Quantcast
Channel: PolitiksiFactTrack ''ARUSHA255''
Viewing all 1899 articles
Browse latest View live

Magdalena Sakaya (Mb) Ndiye Naibu Katibu Mkuu Mpya wa CUF Bara; Mtatiro Ammwagia Sifa Kemkem

$
0
0

Kufuatia kupitishwa kwa Mh Magdalena Sakaya kuchukua nafasi ya Julius Mtatiro kama Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, Mtatiro ameandika ujumbe huu kama salamu za Pongezi kwa Sakaya kwa uteuzi huo. Hii hapa chini isome.

HONGERA MHE. MAGDALENA SAKAYA (MB).

Iam proud of you dada MagdalenaSakaya‬ (MB), NAIBU KATIBU MKUU MPYA, Chama Cha Wananchi CUF - Tanzania Bara.

Wewe pamoja na sekretariati mpya ya chama, nawatakia kila la heri katika majukumu ya kujenga chama chetu.

Nakuahidi wewe binafsi, viongozi na wanachama wetu wote ushirikiano mkubwa sana wakati wote ambapo mtakuwa mkipambana kukijenga chama.

Jambo moja ambalo ni muhimu, mimi naamini sana katika uwezo wa kina mama. Wewe umekuwa mbunge wetu muhimu sana na umeing'arisha CUF ndani na nje ya Bunge.

Natumai kuwa utatumia uzoefu wako mkubwa kukilinda na kukijenga chama katika nafasi ya NAIBU KATIBU MKUU BARA ambayo tumekukabidhi leo.

Nitumie fursa hii pia kuwashukuru viongozi wetu wakuu wa chama, Prof. Lipumba, Juma Duni Haji na Maalim Seif Hamad bila kumsahau Makamu Mwenyekiti mstaafu Mzee Machano Khamis Ali. Katika nyakati zote tulizofanya kazi pamoja nimejifunza mengi kutoka kwenu, nidhamu ya uongozi, uvumilivu, busara, hekima, mashirikiano na mengine mengi.

Miaka mitatu ambayo nimeongoza ofisi ya Naibu Katibu Mkuu Bara nimekuwa mkomavu sana, nimekuwa kiongozi imara na nimechota hekima, busara, uadilifu na nidhamu kutoka kwenu. Kupumzika majukumu haya makubwa ni faraja kwangu na kunanipa sasa muda wa kutosha wa kukamilisha shahada yangu ya tatu ya sheria.

Sitasita kuzidi kutumia uzoefu niliopata kuineza CUF na kuhakikisha inaweka mizizi Tanzania Bara. CUF ni kila kitu kwangu na bado najiona NINA DENI KUBWA katika chama changu, bado leo, kesho na kesho kutwa ntakuwa nafikiria NINI NIKIFANYIE CHAMA CHANGU na siyo CHAMA KINIFANYIE NINI.

Baraza Kuu lililochaguliwa hivi sasa lina uwezo mkubwa sana kuliko lililopita, hili lina wajumbe wengi vijana, wengi wanawake na wazee washauri wachache. Baraza hili litatuvusha vema chini ya uongozi wenu.

Nitazidi kuwa balozi wa chama changu usiku na mchana. Nimekuwa Mkurugenzi wa kitaifa wa chama nikiwa na miaka 26 na nimekuwa Naibu Katibu Mkuu nikiwa na miaka 28, ni nadra sana vijana kupata fursa kwa umri huo. Ni mara chache sana vijana wanaaminiwa kiasi hicho.

Naishukuru sana familia yangu, mke wangu Zakia Hassan na watoto wangu Faustina, Alexander, Elvis na Alma kwa kuwa wavumilivu wakati wote ambapo nilitingwa na majukumu ya kitaifa. Nawashukuru sana ndugu zangu wote ambao walinipa ushauri muda wote, marafiki na wote wenye mapenzi mema na kila aliyekuwa na mchango muhimu katika utendaji wangu.

Julius Mtatiro,
Naibu Katibu Mkuu Mstaafu,
Chama Cha Wananchi CUF,
Tanzania Bara.
28/06/2014.

Naibu Katibu Mkuu Mpya CUF Bara, ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu wa chama hicho Mkoa wa Tabora katika moja ya shughuli zake za kisiasa mkoani humo
Naibu Katibu Mkuu wa zamani Julius Mtatiro Picha Zote na Kapipi Blog!

