya SITE october 13-15,2017 ambapo mgeni rasmi atafahamika hapo baadae.

Mwisho wa mapendekezo ya majina ni tarehe 30/6/2017






WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,PROFESA MAGHEMBE ASEMA MAONESHO YA KILI FAIR YANASAIDIA KUTANGAZA UTALII

$
0
0


Waziri wa Malisili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho ya tatu ya kimataifa ya Utalii yanayofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu Ushirika mjini Moshi.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Devota Mdachi akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho makubwa Afrika Mashariki ya Utalii na Viwanda yanayofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu Cha Ushirika mjini Moshi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB,Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akisalimia wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo.
Mkurugenzi Mwenza wa Kampuni ya Kili Fair inayoratibu maonesho hayo Dominic Shoo akisoma taarifa kuhsu maonesho hayo yanayofanyika wa mara ya tatu sasa .
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba akitoa neno kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho ya Kili Fair yanayojumuisha zaidi ya washiriki 300 kutoka nchi tisa.
Mkurugenzi wa Kili Fair ,Dominic Shoo akimuongoza mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonesho hayo,Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe kutembelea sehemu maonesho katika uwanja wa Ushirika mjini Moshi.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akimsadia Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii,TTB Bi Devota Mdachi kufika katika eneo la mfano wa Kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe ,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi (TTB) Jaji Mstaafu ,Thomas Mihayo,Mkuu wa wilaya ya Moshi Kippi Warioba na viongozi wengine wakiwa katika kilele cha Uhuru cha Mfano kilichopo katika maonesho yanayoendelea katika uwanja wa chuo kikuu cha ushirika mjini Moshi.
Waziri wa Malisili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine mara baada ya kufungua maonesho ya Kili Fair.
Waziri Prof Maghembe akitizama ngoma ya kikundi cha jamii ya Maasai kikitoa burudani katika maonesho hayo.
Bidhaa mbalimbali na zikiwa katika mabanda ya maonesho ndani ya uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi ambako maonesho ya Kili Fair yanafanyika.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

KAMPUNI YA ACACIA YACHANGIA KATIKA HARAKATI ZA GGM KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA MAPAMBANO YA VITA DHIDI YA UKIMWI

$
0
0

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Tulia Ackson akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika lango la kupandia mlima Kilimanjaro,lango la Machame kwa ajili ya kutoa Baraka kwa washiriki wa changamoto ya kupanda mlima kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi zoezi linaloratibiwa na Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM).
Mgeni rasmi katika shughuli ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za mapambano Vita ya Ukiwmwi ,Dkt Tulia Ackson akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mshikizi ,Mrisho Gambo (kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ukimwi na Dawa za kulevya ,Dkt Faustine Ndugulile wakiimba wakipiga makofi.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Tulia Ackson kizungumza wakati wa kutoa baraka kwa wanaharakati 89 wakiwemo wafanyakazi wa Kampuni ya Acacia wanaoshiriki zoezi panda mlima kwa lengo lakuchangisha fedha kwa ajili ya mapambano ,vita dhidi ya Ukimwi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM) Terry Melpeter akizungumza katika shughuli hiyo iliyofanyika katika lango la Machame.
Baadhi ya viongozi wa wilaya za Hai na Moshi mjini wakifuatalia  shughuli hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro mshikizi Mrisho Gambo akizungumza wakati wa shuguli hiyo ambayo hufanyika kila mwaka.
Msanii Mrisho Mpoto ambaye ni Balozi wa TACAIDS akitoa burudani kwa washiriki wa changamoto hiyo.
Kampuni ya Acacia ,wamiliki wa Migodi ya Buzwagi,Bulyanhulu na North Mara ni miongoni mwa kampuni ambazo zimekua zikitoa michango yao kusaidia kampunu ya GGM katika mapambano ya vita dhidi ya Ukimwi ambapo wafanyakazi wake pia ni miongoni mwa wanaharakati waliopanda Mlima Kilimanjaro.
Naibu Spika Dkt Ackson akisalimana na Meneja wa Benki ya NMB,tawi la Moshi ,Emanuel Kishosha kabla ya kuanza kwa zoezi la kupanda mlima Kilimanjaro.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Acacia wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Spika ,Dkt Ackson kabla ya kuanza kwa zoezi la kupanda mlima.
Zoezi la kuapnda Mlima likianza rasi huku likiongozwa na Naibu Spika ,Dkt Tulia Ackson ,Mrisho Mpoto akiongoza kwa nyimbo za kuhamasisha.
Zoezi la kupanda lilianza huku mvua ikinyesha,

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

PICHA ZA TUKIO LA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA HAYATI DK PHILEMON NDESAMBURO UWANJA WA MAJENGO MOSHI LEO

$
0
0

NDESAMBURO AACHA REKODI




Moshi Kilimanjaro. 
Mwili wa mbunge wa zamani wa Moshi Mjini kupitia Chadema (2000-2015), Philemon Ndesamburo jana uliweka rekodi ya aina yake mkoani Kilimanjaro kwa kuagwa na kuhudhuriwa na maelfu ya waombolezaji.
Haijapata kutokea tangu Uhuru wa nchi hii kwa kiongozi kuagwa uwanjani na watu wengi kwani kumbukumbu zinaonyesha wote waliomtangulia ama waliagwa nyumbani kwao au katika makanisa waliyokuwa wakisali.
Awali, Ndesamburo alikuwa aagwe katika Uwanja vya Mashujaa ili kuakisi ushujaa wake wa kuwaletea maendeleo wananchi wa Moshi, lakini Serikali ilizuia.
Hata hivyo, pamoja na kuzuia shughuli ya kufanya kumbukizi na kutoa heshima za mwisho katika uwanja huo na kuhamishia shughuli hiyo katika Uwanja wa Majengo, bado tukio hilo liliutikisa mji wa Moshi.
Mapema jeneza lililobeba mwili wake lilipangiwa kutembezwa katika mitaa na barabara mbalimbali za mji huo, lakini polisi ikazuia ikisema hayo yangekuwa ni sawa na maandamano. Hata jeshi hilo lilipoelekeza msafara huo utoke hospitali ya rufaa ya KCMC hadi Uwanja wa Majengo, bado barabarani watu walikusanyika kuuaga mwili huo hali iliyowapa wakati mgumu polisi.
Kuanzia saa 4:20 asubuhi, polisi wa kutuliza ghasia wakishirikiana na askari wa usalama barabarani, walianza kujipanga katika mzunguko wa magari wa YMCA ili msafara usiingie katikati ya mji.
Polisi hao wakiwa na magari matatu na silaha walijipanga na kuelekezana namna watakavyohakikisha msafara huo hauingii mjini kama jeshi hilo lilivyokuwa limetoa maelekezo.
Msafara ulipokaribia shule ya msingi J.K Nyerere (zamani Kibo) polisi walitumia mbinu ya kukamata magari ya kiraia na kuyatumia kuziba barabara inayoelekea mjini ili kuhakikisha hakuna gari linapita.
Kutokana na ukubwa wa msafara wa magari likiwamo lililobeba mwili wa Ndesamburo, barabara zote zinazoingia na kutoka katika mzunguko huo wa YMCA zilifungwa isipokuwa ya kuelekea Majengo.
Baadhi ya madereva waliokuwa wakienda barabara kuu ya Moshi-Dar es Salaam walilazimika kutumia barabara mbadala, ingawa hata huko mbele walikutana na vizuizi vya polisi wakiwamo wa usalama barabarani.
Msafara huo ulitanguliwa na waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda na kisha watembea kwa miguu ambao walitembea kuanzia maeneo ya madukani hadi Uwanja wa Majengo.
Mbali na pikipiki na watembea kwa miguu, msafara huo ulikuwa na magari zaidi ya 50 yaliyowabeba baadhi ya viongozi wa kitaifa ambao walilazimika kwenda mwendo sawa na wa watembea kwa miguu.
Mamia ya wananchi walijipanga katika barabara nzima kuanzia KCMC hadi Uwanja wa Majengo huku baadhi ya wananchi wakitumia simu zao za mikononi kupiga picha za kumbukumbu.
Msafara ulipofika uwanjani, ulipokewa na wabunge, madiwani na watu waliopata shahada ya udaktari wa heshima (PhD) pamoja na marehemu ambao walipata fursa ya kubeba jeneza lake.
Pia, washirika hao waliopata heshima hiyo pamoja na Ndesamburo walifanya tendo la kuweka joho na kofia ya Ndesamburo aliyotunukiwa juu ya jeneza lake.
Maelezo: MWAANCHI






























Baadhi ya nukuu zahotuba za viongozi waliohutubia uwanjani hapo

Mh Fredrick Sumaye
"Kuna juhudi kubwa sana ya watu kujidanganya kwamba wanaweza kukandamiza demokrasia hii tulipofikia. Demokrasia ni kama 'ball bladder, ukiikandamiza sanaitapasuka.... Chuki sasa ipo dhahiri. Hizi chuki tukiendelea kuzijega hazitaacha mtu hai. Chadema ina watu wengi sana.Hatutaweza kuwaonea muda mrefu"

Mchungaji Peter Msigwa
"Uongozi ni kuongeza thamani kwa watu unaowaongoza, na ndicho alichokifanya Ndesamburo. Tujifunze tutakapokuwa tumekufa tutaacha nini nyumba yetu. Haitakuwa kuhusu muda gani umeishi duniani bali umesaidia nini. Viongozi wa Serikali wajiulize pale ving'ora vinapoondoka na askarihawapo, utapata mapokezi kama haya"

Mh Edward Lowassa
"Niungane na Sumaye na Gwajima. Jitihada zakudidimiza demokrasia zinaendelea kwa kasi sana. Baada kuwakatalia uwanja wa Mashujaa mmeamua kuja Majengo. Hawa tuwasamee bure!"
Mama Mwijage wa CUF
"Wale ambao walifanya Ndesamburo asiagweuwanja wa Mashujaa Mungu anajua mwenyewe. Ndesamburo amemaliza, wao hawajui watakufa namna gani. Yeye kamaliza safari yake,sisi hatujui yakwetu?"
Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo
"Nilazima tumuenzi Mzee huyu. Kumuenzi Ndesamburo ni kuenzi demokrasia. Poleni sana Kilimanjaro. Hajaondoka mtupu, ameacha legacy. Badala ya kulia mnapaswa kumtazamana kushukuru"

John Heche, Mbunge wa Tarime
"Niwaombe viongozi wote wadini na vyama tusimame. Chuki inazidi kushamiri kwenye Taifa letu. Tunapoona watu wanazuiwa kutoa rambirambi, Mzee kama huyu anapewa mizengwe, chuki inapitiliza mtu asiagwe kwenye mahali walipopendekeza. Tukemee sana mambo haya na chuki inayopandikizwa kwa niaba ya vizazivijavyo"

Mh Ester Mmasi, mwakilishi wa wabunge wa CCM
"Wabunge wa CCM tumeguswa sana na msiba huu. Tulipozungumza (Dodoma) wengine walisema tumepotezababa..., wengine wameoteza mtu aliye adimu sana. Nimetumwa nilete salamu za rambirambi kutoka kwa RaisMagufuli ambaye ni Mwenyekiti wa CCM. Naibu Spika (Mh Tulia Ackson) alifika nyumbani kwa marehemu akiambatana na uongozi wa CCM Kilimanjaro na Waziri Maghembe. Naibu Spikaalisema katika wasifu wa marehemu, Mzee Ndesamburo alisimama... bila kujali itikadi na msiba huu utupe nafasi ya kutafakari. tarehe 31 Mei, 2017 wabunge wa CCM walifanya ibada ya kumuombea marehemu iliyoongozwa na Jenista Mhagama. Wamejipanga kuja kibunge (kuwafariji wafiwa)"

Mh Anna Komu, Mbunge Mstaafu CHADEMA
"Ndesamburo alikuwa na masimamo wa vitu vitatu; Kusimamaia dhamira kwahali na mali, Mkweli saa zote na mwenye Upendo kwa wengine. Huwezi kuongoza watu kwakuwabagua matabaka kwa kuona wengine wana maana wengine hawana. Kiongozi lazima uwapende unaowaongoza"
Mh Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa
"...Tukaenda Polisi kuomba Brass Band ya Polisi. Wakasema Mwenyekiti ongea na IGP Simon Sirro. Leo Polisi wanaogopa hata kufanya kazi kwasababu hawajui bwana mkubwa atafurahi au atakasirika.... Wengine wanaogopa mimi niseme, kuna ukandamizaji kwa Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro."

Sheikh Rajab Katimba, Jumuia ya Taasisi za Kiislamu Makao Makuu
"Ndesamburo ndiye aliyewezesha kuweka uzio makaburi ya Moshi. Tunaomba jamii ijifunze kutoka kwa Mzee huyu na ndio tutamuenzi. Kuna hatua tano za maisha ya mwanadamu; roho kuumbwa, kuzaliwa, kuishi, kufa, kuzikwa na hukumu. Tuwasamehe wabaya ambao hawatakii mema amani ta Tanzania na msiba huu usitumiwe kama mtaji wa kisiasa. Chama (CHADEMA) kihakikishe kinatunza kumbukumbu za muasisi huyu (Ndesamburo) tukiamini kuna siku haki itakuja kutamalaki katika Taifa hili."

Mh Ester Bulaya, mwakilishi Wabunge wa CHADEMA
"Wabunge wote wa CHADEMA tumeguswa sana na msiba huu. Ndesamburo ni miongoni mwa wazee walionishauri kuungana na vijana kuleta mageuzi ya kweli. Ukikaa nae huwezi kuhisi uko na mzee. Aliniambia,Ester, huko uliko hustahili njoo huku.Simama na vijana wenzako tetea Taifa lako... Mbali na utajiri wake na heshima kubwa aliwaheshimu wasio na mali na wanyonge na mpaka anakufa alikuwa anaandika cheque kusaidia familia za watoto waliokufa (wa Lucky Vincent) bilakujali walikuwa wachama gani. Tutaendelea kupigania haki za Taifa bila kujali vikwazo vilivyoko..Hatutaki kufa tukiwanyanyasa wananchi, hatutaki kufa tukitoa adhabu kwa wananchi waliotuchagua"

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi
"Baba yetu Ndesamburo, masingialioujenga Moshi, siasa alizokuwa anaziendesha Moshi ndio mafanikio ya Manispaa ya Moshi. Hakuna mtu atakayetuondoa kwenye msingi wa amani na mshikamano aliotuachia. Nawahakikishia, kwa pamoja na Mbunge, aliyoyajenga Ndesamburo tutasimama nayo mpaka ukombozi utakapotokea... Kijana unapofanya mambo bila kutumia busara unadhalilisha vijana wenzako. Tumuombe Mungu atuongezee Busara na sio Madaraka!"

Mh James Mbatia, Mwenyekiti mwenza UKAWA na Mbunge wa Vunjo NCCR Mageuzi.
"Nilimjua Ndesamburo mwaka 1991 mwezi wa sita, wakati huo ndio tumemaliza kongamano la demokrasia. Tarehe 31 Januari 2016 Ndesamburo aliniambia tuandike historia ya mageuzi nchini na atagharamia. Akakutanana Ndimara Tegambwage kwa kazi ya kuandika. Alitaka iandikwe afurahie kazi yake duniani .

Tutamuenzi Ndesamburo kwa kuita wana mageuzi wote wakutane Moshi kuandika historia ya wanamageuzi. Tanzania ni mali ya watanzania. Niwaombe CCM, misiba kama hii inaleta watu wote pamoja. Tusikubali kufarakanishwa namna hii. Hakuna uwakilishi wa CCM hapa. Kamamwenyekiti wa kituo cha demokrasia nimewawakilisha lakini nitawaambia. Tusikubali kugawanywa namna hii. Kitendo hiki ni kibaya sana."