TASWIRA: VIONGOZI NA WATAALAM WA OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO WAKAGUA MAENDELEO MRADI WA MAKAA YA MAWE MCHUCHUMA

$
0
0

SONY DSC

Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango (wa pili kulia), akipata maelezo juu ya Mradi wa Makaa ya Mawe Mchuchuma kutoka kwa Meneja Utawala Msaidizi wa kampuni ya Tanzania – China International Mineral Resources Limited (TCIMRL) Bw. Israel Mkojera. Pamoja nae ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NDC Bw. Mlingi E. Mkucha (wa kwanza kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Viwanda Mama wa NDC Bw. Ramson Mwilangali (wa kwanza kushoto), Naibu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango Bi. Florence Mwanri (wa pili kushoto), Erasmus Masumbuko, Tume ya Mipango (wa tatu Kushoto).

SONY DSC


Viongozi pamoja na Maofisa kutoka Tume ya Mipango wakiangalia sehemu ambayo makaa ya mawe yanaonekana juu ya ardhi. Kulia ni mhandisi wa madini kutoka kampuni ya TCIMRL. Kampuni hii ni ya ubia kati ya Serikali ya Tanzania, na kampuni ya Sichuang Hongda Group Limited ya China.

SONY DSC

Sehemu ambayo makaa ya mawe yanaoneka kwa juu katika uhalisia wake.

SONY DSC

Shimo hili lilichimbwa mwaka 1956 kwa ajili ya utafiti kuangalia tabaka za makaa ya mawe katika eneo hilo la Mchuchuma.

Picha zote na: Thomas Nyindo.

Msafiri Mtemelwa aomba kuondoka CHADEMA; Hali si shwari tena kwake

$
0
0

msafiri

Msafiri Mtemelwa (pichani) aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Kampeni na Uchaguzi CHADEMA, ameomba kuondoka rasmi kwenye chama hicho. 

Habari ambazo zimetufikia kutoka kwa watu wake wa karibu zinasema kuwa Mtemelewa aliomba kukutana na Katibu Mkuu wa CHADEMA, ili walau apate kitu chochote kutoka kwenye chama hicho kwa maana ya ‘mkono wa kwa heri’, kwa kuwa amekuwa mtumishi wa chama hicho kwa nafasi ya ofisa kwa muda mrefu (tangu alipojiunga na CHADEMA), hivyo afikiriwe katika hali yoyote.

Habari hizo zimezidi kutiririka zikimnukuu Mtemelwa akiwaambia watu wake wa karibu kuwa hakutegemea ushirikiano alioupata katika maombi yake ya kufikiriwa kupewa mkono wa kwa heri kwa kuzingatia nafasi yake aliyokuwa nayo ya Ofisa, ambayo inasemekana kwamba alikuwa na fikra hasi kuwa asingesikilizwa kutokana na matendo yake kwa nyakati tofauti tofauti dhidi ya chama hicho.

Kinyume na matarajio yake, Katibu Mkuu wa CHADEMA alimsikiliza Mtemelwa kuhusu maombi yake, ambapo muombaji alikubaliana na kiwango kilichopangwa kwa kuzingatia maombi yake, huku pia akipewa notice ya mwezi mmoja, kwa maana ya kwamba angelipwa ‘mkono wa kwa heri’ pamoja na stahili ya posho yake ya mwezi mmoja huu wa sita.

Sasa habari kutoka kwa marafiki wake wa karibu (ambao wanamfahamu kwa tabia ya uropokaji na kutotunza neon), wamemnukuu akianza kulalamika namna anavyoshawishiwa afanye mkutano na waandishi wa habari ili eti atangaze kuwa amehama ndani ya CHADEMA lakini anakidai chama hicho.

Maelekezo hayo anayapata kutoka kwa MM na MM 1 (hawa wanajulikana) na kundi lao ambao nao wanapata maelekezo kutoka kwa walioko nyuma yao wanaowapatia fedha za mkakati wa kupambana na CHADEMA.

Kutokana na tamaa ya fedha (ni moja ya sifa zake kama itakavyooneshwa hapo chini), Mtemelwa kasikika akiwaambia rafiki zake kuwa amekubali kufanya press conference kati ya leo Jumapili, Jumatatu ya kesho au keshokutwa Jumanne. Tayari MM 1 yuko anandaa taarifa kwa vyombo vya habari ambayo Msafiri Mtemelwa atatakiwa kuisoma mbele ya waandishi watakapoitwa!

Makubaliano ya kikao hicho ni kwamba ndani ya hiyo taarifa kwa vyombo vya habari, MM 1 atatakiwa kutengeneza kila aina ya uongo anaoweza kadri ya kipawa chake cha kupika mambo kinapoishia. 

Wanasema kuwa uongo au matusi dhidi ya CHADEMA na viongozi wake yatakayosemwa na Mtemelwa yanaweza kuwarubuni watu wachache kwa sababu eti alikuwa Ofisa wa Chama hicho.

Mtemelwa amewahi kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Vijana wa NCCR-Mageuzi kabla ya kuhamia Chadema. Akiwa NCCR alishirikiana na Augustine Mrema kwenye ‘mission’ iliyotumika kukirudisha nyuma kama si kukiua chama hicho, akihusishwa na kikundi hatari maarufu kama Black Mambaz wakati huo. Wadadisi wa mambo wanadai huenda amejiona ni ‘misfit’ ndani ya CHADEMA na hivyo kuomba kuondoka ‘rasmi’ kwenye chama hicho.

Aidha taarifa zinaeleza zaidi  kuwa maboresho yanayoendelea ndani ya CHADEMA ya kujipanga kwa ajili ya majukumu makubwa mbele ya safari, yamekuwa yakimnyima raha kwa sababu atalazimika kurudi kutumikia nafasi yake stahili yaani ya uofisa ambapo angepaswa kuwa chini ya moja ya kurugenzi za chama hicho.

Hiyo inatokana na kwamba chama hicho kimeondoa Kurugenzi ya Kampeni na Uchaguzi katika mfumo wake, kwa sababu kwa namna chama hicho kinavyoendesha shughuli zake na operesheni, wakati wa kampeni za uchaguzi, chama kizima huwa kinahusika, sasa majukumu mengine ya kurugenzi hiyo yakarudishwa chini ya ile Kurugenzi ya Benson Kigaila na machache yamekuwa chini ya Kurugenzi ya Uenezi.

Baada ya kujiona ni ‘misfit’ amefikia hatua ya kuomba aondoke, kuliko kuendelea na nafasi yake ya Ofisa wa Makao Makuu. Kwa mujibu wa vikao vya mamluki na wasaliti vinavyoendelea kufanyika, ameagizwa afanye hiyo press conference ya kutukana CHADEMA, kutukana viongozi na kuzua uongo mwingine, wakati wowote kuanzia sasa, kama alivyofanya akiwa NCCR, TLP, CUF na mara kadhaa alipokuwa hapo hapo CHADEMA.

KITAA WEAR YA MIKE T IKO MTAANI… ANGALIA UBUNIFU HUU

$
0
0

 

Kama umependa KITAA wear cheki na..

--
Mike Mwakatundu
Marketing Manager
SHOWBIZ DEFINED MEDIA Co. Limited,
P.O.Box 6380, Magomeni, Mwembechai
Dar Es Salaam, Tanzania
Skype: mwakatundu.m
F: +255-73-660-4908
M:+255-754-310-202 Whatsapp/ Viber
M:+255-78-470-8944
F: +255-22-217-2454

RPC Arusha akutana na waendesha Bodaboda kusaidia Ulinzi Shirikishi

$
0
0

20140630_103112

Baadhi ya waendesha pikipiki za kubeba abiria Jijini Arusha maarufu kama bodaboda wakiwa katika kikao cha dharula na RPC Sabas katika mjadala uliofanyika Ofisi ya Kata ya Ololrieni ukilenga kuoba ushirikiano wa maswala ya usalama baina ya waendeshaji hao ili kufanikisha ushirikiano baina ya Jeshi la Polisi na wananchi wema katika kuzuia uhalifu Jijini Arusha kupitia mradi wa Ulinzi Shirikishi.20140630_104917

 

20140630_104751

Baada ya kikao waokiondoka kurejea vituoni kwao.

AJTC BINGWA WA BONANZA LA TISA LA TASWA KANDA YA KASKAZINI

$
0
0

washabiki wa timu ya AJTC wakiwa wanashangilia mara baada yakukabidhiwa kombe katika bonanza la Taswa

mwenyekiti wa Taswa Taifa Juma  Pinto akiwa akiwa anakagua timu ya mpira wa pete kutoka AJTC kabla ya mechi ya fainaili kuchezwa

Meneja masoko wa Mega trade, Godluck Kway akitoa  neno ndani ya bonanza hilo

Mkuu wa matukio ya kanda ya kaskazini Bw. Christ Sarakana kutoka TBL akiongozana na meneja masoko na mauzo wa kampuni ya Mega Trade Investment Godluck Kway kukagua timu ya netball ya chuo cha uandishi wa habari AJTC