UPDATES MSIBA WA MAREHEMU BALOZI CISCO MTIRO, MAZISHI KUFANYIKA JUMATANO

$
0
0


Mkuu wa Itifaki mstaafu Balozi Cisco Mtiro (pichani) ambaye amefariki dunia leo asubuhi  katika hospitali ya Aga Khan jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu, anatarajiwa kuzikwa siku ya JUMATANO, kwa mujibu wa msemaji wa familia, Bw. Shaaban Kessy Mtambo

Jioni hii Bw. Mtambo ameiambia Globu ya Jamii kwamba mazishi ya mwanadiplomasia huyo yamepangwa kufanyika siku ya JUMATANO saa saba adhuhuri katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. 
Hiyo ni baada ya kuwasili watoto wake walioko Marekani ambao wanategemewa kuwasili Jumanne usiku, pamoja na mjane wa marehemu anayetegemewa kuwasili Jumanne mchana akitokea Bangui, Afrika ya Kati.
Amesema mwili wa marehemu unatarajiwa kuwasili nyumbani kwa marehemu saa tano asubuhi siku hiyo ya JUMATANO ambapo utafanyiwa kisomo na kuswaliwa kabla ya kuelekea makaburini kwa mazishi.
 Msiba upo nyumbani kwa marehemu mikocheni B jijini Dar es salaam ambako ndugu, jamaa marafiki, majirani na waliofanya kazi na marehemu wamekuwa wakimiminika kutoa mkono wa pole kutwa nzima ya leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia msiba huu.

Mola aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi - AMINA

MWILI WA HALILA TONGOLANGA WAAGWA

$
0
0


Halila Tongolanga amefariki jana usiku katika hospitali ya Muhimbili. Alikuwa mwanamuziki wa siku nyingi na alifahamika kwanza  kwa wengi baada ya kuanza kusikika kibao chake cha lugha ya Kimakonde cha Kila munu ave na kwao, chenye tafsiri ya ‘Kila mtu ana kwao’ ambacho alikirekodi akiwa bendi ya jeshi ya CTU Monduli, iliyojulikana kama  Les Mwenge. Kwa kifupi ni kuwa baada ya hapo aliitwa kujiunga na bendi iliyokuwa mali ya Dr Alex Khalid, iliyokuwa ikiitwa Makondeko Six. Wakati huo Dr Khalid alikuwa na sehemu kubwa ya burudani iliyokuwa pia na ukumbi na ilikuwa inaitwa Makondeko ikawa na bendi ya watu sita hivyo bendi hiyo ikaitwa Makondeko Six. Bendi hii awali ilikuwa ikipiga muziki kwa kufuata nyayo za bendi ya Tatu Nane, lakini Dr Khalid baada ya kuona bendi haina umaarufu kutokana na aina ya muziki iliyokuwa ikipiga, ndipo alipomuita Halila Tongolanga nae akaja na baadhi ya wanamuziki wakajiunga na kuanzisha kundi lililoendelea kutumia jina la Makondeko Six japo wanamuziki walikuwa wengi zaidi ya sita. Na ndipo katika kundi hili lilikuwa na wanamuziki wengine kama Innocent Nganyagwa, Anna mwaole wakaweza kurekodi tena wimbo wa Kila Munu Ave na kwao na kundi kupata umaarufu mkubwa mpaka baada ya kusambaratika kwa Makondeko baada ya kifo cha Dr Alex Khalid, lakini Tongolanga aliendelea kutumia jina la Makondeko.
Baadhi ya wanamuziki waliowahi kufanya kazi na Tongolanga katika kundi la makondeko Six, wakiwa wanasubiri kusafirisha mwili wa mpendwa wao.Toka kushoto, Innocent Nganyagwa, Meneja wa bendi, mpiga solo, Waninga
                       Tongolanga amefanya kazi nyingi za muziki ikiwemo kuwa mmoja wa kundi lililoundwa na wanamuziki wengine mahiri kama Moshi William, Muhidin Mwalim, Huluka Uvuruge, Kandaya na wengine lililojulikana kama Bana mwambe, ambapo waliweza kutoka nyimbo nyingi nzuri sana wakati biashara ya kuuza album ilipokuwa ina faida. Tongolanga ameagwa na wapenzi wa muziki ndugu na marafiki, lakini kulikuwa na uhaba mkubwa wa wanamuziki wenzie katika kundi lililokuja kumuaga mwanamuziki huyu. Waliojitokeza hasa ni wanamuziki wale tu ambao waliwahi kupiga nae katika kundi la Makondeko na Bana Mwambe na wanamuziki wengine wachache wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki John Kitime, Katibu Mkuu wa Chamudara Hassan Msumari. Serikali iliwakilishwa na Katibu Mtendaji wa BASATA.  Katika jambo moja kubwa lililotokea wakati wa kuaga mwili ni kujitokeza kwa balozi wa Msumbiiji Bi Monica Patricio Clemente aliyefika Muhimbili kuaga mwili wa Tongolanga akiwa amesindikizwa na maafisa wengine, na pia Balozi huo alitoa rambirambi zake kama Balozi na alitoa rambirambi kutoka kwa Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji. Hili lilikumbusha usemi wa wahenga ‘Nabii hathaminiwi kwao.’ Taarifa zilizopatikana pale ni kuwa Tongolanga alikuwa mtu maarufu sana nchini Msumbiji, na aliyekuwa ni msanii muhimu wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu nchini humo.
Balozi wa Msumbiji Bi Monica Patricio Clemente akiaga sanduku lililokuwa na mwili wa Halila Tongolanga

Nilipokutana nae kwa mara ya mwisho akiwa kitandani Tongolanda kwa sauti ya uchovu alinambia alikuwa na mengi ya kunambia, wakati tunasubiri taratib kukamilika za kuanza kusafirisha mwili, Innocent Nganyagwa ambaye alikuwa mmoja ya wanamuziki waliotengeneza kundi la Makondeko Six alinambia Tongolanga alikuwa amepanga kufanya onyesho la ‘Usiku wa Makondeko’ na alikuwa na mipango mingine mikubwa ya kufanya kupitia kipaji chake. Pengine ndiyo hayo aliyotaka kunambia Mungu pekee anajua. 
Shukrani za pekee zimfikie Mbunge wa Tandahimba Mheshimiwa Katani Ahmed Katani, kwani kwa juhudi zake Tongolanga alisafirishwa akiwa hai kutoka Ndanda hadi Dar es Salaam kwa matibabu, na pia ndie aliyeusafirisha mwili wa mwanamuziki huyu kwenda Mchichila kwa ajili ya mazishi.
Toka kushoto Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Nyangamale, Balozi wa Msumbiji nchini, Katibu Mtendaji wa BASATA, Mbunge wa Tandahimba Mhe Katani Katani, afisa wa Ubalozi wa Msumbiji

Tongolanga anategemewa kuzikwa kijijini kwao Mchichila kesho Junanne 6 Juni 2017.

Mungu Amlaze Pema Halila Tongolanga 
Mpiga Kinanda Geophrey Kumburu, Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza, Katibu Mkuu wa CHAMUDATA Hassan Msumari
John Kitime, wanamuziki wa Makondeko Six, Mngereza, KumburuAdd caption

Sanduku alilolazwa Halila Tongolanga likitayarishwa kuingizwa kwenye gari la kusafirisha kuelekea Mcjichila




Sanduku likiingizwa kwenye gari

Imetayarishwa na John Kitime wa www.tanzaniarhumba.blogspot.com

Taswira za Awali Ibada ya Maziko ya Hayati Dk Philemon Ndesamburo

$
0
0
Zoezi la kuatoa heshima za mwisho kwa Dk Ndesamburo linaendelea katika Kanisa la  Usharika wa Kiborloni kabla ibada kuaanza.
Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo unaagwa kwa mara ya pili na wafuasi wa Chadema pamoja na  wananchi ambao hawakupata nafasi ya kumuaga siku ya jana katika viwanja vya Majengo mjini Moshi.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mazishi, Joseph Selasini amewataka wananchi na watu wote waliohudhuria ibada ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania(KKKT)Usharika wa Kiborloni kuacha kupiga picha mwili wa marehemu ili kutunza heshima yake.
Viongozi mbalimbali wameendelea kuwasili katika kanisa hilo wakiwemo viongozi wa Chadema na Mbunge wa Singinda Kaskazini(CCM), Lazaro Nyalandu.
Awali wafuasi na wanachama wa Chadema walifurika nyumbani kwa Ndesamburo kwa ajili ya kuandamana kupelekwa mwili wake  kanisani.
Mwili wa Ndesamburo umesaliwa nyumbani kwake  kabla ya kupelekwa kanisani.