IMG-20140629-WA0000kikosi cha timu ya mpira wa miguu kutoka cho cha AJTC
IMG-20140629-WA0002
IMG-20140629-WA0003Nahodha wa timu ya mpira wa miguu wa AJTC Bw. Alli Ahmedi akikabidhiwa kombe la ubingwa na Mkuu wa matukio ya kanda ya kaskazini Bw. Christ Sarakana kutoka TBL
IMG-20140629-WA0004
Timu za Chuo Cha Uandishi wa Habari Arusha (AJTC) juzi zilitwaa ubingwa katika bonanza la tisa la waandishi wa habari Kanda ya Kaskazini, lililofanyika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Katika bonanza hilo, ambalo mgeni rasmi alikuwa, Mwenyekiti wa Taswa Taifa, Juma Pinto  jumla ya timu  10 zilishiriki na  liliandaliwa na Taswa Arusha kwa ushirikiano na kampuni ya Ms Unique.
Timu ya soka ya AJTC ilitwaa ubingwa baada ya kuifunga kwa mikwaju ya penati 5-4 timu ya Radio Sunrise, wakati wasichana wa timu hiyo, waliwashinda timu ya chuo cha  uandishi wa habari na maendeleo ya jamii (IMS), magoli 18-5.
Mgeni rasmi Pinto ambaye pia ni Mjumbe wa bodi vya Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro alikabidhi vikombe na fedha taslimu, ambapo bingwa wa  soka alipewa kikombe, pamoja na fedha taslimu 200,000 na seti ya jezi.
Mshindi wa pili wa soka akipata 100, 000 wakati bingwa wa mpira wa pete alizawadiwa kikombe na fedha taslimu 100, 000 huku mshindi wa pili akikabidhiwa tsh 50, 000.
Katika bonanza hilo, ambalo lilidhaminiwa na kampuni ya bia nchini, (TBL), kampuni ya Megatrade Investment, Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro, Cocacola, SBC (T) ltd, AICC, Tanzanite Forever, TANAPA na Alphatel,
Timu zilizoshiriki ni Radio 5, timu ya Arusha One, ORS kutoka mkoa wa Manyara, Salam Club, IMS na  Taswa Arusha  ambayo iliibuka na ushindi katika kukamata kuku.
Akizungumza katika bonanza hilo, Pinto alipongeza washindi na viongozi wa Taswa Arusha kwa kazi  nzuri waliofanya.
“Nachukuwa fursa hii kuwapongeza sana Taswa Arusha kwa kuandaa bonanza hili kwani halifanyiki sehemu nyingine nchini”alisema
Awali Meneja matukio wa TBl, Chris Sarakana aliahidi TBL kuendelea kudhamini bonanza hilo kutokana na kuvutia wanahabari na wakazi wengi wa Arusha.
Meneja masoko wa Mega trade, Godluck Kway aliwapongeza wanahabari kwa kushiriki kwa wingi katika bonanza hilo na kuahidi kuendelea kulidhamini.

 

CHANZO: LIBENEKE LA KASKAZINI

Uchaguzi Serikali za Mitaa shakani Pinda asema hatma yake inategemea mchakato wa katiba

$
0
0

Uchaguzi Serikali za Mitaa shakaniUCHAGUZI wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, upo shakani kufanyika.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akizungumza na mameya wa majiji, manispaa na wenyeviti wa halmashauri za miji na wilaya Tanzania katika kikao cha siku moja kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Regal Naivera jijini Tanga.

Pinda ambaye ni mara yake ya pili kutilia shaka uwezekano wa kufanyika kwa uchaguzi huo, alisema hatma yake kwa kiasi kikubwa inategemea kukamilika kwa mchakato wa katiba mpya.

“Uchaguzi wa Serikali za Mitaa bado ni kitendawili kwa sababu kwa kiasi kikubwa inategemea sana kukamilika kwa mchakato wa Bunge la Katiba,” alisema na kuongeza:

“Kama wizara tunaendelea na maandalizi tukiamini uchaguzi upo, kama hiyo fursa isipotokea bado tutakuwa tumekamilisha maandalizi kwa upande wetu. Tunaendelea kuandaa kanuni kwa kushirikisha wadau wote.”

Kwa mujibu wa Pinda, maandalizi ya uchaguzi huo muhimu ambao unatarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu yanaendelea vizuri.

Hii ni mara ya pili kutilia shaka uwezekano wa kufanyika kwa uchaguzi huo.

Akiwa bungeni, Waziri Pinda aliwahi kutamka kwamba ucheleweshaji wa kupatikana kwa katiba mpya utaathiri uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unaweza kufanyika mapema mwakani.

Aliliambia Bunge kabla ya serikali kuongeza muda wa Bunge la Katiba kwamba watamwomba Rais Jakaya Kikwete aongeze muda wa Bunge la Katiba na endapo litaongezewa muda, litaathiri uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa ratiba, Bunge la Katiba linatarajiwa kuanza mapema Agosti na kuendelea hadi Oktoba na baada ya hapo itafuatiwa na kura ya maoni ili kupata katiba mpya.

Wadadisi wa mambo ya siasa wanasema kuwa ukiangalia ratiba ya Bunge la Katiba, ni vigumu kwa uchaguzi huo kufanyika Oktoba na kuna uwezekano mkubwa ukafanyika mapema mwakani.