Maelezo ya Ziada: Mwananchi Digital

UNESCO YATAKA WANANCHI KUENZI URITHI WA DUNIA KWA KUTEMBELEA

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Bi. Irina Bokova, katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, leo ametaka wananchi mbalimbali kutenga muda binafsi na kutembelea moja ya maeneo ambayo ni urithi wa dunia yakifadhiliwa na UNESCO.
Amesema anaamini kuwa kwa wananchi kushiriki watashawishika kuendelea kuishi kwenye maeneo hayo na kuyaenzi.
Amesema kitendo hicho kidhati kitakuwa kimewaunganisha watu na asili na hivyo kuondoa dhana ya zamani ya kuweka maeneo hayo mbali na watu.
“Inaweza kuwa vigumu kuamini sasa, lakini miaka hamsini iliyopita ilidhaniwa kuwa njia bora ya kulinda asili ni kuiweka mbali na watu ...Hii leo, tunajua vyema zaidi kwamba kwa kadri uhusiano baina ya watu na mazingira yao unavyokuwa wa karibu zaidi ndivyo watu wanavyofahamu zaidi juu ya umuhimu wa asili na viumbe hai, urithi na maji, kwa ajili ya ustawi wao binafsi na kwa ajili ya hali ya baadaye ya sayari yetu.”Alisema.
Mkuu huyo alisema hayo akizungumzia umuhimu na uhifadhi kwa maeneio zaidi ya 2000 duniani ya bayongahewa, maeneo ya hifadhi ya jiolojia ya na maeneo ya Urithi wa Dunia yanayodhaminiwa na UNESCO.
Alisema maeneo hayo pamoja na kuhifadhi urithi wa dunia pia hutoa ajira kwa watu wanaoyazunguka na milango yake iko wazi kwa umma wote.
“Maeneo ya hifadhi ya jiolojia ni vitabu vilivyo wazi vya kihistoria ambavyo huturudisha nyuma mamilioni ya miaka. Hifadhi za Bayongahewa ni mahali ambapo jamii hukabiliana na changamoto za maendeleo kwa kuunda njia mpya za kijamii na uchumi endelevu. Maeneo ya hifadhi ya jiolojia na hifadhi za Bayongahewa huunganisha uhifadhi na elimu kwa mbinu mpya ya maendeleo endelevu, kama vile utalii wa mazingira na kilimo hai.”alisema katika ujumbe wake kwa dunia.
Aliwataka wananchi kuheshimu mazingira ya asili hutokana na uelewa.
Aliwataka wananchi kupitia katika tafakari ya kina kujitumbukiza katika Bustani ya Kiajemi ya Iran ambako maji hufanya ishara za maumbo ya mapambo mbalimbali.
Aidha alisema vyema kuona eneo la hifadhi ya jiolojia la UNESCO la Tumbler Ridge nchini Canada, na kuogelea katika maziwa ya Alpine yenye maji angavu kama kioo na kulala chini ya nyota.
Pia amewataka kufanya safari ya kutembea kwa miguu katika hifadhi ya Bayongahewa ya Mujib huko Jordan ambayo ipo mita 420 chini ya usawa wa bahari ikiwa karibu wake na Bahari ya Chumvi.
Mkuu huyo wa Unesco ametaka wakazi wa dunia hii wakati wakiadhimisha Siku ya Mazingira Duniani, kutumia ipasavyo maeneo teule ya UNESCO kila mahali kuungana na asili inayowazunguka na inayoleta uzuri, maana na amani katika maisha.

Mama Mghwira aapishwa tayari kwa kazi ya Ukuu wa Mkoa Kilimanjaro

$
0
0
Mkuu mpya wa Mkoa wa Kilimanjaro Mh Anna Mghwira akiingia kwenye gari yake ramsi kwa kazi baada ya kuapishwa na Rais Magufuli asubuhi ya leo.

Picha na ISSA MICHUZI
KWA MUJIBU WA MTANDO WA GAZETI LA MWANANCHI 
Dar es Salaam
Wakati Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amekula kiapo Ikulu jijini hapa leo, Jumanne Chama cha ACT- Wazalendo kimesema kitajadili utekelezaji wa majukumu yake mapya na ya uenyekiti wa chama hicho.
ACT imesema ilipokea taarifa ya uteuzi huo wakati Mghwira akiwa nje ya nchi hivyo baada ya kurejea, viongozi wa juu wa chama hicho pamoja na yeye walifanya mazungumzo kuhusu uteuzi huo.
Mghwira aliteuliwa nafasi hiyo Juni 3, mwaka huu na Rais John Magufuli kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Saidi Meck Sadick aliyeamua kuachia ngazi ili vijana waendelee kufanya kazi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Jumanne na kuthibitishwa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa ACT, Ado Shaibu ni kuwa kufuatia uteuzi huo na uenyekiti na majukumu ya Mkuu wa Mkoa kamati ya uongozi wa chama itakutana kesho kwa ajili ya mazungumzo.
Pamoja na mambo mengine chama kitajadili namna ambavyo Mghwira atatekeleza wajibu wake wa uenyekiti wa chama na majukumu yake mapya.


 “Chama kinatoa wito kwa wanachama wake kuendelea na utulivu wakati wa vikao vyake vya chama vinachukua hatua stahiki kuhusu jambo hilo,”imesema taarifa hiyo.

PICHA KUTOKA CHADEMA: MATUKIO YA IBADA NA MAZIKO YA DK PHILEMON NDESAMBURO


IJUE HISTORIA YA FREEMAN AIKAEL MBOWE NA MAGEUZI

$
0
0

MJUE FREEMAN AIKAEL MBOWE

FREEMAN AIKAEL MBOWE
Freeman Aikael Mbowe alizaliwa tarehe 14/09/1961 Wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro.

Mbowe ni miongoni mwa Watu waliofanya Kazi katika Bank kuu ya Tanzania kama Afisa wa Bank Kuu (BoT)  akiwa chini ya Edwin Mtei, Bob Makani.

Katika harakati za kisiasa, Freeman Aikael Mbowe aliingia rasmi katika siasa mwaka 1992.

Freeman Aikael Mbowe ni miongoni mwa WAASISI au waanzilishi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) chama ambacho kilisajiliwa usajili wa kudumu mwaka 1993 kwa namba 0000003 kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu cha 7(1),(2),(3), kifungu cha 8(1),(2),(3)(4)& (5)pamoja na kifungu cha 9(1)(a)(b)(c) (2)(a),(b),(c),(d),(e) na 10(1)(a),(b),(c) na (d)

Mbowe akiwa ndio kijana mdogo kuliko Wote wakati wa uasisi wa CHADEMA aliingoza kurugenzi ya Vijana ya CHADEMA chini ya Uenyekiti wa Edwin Mtei. Waasisi wengine wa CHADEMA kutaja kwa uchache ni Pamoja na -

1/EDWINI MTEI - ARUSHA

2/BOB MAKANI - SHINYANGA

3/FREEMAN MBOWE - KILIMANJARO

4/BROWN NGWILUPIPI - MBEYA

5/EDWARD BARONGO - KAGERA

6/WASIRA-MARA

7/MENRAD MTUNGI - KAGERA

8/MARRY KABIGI-MBEYA

9/EVARIST MAEMBE - MOROGORO

10/COSTA SHIGANYA - KIGOMA

Wakati wa kusaka wanachama wa CHADEMA ili kupata usajili wa Muda(Provisional registration) kwa mujibu wa sheria ya vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 kifungu cha 8 na usajili wa kudumu (Full registration) kwa mujibu wa kifungu cha 10(1)(b) kinachotaka chama cha siasa Ili kupata usajili wa kudumu ni lazima kiwe na wanachama miambili katika mikoa kumi(10) huku mikoa miwili ikiwa mmoja Pemba na mwingine Unguja, CHADEMA iliasisi hatua hiyo kama SAFARI YA TREN KUTOKA DAR ES SALAAM KWENDA KIGOMA.

Dhana ya "SAFARI YA KUTOKA DAR ES SALAAM KWENDA KIGOMA ilimaanisha kwamba, katika dhamira ya kutafuta mabadiliko ya kweli na kuunda Serikali kwa kushinda uchaguzi , wapo watakaonunuliwa, wapo watakaoamua kuacha siasa, wapo watakaohama chama, wapo watakaoachana na CCM na kupanda Treni popote iwe Morogoro, Dodoma, Kibaha nk.

Kwa tafsiri nyepesi, Mbowe na Waasisi wenzake waliipa safari ya kutoka Dar Es Salaam kwenda Kigoma kwamba kufika Kigoma ni CHADEMA kushinda uchaguzi na kuunda serikali. Waliamini kwamba katika safari, wengine watashukia Kibaha, wengine watapanda, wengine watapanda Treni Morogoro, wengine watashuka, wengine watapanda Dodoma wengine watashuka. Hivyo walimaanisha kwamba, katika safari ndefu ya kufika kigoma (Kipindi hicho safari ya Treni kutoka Dar Es Salaam kwenda Kigoma ilikua ni ya shida, mteso na maumivu. Ilichukua siku Tatu hadi Tano kutoka Dar Es Salaam kufika Kigoma.). Hivyo Mateso waliyoyapata Waasisi kuijenga CHADEMA walifananisha na safari ya kutoka Dar Es Salaam kwenda Kigoma. Mfano, Viongozi wa CHADEMA wakiongozwa na Edwin Mtei, Bob Makani, Freeman Mbowe, Mary Kabongo na Evarist Maembe walipigwa mawe na kufukuzwa na wananchi Morogoro. Waliambiwa kwamba CHADEMA ndio nini?? Kwa nini mnampinga chama chetu kilichotukomboa Kutoka kwa utumwa wa wakoloni. Kwa nini mnapinga chama cha Mwalimu Nyerere baba wa taifa ??.Kwa nini mnapinga chama cha wanyonge CCM chama chenye matumaini kwa wakulima na wafanyakazi????. Waasisi hawa walipigwa mawe, kufukuzwa maeneo mbalimbali, kutukanwa, kudhalilishwa na kudhihakiwa. Kuzungumza siasa za upinzani ilionekana ni usaliti, uhaini nk. Yote hayo, walivumilia. Wengine walikata tamaa,wengine waliamua kurudi Ccm, wengine waliamua kulinda Vyeo vyao na maslahi yao na kurudi Ccm.

Mwaka 1995 Edwin Mtei na Bob Makani wote wawili walichukua Fomu ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wote walionekana kuwa na nguvu. Mapambano huo ulileta sitofahamu kubwa ndani ya CHADEMA. Freeman Mbowe kama kijana alitoa ushauri kwa chama kwamba CHADEMA isisisimamishe mgombea urais ili kuepusha mpasuko ndani ya chama na badala yake CHADEMA imuunge mkono mgombea wa urais kupitia NCCR MAGEUZI Agustine Lyatonga Mrema. Ushauri huu wa Mbowe uliungwa Mkono na wanachama na Viongozi. Mtei na  Makani waliacha mchakato huo na CHADEMA ilimuunga mkono mgombea urais Lyatonga Mrema.

Freeman Aikael Mbowe alichukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Hai mwaka 1995. Mbowe wakati wa Kampeni jimbo la Hai , aliombwa kugharamia Mkutano wa mgombea urais Lyatonga Mrema na aliahidiwa kwamba Mrema atamnadi jukwaani. Mbowe kwa kuwa alikua na Fedha na uchumi mzuri, aligharamia Mkutano na malazi ya timu ya kampeni ya Mrema nk. Lakini Mrema alipofika Jukwaani alimpuuza Freeman Mbowe wa CHADEMA na kumnadi mgombea wa NCCR MAGEUZI aliyeitwa Mwinyihamisi Mushi. Katika uchaguzi huo Mgombea wa NCCR MAGEUZI Mwanahamisi Mushi alishinda uchafu kwa kupata kura 29,046 (52.0%) huku Freeman Mbowe akiambulia kura 15,995(28.6%)

Mbowe hakukata tamaa, Mwaka 2000,Freeman Aikael Mbowe aligombea tena ubunge jimbo la Hai na kupata ushindi mnono wa kura 64.5% dhidi ya mpinzani wake wa NCCR MAGEUZI ambaye alipata mweleka kutokana na chama chake kuwa na mvurugiko mkubwa ndani ya Chama kutokana na mgogoro mkubwa wa kisiasa kati ya Mabere Nyaucho Marando  na Agustine Lyatonga Mrema. Mbowe aliongoza jimbo la Hai mpaka mwaka 2005.

Katika nafasi ya Urais, Mbowe na CHADEMA Kwa ujumla walikubaliana kwamba CHADEMA isisimamishe mgombea yeyote bali chama kimuunge mkono mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof Ibrahim Haruna Lipumba.

Mwaka 2004,Freeman Mbowe aligombea uenyekiti wa CHADEMA TAIFA na kushinda akimpokea Bob Makani ambaye aliongoza kuanzia mwaka 1999. Mbowe baada ya kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA alifanya mabadiliko makubwa Sana ndani ya chama.

Baada ya kuchaguliwa, Mbowe alifanya mabadiliko makubwa Sana Ni kipindi hiki Mbowe alianza kutembelea vyuo vikuu mbalimbali vya Tanzania, kufuatilia wanasiasa mbalimbali kutoka CCM, NCCR MAGEUZI, CUF, TLP na vyama vinginevyo. Mifano iko Mingi.

John Mnyika ambaye alikua mwanaharakati wa kutetea haki za wanafunzi na watu mbalimbali na pia akiwa mtangazaji wa Redio One Stereo, Freeman Mbowe alimshawishi kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili kuungana na wanamabadiliko wengine. Hata hivyo, UWEZO mkubwa wa John Mnyika ambao aliuonesha katika ukumbi wa Nkrumah Chuo kikuu cha Dar Es Salaam (ingawa yeye alikua akisoma masomo ya jioni) alisimama na kupinga sera ya uchangiaji wa masomo elimu ya Juu (cost sharing) na kusababisha wanafunzi kuanza Mgomo chuoni hapo. Mnyika akiwa Morogoro, aliombwa kutuliza hali hiyo na alipofika chuoni, aliita wanafunzi na kuwaambia mambo kadhaa ili kupima ujasiri wao. Alimuomba Rafiki yake kurusha jiwe katikati ya kusanyiko Mabibo Hostel, baada ya kurushwa jiwe Hilo, wanafunzi walitawanyika kukimbia ndipo Mnyika akasema ninyi ni waoga. Hamuwezi kupambana. Nawataka muache Mgomo endeleeni na masomo.

Mnyika alikua mfuasi wa CHADEMA tu mpaka 2005 alipoamua kujiunga rasimi CHADEMA na kuchukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Ubungo. Alipochukua fomu ya Ubunge, Chuo kikuu cha Dar Es Salaam kilimfukuza kama njia ya kumdhoofisha. Mbowe alipoona uwezo wa Mnyika wa hoja, umakini, weledi na akili Alimuomba kujiunga na CHADEMA. Hotuba ya John Mnyika Bungeni mwaka 2001 akielezea kuhusu UONEVU na uharibifu wa Serikali baada ya kumuua mwanafunz mmoja Kule shule ya Sekondari Iyunga Mbeya ni rekodi pia kubwa kwa Mnyika.