Waziri Mkuu yuko Tanga kwa ajili ya sherehe za Serikali za Mitaa ambazo kilele chake kitafanyika leo kwenye viwanja vya Tangamano.

Ameamua kukutana na viongozi hao ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya kukutana nao aliyoitoa Mei 14 mwaka huu wakati akifungua mkutano mkuu wa ALAT.

Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kusisitiza suala la ukusanyaji mapato na udhibiti wa matumizi ya fedha za serikali ambapo alisema katika mwaka wa fedha unaoisha, hali ya ukusanyaji mapato haikuwa nzuri.

Kutokana na hali hiyo, amewaandikia barua wakuu wa mikoa akiwataka waweke utaratibu wa kutoa taarifa kila baada ya miezi mitatu juu ya makusanyo ya halmashauri zilizo kwenye mikoa yao.

“Katika taarifa hizi itabidi kila halmashauri ieleze ilipanga kukusanya kiasi gani, je imefikia lengo na kama sivyo ni kwanini. Nia yetu ni ku-track down makusanyo na kuona yamekwama wapi na yamekwamishwa na nini,” alisema.

Kuhusu udhibiti wa matumizi, aliwataka mameya na wenyeviti hao kuendelea kuwabana wahusika ili kudhibiti matumizi yasiyofaa.

“Lazima muendelee kuwabana na kuwasimamia wakurugenzi na wataalamu wa kwenye halmashauri zenu. Fanyeni kazi kwa ufanisi, msiwachekee wale wanaoharibu.

“Ili muweze kuwabana vizuri, lazima mdai kupatiwa taarifa za fedha kutoka kwa mkaguzi wa ndani (Internal Auditor)… kuna baadhi ya watendaji wanadai kuwa hizi taarifa ni siri wakati siyo siri,” alisema.

Aliwaeleza washiriki wa kikao hicho kwamba taarifa hizo ni muhimu kwao kuzipata na zitawasaidia kuonyesha mapungufu yoyote kama yapo.

Aliwataka kila mmoja wao kwa nafasi zao za meya na mwenyekiti wahakikishe wanalenga kupandisha pato la wananchi wanaowaongoza.

 

CHANZO: TANZANIA DAIMA

TASWIRA: RAISA NDIO REDD'S MISS KANDA YA KASKAZINI 2014

$
0
0

hawa ndio washindi wa redd's miss kanda ya kaskazini kwa mwaka 2014

hawa ni wadhimini wa shindano hilo kutoka minjingu

LEMUTUZ nae alikuwemo ndani ya Redd's miss kanda ya kaskazini  bila kumsahau mwenyekiti wa Taswa Juma pinto

mkuu wa mkoa wa Arusha pamoja na mkuu wa mkoa wa Manyara waliuthuria katika usiku huo wa kumsaka mrembo wa kanda ya kaskazini ambapo katika shindano hilo warembo wanne wamwanzo watakingia katika kambi ya Redd's miss Tanzania

mh hashimu Lundenga akiwa anatangaza washindi wa tatu bora

watembo wakiwa wameingia ukumbini wakicheza wimbo wa ufunguzi

papa mwandago akimwaga maneno akiwa kama muandaaji mkuu wa shindano hili

hawa ndio warembo walioingia tano bora

waandaji wa shindano hilo wakiwa wamekaa kwa mapozi wakifuatilia shindano

PICHA zote na LIBENEKE LA KASKAZINI BLOG


Mamlaka ya Mawasiliano, TCRA yapata cheti cha Kimataifa

$
0
0

tcra2MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetakiwa kuongeza juhudi katika kuboresha sekta hiyo, baada ya kukabidhiwa cheti cha kiwango cha kimataifa na Shirika la Viwango Duniani.

Cheti hicho kilikabidhiwa jijini Dar es Salaam jana, mbele ya wafanyakazi wa TCRA na Mkaguzi wa kimataifa kutoka Uingereza, Andrew Rowe na kumkabidhi Mkurugenzi wa TCRA, Profesa John Mkoma.

Akipokea cheti hicho, Profesa Nkoma, alisema wamepata cheti hicho kutokana na utendaji kazi wa mamlaka hiyo katika kudhibiti mawasiliano nchini.

Alisema umefikia wakati wa sekta hiyo kufanya kazi kwa ufanisi ili ifikapo mwaka 2017, shirika hilo litakapokuja kufanya ukaguzi wakute utendaji kazi upo juu zaidi.

“Cheti tulichopata ni ISO 900:2008, kimetokana na ushirikiano tulionao miongoni mwa wafanyakazi wote na sio mkurugenzi peke yake, tutaendelea kufanya kazi kwa bidii ili kutetea cheti hiki ambacho kinadumu hadi mwaka 2017,” alisema Prof. Mkoma.