Mbowe pia alifanikiwa kumvua samaki nguli wa siasa Zitto Zuberi Kabwe (ZZK) akiwa ni kiongozi chuo kikuu cha Dar Es Salaam. Zitto Kabwe akiwa Waziri mkuu wa chuo kikuu cha Dar Es Salaam na mwanaharakati wa utetezi wa wanafunzi (moja ya WAASISI wa TSNP) alifanikiwa kuvuliwa na Mbowe. Mbowe alimshuhudia Zitto Kabwe katika majukwaa ya chuo kikuu cha Dar Es Salaam hasa mahali maarufu kama REVOLUTION SQUARE. Zitto alionekana kutoa matamko mbalimbali yaliyoitetemesha Serikali akihoji Ufisadi, kuibua uchafu mbalimbali wa Serikali ya Mkapa, na pia utetezi wa wanafunzi. Mbowe alimuona Zitto na kushawishi ajiunge CHADEMA. Zitto Kabwe alikubali kujiunga CHADEMA na Mwaka 2005 Zitto Kabwe aligombea ubunge jimbo la Kigoma Kaskazini na alinadiwa na Freeman Mbowe kama mgombea urais wa CHADEMA. Zitto Kabwe alishinda jimbo hilo na kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini.

Halma James Mdee naye ni miongoni vijana ambao Mbowe aliweza kuwashawishi kuingia katika siasa. Zitto na Halma Mdee wakiwa marafiki Sana chuoni, Halma Mdee akisomea Sheria na Zitto akisomea Uchumi, kama iliyokua kwa Zitto, Halma Mdee kama mwanaharakati wa Kutetea wanafunzi (Muasisi wa TSNP) alikubali kujiunga na CHADEMA.

Tundu Antipas Lissu ambaye alikua mwanachama wa NCCR MAGEUZI pia alifuatwa na Freeman Mbowe kuomba msaada wake katika mambo ya Sheria kutetea wanachama wa CHADEMA, wananchi katika migodi mbalimbali nk. Tundu Lissu alikua ni tishio kubwa katika mambo ya Sheria na mtetezi mambo ya mazingira. Alipinga na kupambana vikali Sana na serikali ya Benjamin Mkapa iliyowapa wawekezaji migodi na kufukuza wananchi maeneo mbalimbali ya nchi hasa Geita, Shinyanga, Mara nk. Harakati hizi za Lissu ziliifanya Serikali ya Mkapa kumtafuta na baadaye Lissu alielekea Uingereza na baadaye Afrika Kusini. Kutokana na rekodi hiyo ya harakati za mapambano, Freeman Mbowe alimuona Lissu ni silaha nzuri dhidi ya Ccm na silaha njema katika ukombozi wa Mtanzania. Alimuomba kujiunga CHADEMA.

Wengine waliojiunga na CHADEMA kipindi cha uongozi wa Mbowe kuanzia mwaka 2004 ni Pamoja na Prof Mwesigwa Baregu, Livingstone Lusinde (alirudi Ccm na sasa ni Mbunge wa Mtera), Peter Msigwa kutoka TLP, David Ernest Silinde na wengine wengi. Ni kipindi hiki CHADEMA ilifungua milango kwa wanachama kujiunga, Wasomi na vijana walijiunga CHADEMA. Baadhi ya watu walianza kuita CHADEMA ni Chama cha vijana Wasomi ingawa hata wazee Wasomi walijiunga.

Mabadiliko mengine aliyotaka Mbowe ni Pamoja na kutumia ngumi kama ishara ya salamu ya chama

Mwaka 2005 Freeman Mbowe  aligombea uraurais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa na mgombea mwenza kutoka Zanzibar bwana Jumbe Rajab Jumbe ambaye alifariki siku chache kabla ya uchaguzi mkuu uliokua ufanyike tarehe 30/10/2005 na hivyo uchaguzi kuahirishwa mpaka tarehe 14 /12/2005.

CHADEMA ilimteua mgombea mwenza Anna Maulid Komu kuwa mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika uchaguzi ule, Mbowe alitumia chopper au Helkopta kupiga kampeni maeneo mbalimbali nchini na kubatizwa jina "Kamanda wa Anga".Katika kampeni za urais Mbowe aliasisi Vazi la Magwanda ya Khaki na neno Kamanda kwa mwanachama yeyote wa CHADEMA .

Wakati wa kampeni, Mbowe alipendelea kuvaa Nguo za khaki zenye sura ya gwanda kwa kuwa zilikuwa hazichafuki Sana na Muda wa kufua mara kwa mara haukuwepo. Alipofika eneo fulani kwa ajili ya kampeni za urais, wananchi walimshangilia na kumwambia kwamba amependeza Sana kuvaa zile nguo za kikamanda(Magwanda ya khaki). Aliwauliza wananchi, niendelee kuvaa mavazi ya kikamanda?? Maelfu ya wananchi wakajibu ndio oooooooo oooooooo. Mbowe akawaahidi wananchi kwamba atapeleka pendekezo kamati kuu, Baraza kuu na Mkutano mkuu ili gwanda la khaki kuwa Vazi rasimi la Kamanda wa CHADEMA (mwanachama wa CHADEMA).Mbowe alifikisha pendekezo hilo kamati kuu ya CHADEMA baadaye Baraza kuu na kupitishwa na Mkutano mkuu 2006 kuwa Vazi rasimi la chama.

Jakaya Mrisho Kikwete alishinda kwa kishindo uchaguzi mkuu ule kwa kupata ushindi wa 80.28% akifuatiwa na Prof Haruna Ibrahim Lipumba aliyepata 11.68% na Freeman Mbowe akishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 5.88%.

Miaka ya 2008,2009 CHADEMA chini ya Mbowe ilishiriki chaguzi ndogo ambazo ni Pamoja na Uchaguzi wa Jimbo la Busanda, Jimbo la Tarime na Mbeya vijijini. CHADEMA ilishinda Tarime na kushindwa Busanda huku jimbo la Mbeya vijijini Shambwee Shitambala alijiapisha kupitia ofisi yake ya Mawakili hali iliyopelekea CCM kupitia mgombea wao Luckson Mwanjali kuweka pingamizi dhidi ya Shitambala na hivyo CCM kupata ushindi dhidi ya wagombea dhaifu wa TADEA, TLP nk.

Mwaka 2009, Freeman Mbowe aligombea tena uenyekiti wa CHADEMA. Alipata mpinzani Zitto Zuberi Kabwe. Zitto alitangaza kugombea uenyekiti wa CHADEMA taifa na kutoa sababu zake za kutaka nafasi hiyo katika gazeti la The Citizen la tarehe 26/08/2009. Zitto alieleza kwamba anaweza kuisaidia CHADEMA kushinda serikali za mitaa 2009 na uchaguzi mkuu 2010.Wazee wa CHADEMA walimuomba Zitto Kabwe kujitoa kugombea ili Freeman Mbowe kupita bila Kupingwa. Jambo hili liliwaumiza Sana wafuasi wa Zitto Kabwe akiwepo Habib Mchange, David Kafulila, Mtemelwa, Nyakarungu, Mtela Mwampamba nk.

Katika uongozi wa Freeman Mbowe mwaka 2004-2010 ilifanyika Operation maarufu Sana "OPERATION SANGARA KANDA YA ZIWA " ambayo ilihusisha Katibu Mkuu Dk Slaa, John Mnyika kama mkurugenzi wa vijana, Zitto Kabwe na Viongozi mbalimbali.

Operation Sangara ilisababisha CHADEMA kuungwa mkono na kupata wabunge wengi Kanda ya ziwa katika majimbo ya Maswa Magharibi, Maswa Mashariki, Bukombe,Ukerewe Musoma mjini, Nyamagana, Ilemela,na majimbo mengine mengi mikoa ya Kagera, Shinyanga, Mwanza

Baada ya Mbowe Kushinda tena kama Mwenyekiti wa CHADEMA (Kupita bila Kupingwa) mwaka 2009 aliongoza chama katika uchaguzi mkuu mwaka 2010 ambapo yeye aligombea tena ubunge jimbo la Hai na kupata kura 28,545(51.63%) huku mgombea wa CCM Godwin Kimbita akipata kura 23,349(42.17%)

Baada ya kushinda ubunge, Mbowe alipewa nafasi ya kuunda serikali Mbadala yaani Kambi Rasimi ya Upinzani Bungeni (KUB/KRUB) huku akisaidiwa na Naibu kiongozi wa kambi rasimi ya Upinzani Bungeni Zitto Zuberi Kabwe ambaye alivuliwa nyadhifa zake mwishoni mwa mwaka 2013, Mnadhimu wa kambi Rasimi ya Upinzani Bungeni Tundu Antipas Lissu nk. Mwaka 2010 mpaka mwanzoni mwa mwaka 2014 Mbowe aliunda serikali Kivuli ya Baraza la mawaziri vivuli (Shadow government) yenye mawaziri vivuli (Shadow ministers) kutoka CHADEMA pekee yake na Mwaka 2014 Mawaziri vivuli waliongezwa kutoka vyama vya NCCR MAGEUZI na CUF.

Kati ya mwaka 2010 mpaka 2014 , Chini ya uongozi wa uenyekiti wa Mbowe, Chaguzi ndogo zimefanyika za udiwani na ubunge. Majimbo ya uchaguzi mdogo wa ubunge ulifanyika katika majimbo ya Igunga, Chalinze, Arumeru Mashariki, Kalenga huku CHADEMA ikishinda jimbo moja la Arumeru Mashariki na mengine kuangukia mikononi mwa CCM

Katika kipindi hicho hicho cha uongozi wa Mbowe 2010 - 2014, CHADEMA imefanya Operation za kichama ikiwepo Vuvuvugu la Mabadiliko (Movement For Change-M4C),CHADEMA ni Msingi, Pamoja DAIMA. Operation hizo zilileta changamoto kubwa kwa siasa za CHADEMA mfano kejeli ya "COPPER TATU KATA TATU"   operation ambayo kwa kiasi kikubwa ilikua ni kudhibiti madhara zaidi ya kufukuzwa Zitto Kabwe ambaye vijana wake walifanya Kazi kubwa kuhujumu CHADEMA Kwa njia halali na za nuruni, gizani na mafichoni ikiwa ni Pamoja na kuchoma bendera za CHADEMA, kadi, kushusha bendera za CHADEMA na kupandisha za ACT Wazalendo na CCM, kutoa matamko ya kupinga CHADEMA na Viongozi, matusi na kejeli nyingi.Hata hivyo Operation hizo zimesaidia CHADEMA kushinda serikali za mitaa nchi nzima ikiwepo kusini pamoja na uchaguzi mkuu mwaka 2015 ambapo CHADEMA na  UKAWA kwa ujumla imevuna majimbo Mtwara, Lindi, Tabora, Tanga, Dar Es Salaam nk ambazo zilikuwa ngome za CCM.

Pia ni kipindi hiki, CHADEMA iliungana na vyama vingine vya CUF, NCCR, ND NA DR ingawa kilijitoa baadaye kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA)  mwezi Septemba 2013 na kuuimarisha zaidi mwaka 2014 na 2015

Septemba 14, 2014,Freeman Mbowe aligombea tena Uenyekiti wa CHADEMA akipambana na Gambaranyere Mwagateka. Katika uchaguzi huo, Freeman Mbowe aliibuka mshindi kwa kupata kura 789 huku mpinzani wake Gambaranyere Mwagateka akijipatia kura 20.

Disemba 14,2014 ulifanyika uchaguzi wa Serikali za mitaa nchi nzima kasoro Sumbawanga mjini na maeneo machache. CHADEMA na UKAWA kwa ujumla ilipata ushindi katika maeneo mbalimbali nchini hata ngome za Ccm. Mfano, Wilaya ya ILEJE ambayo mwaka 2009 CHADEMA ilikua na kijiji kimoja tu Cha Ikumbilo lakini katika uchaguzi wa Serikali za mitaa 2014 ilivuna vijiji 22 na CUF kijiji 1 na kuifanya Ileje kuwa wilaya ya tatu kuchagua CHADEMA Mkoa wa Mbeya. Hali ilikua hivyo Dar Es Salaam, Tanga, Mwanza, Kigoma, Mtwara, Lindi nk

Katika uchaguzi Mkuu mwaka 2015,Freeman Mbowe aligombea ubunge jimbo la Hai na kushinda kata zote 16 kasoro moja ya  17 ambayo uchaguzi uliahirishwa baada ya mgombea kufariki. Mbowe alishinda uchaguzi kwa kupata kura 51,124 huku mgombea wa CCM Dastan Mally akipata kura  26,996,Nuru Muhammed wa  ACT Wazalendo akijizolea kura 315 na  Ndashuka Issa wa APPT - Maendeleo akijinyakulia kura  279.

Katika nafasi ya Urais, Mbowe na kamati kuu walishirikiana kumuingiza Edward Lowassa ndani ya  CHADEMA na kupeleka Jina Lake Baraza kuu na hatimaye kupitishwa na Mkutano mkuu wa CHADEMA tarahe 04/08/2015 kama mgombea urais wa CHADEMA anayeungwa mkono na UKAWA. Lowassa alijipatia kura zaidi ya milioni 6 kwa mujibu wa Tume ya uchaguzi chini ya Jaji Damian Lubuva huku CHADEMA ikisema imeshinda uchaguzi kwa 62% dhidi ya CCM na vyama vinginevyo.

Baada ya uchaguzi Mkuu 2015 , Freeman Aikael Mbowe aliunda Serikali mbadala (Shadow Government) au Kambi rasimi ya Upinzani Bungeni (KUB/KRUB) mapema mwaka 2016 ambayo inahusisha vyama vyote ndani ya UKAWA.....
      
              ******MWISHO******

MAKAMU WA RAIS AMALIZA ZIARA MUSOMA MJINI LEO

$
0
0


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia wakazi wa Musoma mjini kwenye kiwanja cha Mukendo ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake mkoani humo. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia boksi lililohifadhiwa samaki tayari kwa kusafirisha nje ya nchi wakati alipotembelea kiwanda cha Kuchakata Samaki cha Musoma.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kamwe Serikali haitagawa chakula kwa wananchi wavivu ambao hawataki kufanya kazi na kusubiri chakula kutoka Serikalini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassana ametoa kauli hiyo wakati akihutubia mamia ya wananchi wa Manispaa ya Musoma katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mukendo mjini Musoma.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa Serikali itapeleka chakula kwa wananchi ambao mazao yao yaliharibiwa kwa mvua au yalikauka kwa ukame au kwa  maafa mengine na sio kwa wananchi wanaokaa vijiweni mchana kutwa bila kufanya kazi wakisubiri neema ya chakula kutoka kwa Serikali.

Amewahimiza wananchi kote nchini kuendelea kufanya kwa bidii ikiwemo shughuli za kilimo na pindi wanapovuka wajiwekee akiba na waache tabia ya kuuza mazao yote wanayovuka ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa chakula kwenye familia zao.

Makamu wa Rais pia amewataka viongozi wa mkoa wa Mara washirikiane na wananchi katika kuwaelemisha mbinu bora za kilimo ili waweze kupata mazao mengi ikilinganishwa na hali ilivyo kwa sasa.

Kuhusu tatizo la uvuvi haramu, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameziagiza Kamati za Ulinzi na Usalama kufanya misako ya hali na mali katika kupambana na tatizo hilo ambalo limechangia kupunguza samaki katika maeneo mbalimbali nchini.

Ametoa mfano kwa mkoa wa Mara kuwa ulikuwa na viwanda Vinne vya kuchakata samaki lakini kutokana na shughuli za uvuvi haramu na wa kutumia sumu umepelekea viwanda Vitatu kukosa malighafi hiyo na kusitisha uzalishaji.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema jambo hilo ni baya kwa sababu limeikosesha Serikali mapato na kusababisha wananchi wakose ajira kutoka kwenye viwanda hivyo jitihada za makusudi lazima zifanyike katika kukomesha uvuvi haramu katika maeneo mbalimbali nchini hasa katika Ziwa Victoria.

Aidha, Makamu wa Rais ameeleza kufurahishwa na kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji wa Musoma ambao umetekelezwa na Serikali ya Tanzania na Serikali ya Ufaransa  na kusema kuwa mradi huo utaondoa tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa wilaya ya Musoma.
Amewataka wananchi wa Manispaa ya Musoma kuulinda na kuutunza mradi huo ili uweze kudumu kwa miaka mingi kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa Manispaa hiyo.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mara Dakta Charles Mlingwa amewahimiza wananchi wa mkoa wa Mara kuweka itikadi zao kando na washirikiane katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.