Rowe aliitaka TCRA kuhakikisha wanapigania katika utoaji wa huduma bora, ili kuendelea kubaki na cheti hicho kinachowatambulisha kimataifa.

CHANZO: TANZANIA DAIMA

IJUE SAFU MPYA YA KAMATI YA UTENDAJI YA TAIFA (SEKRETARIETI) YA CHAMA CHA WANANCHI CUF

$
0
0

---

1. Naibu Katibu Mkuu (Bara), Mhe. Magdalena Sakaya.

2. Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Mhe. Nassor Ahmed Mazrui.

3. Mkurugenzi wa Mipango na Chaguzi, Mhe. Omar Ali Shehe.

4. Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Chaguzi, Mhe. Shaweji Mketo.

5. Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano na Umma, Mhe. Salim Bimani.

6. Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano na Umma, Mhe. Abdul Kambaya.

7. Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria, Mhe. Kulthum Mchuchuli.

8. Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria, Mhe. Pavu Abdallah Juma.

9. Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha, Mhe. Joran Bashange.

10. Naibu Mkurugenzi wa Uchumi nau Fedha, Mhe. Abdallah Bakari Hassan.

11. Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama (hajateuliwa).

12. Naibu Mkurugenzi wa Uinzi na Usalama, Mhe. Yussuf Salim Hussein.

13. Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, Mhe. Ismail Jussa.

14. Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, Mhe. Abdallah Mtolea.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi-CUF Profesa Ibrahim Lipumba

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi-CUF Maalim Seif Sharrif Hamad

Mgambo wa Jiji Arusha Wanakosa Busara ya Kutekeleza Majukumu Yao Bila Kukwaruzana na Wanajamii

$
0
0

Blog hii ilikutana na tukio hili jana jioni katika pitapita yake katikati ya  mitaa fulani ya Jiji la Arusha. Mgambo wa Jiji wakilazimisha kuondoka na machungwa ya kijana anayeonekana pichani, aliyekataa kuiba na kuamua kujikusanyia sh mia mia halali. Wote majina yao hayakuweza kupatikana haraka.

Pamoja na sheria za kutoruhusu biashara kienyeji mijini, utekelezaji wake ni wa hovyo na kudhalilisha sana, hususani kwa Jiji letu la Arusha. Mgambo wa Jiji wamekuwa wakatili kiasi cha kukosa busara ya kutekeleza majukumu yao bila kukwaruzana na jamii husika.

Kwa mfano, kama nia ni kuwa na mgambo wanaozurura muda wote ili mtu asiweze kufanya biashara pasiporuhusiwa maana yake ni kwamba yeyote akionekana anajaribu anzuiwa.

Sasa ajabu hawa 'law enforcers' wao hawana habari na kwamba wamefanikiwa kumzuia mtu, bali kwao ni lazima wapore na mali zake..mbaya zaidi kama ni za kuliwa wazile. Nikajiuliza hivi siku mtu akaamua kuwategeshea sumu na uroho wao watapona!??

Purukushani ya kupora machungwa yaliyokuwa kwenye ndoo ya kijana huyo anatembea nayo iliishia kujaza umati wa watu na vurugu bila sababu ambapo wangeweza tu kumwamuru aondoke mahala hapo na hata kumuelekeza katazo husika. Baadae machungwa yale yalichukuliwa na raia mmoja aliyeingilia kati na kwenda kuyahifhadhi mahali kwa vile ndio yalikuwa kiini cha mvutano, huku kijana akiwa amepandwa na hasira na mgambo hao nao wakitaka kuonesha nafasi yao.

IMG-20140702-WA0011Hii inatukumbusha pia kukosa weledi kwa baadhi ya askari Polisi wanaokwenda kutawanya kundi la watu mahala fulani na badala yake wanalazimisha kuvunja miguu hata waliotawanyika. Kwamba unakuta amri ya kutawanyika imetolewa na haijatekelezwa. Lengo la amri ni kuwataka watawanyike eneo fulani. Sasa nguvu inaweza kutumika kuwatawanya pengine kwa kupiga mabomu ya kutoa machozi.

Ajabu sasa, wakati watu wale wanakimbia huku na huko kutawanyika kinguvu, unamuona askari anamuandama mtu mmoja tuu hata kama ataingia ndani umbali gani yeye yuko nae, atamkata ngwala, atadondoka chini na kuanza kumvunja miguu na marungu. Unajiuliza hivi lengo ni kuwataka watawanyike ama ni kuwaumiza? Sasa mbona wanamuandama mtu ambaye ameshondoka eneo la tukio?

Wenyewe watakwambia lazima wapate sample za watu wa kushitaki. Lakini hatari yake ni kwamba huishia kukamata hata wasio husika na pengine kuwatia ulemavu bila hatia.

Nadhani jambo la muhimu kwa migambo hawa na askari wengine ni kutimiza wajibu wao kwa kuwatendea binadamu wenzao yaliyohaki huku busara ikitawala zaidi. Kinyume na hapo ni kutengeneza uadui baina yao na jamii!

Taarifa Kwa Umma: Tanzania imeridhia rasmi Itifaki ya Umoja wa Fedha ambayo ni sheria muhimu katika utekelezaji wa hatua ya tatu ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

$
0
0

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

Tanzania imeridhia rasmi Itifaki ya Umoja wa Fedha ambayo ni sheria muhimu katika utekelezaji wa hatua ya tatu ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Itifaki hiyo iliridhiwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  tarehe 25 Juni 2014.

Itifaki ya Umoja wa Fedha ilisainiwa na Wakuu Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Novemba 30, 2013 Jijini Kampala, Uganda wakati wa Mkutano wa 15 wa Kilele wa Wakuu wa Nchi hizo. Baada ya kusainiwa na Wakuu wa Nchi, Nchi wanachama zilitakiwa ziwe zimeridhia Itifaki hiyo ifikapo Julai 1, 2014 ili kuruhusu kuanza kwa utekelezaji wake.

Baada ya kuridhiwa kwa Itifaki, Nchi wanachama zitatakiwa kufuata mpango mkakati wa utekelezaji ambao umeelezwa bayana kwenye Itifaki hiyo.

Utekelezaji wa Itifaki ya Umoja wa Fedha utapelekea Nchi wanachama yaani Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda kuwa na sarafu moja ifikapo mwaka 2024. Ili kufikia hatua ya kuwa na sarafu moja mwaka 2024 baadhi ya mambo muhimu yanayotakiwa kufanyika ni pamoja na uanzishwaji wa Taasisi za Kifedha.

Taasisi hizo ni pamoja na Taasisi ya Fedha ya Afrika Mashariki (ambayo baadaye itakua Benki Kuu ya Afrika Mashariki), Taasi ya Takwimu ya Afrika Mashariki, Tume ya Usimamizi, Ufuatiliaji na Udhibiti na Tume ya Huduma za Kifedha ya Afrika Mashariki. 

Utekelezaji wa Itifaki utahusisha pia uhuishaji wa sera zao za kifedha zikiwemo za kubadilisha fedha, sera za malipo kupitia benki, sera zinazohusu uzalishaji na usambazaji wa takwimu na sera za masoko ya fedha.

Izingatiwe kuwa, kabla ya kuingia kwenye Sarafu moja mwaka 2024, nchi wanachama zitatakiwa kukidhi vigezo vya Muunganiko wa uchumi mpana (Microeconomic Convergence Criteria)  vilivyowekwa ambavyo ni pamoja na:

i. kuwa na mfumuko wa bei usiozidi 8%;

ii. Kuwa na nakisi ya Bajeti isiyozidi 3% (pamoja na misaada);

iii. Kuwa na deni la taifa lisilozidi 50% ya Pato la Taifa;

iv. Kuwa na akiba ya fedha za kigeni ambazo zinatosheleza manunuzi ya bidhaa kutoka nje kwa kipindi cha miezi minne na nusu.

Vigezo hivyo vinatakiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kukaribia 2024. Kama kutakua angalau na nchi tatu za Jumuiya zitakazoweza kufikia vigezo hivyo basi zitaweza kuanza kutumia sarafu moja.

Umoja wa Fedha ni hatua ya tatu ya Mtangamano wa Afrika Mashariki baada ya hatua za awali, Umoja wa Forodha (2005) na Soko la Pamoja (2010) kutekelezwa. Hata hivyo ili hatua ya Umoja wa Fedha iweze kufanikiwa inategemea utekelezaji wa hatua za awali za mtangamano na ushiriki wa wananchi katika kuzitumia fursa zitokanazo na mtangamano. Wizara inawahamasisha Watanzania kutumia fursa mbalimbali zitokanazo na Umoja wa Forodha na Soko la Pamoja.

Imetolewa na

KATIBU MKUU

WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

Habari Mpya: Majambazi yamiminia risasi basi la Magereza na kutorosha wafungwa Jijini Dar

$
0
0

Taarifa ambazo Blog hii imezipata muda mfupi uliopita zinaeleza kuwa Badi la Magereza limeshambuliwa kwa risadi na watu wansodhaniwa kuwa majambazi maeneo ya TMJ Mikocheni Dar es  Salaam.