Makamu wa Rais katika ziara yake katika wilaya za Butiama na Musoma amekagua shamba la mbegu bora za muhogo katika eneo la Rwamkoma, Butiama na kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Mutex hadi Buhare yenye urefu wa kilomita 9.9 katika Manispaa ya Musoma pamoja na kutembelea kiwanda cha kuchaka samaki cha Musoma.

BULEMBO AFUNGA KAZI WILAYA YA MISENYI NA BUKOBA MJINI MKOANI KAGERA

$
0
0


 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo akiwasili ukumbini kuendesha kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Misenyi, Mabalozi, viongozi wa Jumuia za CCM na watendaji wa Serikali katika Wilaya hiyo mkoani Kagera, leo
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwaili ukumbini.
 Wajumbe wakiwa ukumbini tayari kumsikiliza Alhaj Bulembo

Katibu wa Jumuia ya Wazazi Tanzana, Wilaya ya Misenyi Rehema Mtawala akimkabidhi zawadi maalum Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo kabla ya kikao kuanza
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akionyesha zawadi hiyo maalum baada ya kukabidhiwa. Zawadi hiyo ina maneno ya kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa Mbunge.
 Mwenyekiti wa CCM wa CCM Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Haji Seruhu akifungua kikao hicho
 Katibu wa CCM Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera Mwajuma Mboha, akieleza maneno ya utangulizi katika kikao hicho

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Misenyi Haji Seruhu, wakati wanapita taarifa iliyosomwa na Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo
 Wajumbe wakihamasika kwenye kikao hicho
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na wajumbe wakati wa kikao hicho
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akitulia kumsikiliza kwa makini mshairi Mansur Athan wakati akighani shairi mwishoni mwa kikao hicho
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akipokea zawadi ya Mbuzi aliyopewa na Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Misenyi wakati wa kikao hicho leo.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera Yahya Kateme (kushoto) akibadilishana mawazo na Vijana wa wa CCM nje ya ukumbi baada ya kikao
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Ajhaj Abdallah Bulembo akiendelea kuwasikiliza nje ya ukumbi badhi ya wadau waliotaka ufafanuzi wa baadhi ya mambo baada ya kikao hicho 
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM akiwafafanulia jambo nje ya ukumbi baadhi ya wadau
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj abdallah Bulembo akiendelea kuwasikiliza wadau hata baada ya kupanda gari lake tayari kwa kuondoka

Baada ya wadau kuridhika wakamuaga kwa furaha na kumtakia safari njema kwenda Wilaya ya Bukoba mjini
 Safari ya Alhaj Bulembo kutoka Misenyi kwenda Wilaya ya Bukoba mjini ilipitia kwenye daraja hili la Mto Kagera, eneo la Kyaka.
 Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera Yahya Kateme akizungumza na vijana waendesha bodaboda aliowakuta Bukoba Mjini, baada ya msafara wa Alhaj Abdallah Bulembo kuwasili
 Mwenyekiti huyo wa UVCCM akapiga picha ya pamoja na vijana wa green Guard wa Bukoba mjini
 Baada ya kuwasili tu Bukoba Mjini, Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo alieanda ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Mustafa Kijuu na kuwa na mazungumzo naye kwa muda. Pichani, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo hayo. Wengine kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Lahel Ndegeleki na Mwenyekiti wa CCM mkoa huo Costansia Buhiye
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimweleza jambo Mkuu huyo wa mkoa kabla ya kuondoka
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akiwasalimia vijana wa green Guard nje ya Ofisi ya Mkuu wa mkoa.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimwelekeza jambo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba mjini Yusuf Ngaiza wakati wa kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya hiyo, Mabalozi, viongozi wa Jumuiya na Watendaji wa serikali, leo
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba Mjini mkoani Kagera Yusuf Ngaiza akifungua kikao hicho
                                                       Wajumbe wakiwa ukumbini katika kikao hicho
Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na wajumbe wakati wa kikao hicho Bukoba mjini mkoani Kagera, leo. 
PICHA ZOTE NA  BASHIR NKOROMO

SPIKA NDUGAI APATA UGENI WA BALOZI WA MOROCCO NCHINI TANZANIA PAMOJA NA KATIBU MKUU WA CCM TAIFA LEO OFISINI KWAKE MJINI DODOMA.

$
0
0


Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Balozi wa Morocco nchini Tanzania, Mheshimiwa Abdelilah Benryane (kushoto) pale alipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akizungumza jambo pale alipopata ugeni wa Balozi wa Morocco nchini Tanzania, Mheshimiwa Abdelilah Benryane (kushoto) katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akimsikiliza Balozi wa Morocco nchini Tanzania, Mheshimiwa Abdelilah Benryane (kushoto) katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akisisitiza jambo pale alipopata ugeni wa Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Ndg. Abdulrahman kinana (kulia) katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Ndg. Abdulrahman kinana (kulia) pale alipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akipiga picha ya pamoja na katibu Mkuu wa CCM Taifa, Ndg. Abdulrahman kinana (kulia) pale alipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, kushoto ni katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah.

(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

YANGA NAYO YAONDOSHWA SPORTPESA CUP, ZIMEBAKI TIMU ZA KENYA

$
0
0

FAINALI YA SPORTPESA SUPER CUP NI TIMU ZA KENYA,YANGA YAONDOLEWA NUSU FAINALI

 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MABINGWA Ligi Kuu Tanzania Bara Vodacom (VPL) Yanga leo wameaga amashindano ya SportPesa Super Cup kwa mikwaju ya penati 4-2 katika mchezo wa hatua ya nusu fainali yanayoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Uhuru ulianza majira ya saa 8 kamili kwa kuzikutanisha timu ya Yanga dhidi ya AFC Leopard ya nchini Kenya.Mpaka dakika 90 za mpira zinamalizika timu hizo zilitoshana nguvu kwa kutoka suluhu na kuelekea kwenye mikwaju ya penati.

Timu zote zilionekana kushambulia kwa kupokezana lakini safu za ushambiaji hazikuwa makini na kupoteza nafasi walizozipata mara kadhaa.

Yanga walifanya mabadiliko kwa kumtoa Emanuel Martin na kuingia Said Musa, akatoka Maka Edward na kuingia Said Makapu, Yusuph Mhilu alitoka na kuingia Samwel Greyson na Pato Ngonyani alitoka na kuingia Babu Ally.
AFC Leopard wakafanya mabadiliko kwa kumtoa Abwao Marcus na kuingia Ingotsi Marselas.

Wachezaji waliopiga penati kwa upande wa Yanga ni Nadir Haroub, Obrey Chirwa ambao walipata na Said Makapu na Said Musa kukosa kwa upande wa Yanga.Kwa upande wa AFC Leopard ni golikipa Jan Otieno, Otieno Duncan, Bernad Mango na Katerega Allan ambao walipata na Ingotsi Marselas alikosa.
Beki wa Yanga, Juma Abdul, (kulia) akiruka kuwania mpira na beki wa AFC Leopards Abwao Marcus, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo. Katika mchezo huo AFC Leopards wameibuka na uwashinda wa mikwaju ya penati 4-2 baada ya kumalizika dakika 90 kwa sare ya 0-0.
Mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi (kulia) akiwania mpira na Kiungo wa AFC Leopards, Alan Katerega, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi (kulia) akimtoka mpira na beki wa AFC Leopards, Abdallah Salim, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. 

Mshambuliaji wa Yanga Obrey Chirwa, akijiandaa kupiga shuti huku akizongwa na mabeki wa AFC Leopards, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa Yanga Yusuph Mhilu (kushoto) akimtoka beki wa AFC Leopards, Abwao Marcus, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam

Winga wa Yanga, Yusuph Mhilu (kushoto) akimfinya beki wa AFC Leopards, Abwao Marcus, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji wa Yanga, Juma Mahadhi (kushoto) akichuana kuwania mpira na Abdallah Salim, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam

Mshambuliaji wa Yanga, Juma Mahadhi (kushoto) akichuana kuwania mpira na Abdallah Salim, wakati wa mchezo Nusu Fainali wa mashindano ya SportPesa Super Cup, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam

Mhilu akimkalisha beki wa AFC Leopards



Viewing all 1899 articles
Browse latest View live