Taarifa hizo ambazo hazijathibitishwa na Jeshi la Polisi au Magereza zinadai majambazi hayo yanahisiwa kutorosha baadhi ya wafungwa waliokuwa kwenye basi hilo huku askari magereza wa kike hali yake ikielezwa kuwa mbaya kwa kujeruhiwa na risasi kifuani. Inaelezwa kuwa basi hilo lilikuwa linatoka Mahakama ya Mwanzo Kawe na kwasasa limeshikiliwa kituo cha Polisi Oysterbay pamoja na wafungwa waliomo. Idadi kamili ya majeruhi na wafungwa/watuhumiwa waliotoroka haijajulikana bado...

Picha na mdau Martha Mtiko

Nassari Azuru Fayetteville-Arkansas Marekani na Kujionea Kikao cha Halmashauri ya Mji Kinavyoendeshwa

$
0
0

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Mh Joshua Nassari ameweza kutembelea mji wa Fayetteville-Arkansas na kujionea namna vikao vya Halmashauri za Miji zinavyoendeshwa huku wajumbe wakitanguliza maslahi ya umma kwanza. Nassari yupo nchini Marekani kwa ziara ya mafunzo kwa viongozi vijana kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Pichani akiwa na Viongozi vijana wenzake kutoka Afrika; Eric Bukasa Ntumba ( DRC), Piet (Namibia), Dr. Gwamaka Kifukwe PhD(Tanzania), Joshua Nassari ( Tanzania)
Hapa akiwa na Mwakilishi wa Arkansas Bw Grag Leding kupitia chama cha Democrats cha Rais Obama. Akiwa katika mji wa Fayetteville Arkansas, alipata wasaa wa kujifunza mengi toka kwa wenyeji namna wanavyoendesha Serikali za Mitaa. Nassari anaeleza kuwa Mwakilishi Leding alichaguliwa akiwa na miaka 32 tu na hakuwa ameoa. Alikuwa ni mtu wa kawaida asiyefahamika kwenye siasa za mji huo, sifa ambazo zinawiana na namna Nassari alivoibuka na kutwaa Ubunge wa Arumeru Mashariki ambako anafanya uwakilishi mzuri Bungeni.

Cargo plane crashes into building in Kenya shortly after takeoff in Nairobi, 4 people were killed

$
0
0

Policemen and firefighters search in the wreckage of a cargo plane which crashed at a commercial building in a Nairobi suburb shortly after takeoff early Wednesday.

NAIROBI, Kenya — Four people were killed when their cargo plane crashed shortly after takeoff in Nairobi, a police official said Wednesday.

The plane transporting the mild stimulant known as Khat to the Somali capital, Mogadishu, crashed into a commercial building after taking off from Jomo Kenyatta International Airport early Wednesday, said Joseph Ngisa, the airport's head of police investigations.

Ngisa said preliminary investigations found the plane was flying low after takeoff and might have hit an electrical pole before crashing in the Embakasi area of the city.

Ngisa said the four on board included the pilot and his assistant.

Source: Kenyan Daily News 
******************************

UPDATES NA SALAAMFM

Idadi ya waliofariki kwenye ajali ya ndege jijini Nairobi imeongezeka hadi watu saba

ndege 2

Idadi ya waliofariki kwenye ajali ya ndege inayomilikiwa na shirika la Skyward katika eneo la Utawala, kaunti ya Nairobi imefikia saba.

Hii ni baada ya polisi kupata miili zaidi iliyokuwa kwenye mabaki ya ndege hiyo iliyoanguka kwenye jengo moja la makaazi.

Miongoni mwa waliofariki ni marubani wa ndege hiyo na wahudumu wengine waliokuwemo kwenye ndege hiyo. Walinzi wawili wanauguza majeraha kuhusiana na ajali hiyo na wamelazwa hospitali ya Mama Lucy Kibaki jijini Nairobi.
Kulingana na kamanda wa polisi wa kaunti ya Nairobi Benson Kibue, ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa kumi alfajiri, siku ya jumatano bila kufichua chanzo cha ajali hiyo.

Ndege hiyo  ilikuwa inaelekea jijini Mogadishu, nchini Somalia huku ikisafirisha miraa.


TASWIRA KUTOKA OFISI YA RAIS: TUME YA MIPANGO YAKAGUA MRADI WA MAKAA YA MAWE NGAKA

$
0
0

Viongozi na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na wale wa NDC wakipata maelezo kuhusu mradi wa makaa ya mawe Ngaka kutoka kwa Mtaalam wa Kudhibiti Ubora (Quality Control Superintendent) Bw. Boscow R. Mabena.Timu kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na NDC wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kikundi cha Wanawake cha Mbalawala, Bi. Joyce Haule juu ya matumizi ya makaa ya mawe majumbani. Makaa hayo hutumika majumbani kwa kutumia majiko maalum baada ya kubadilishwa kitaalam na kuwa rafiki kwa matumizi ya majumbani. Mbalawala kinajihusisha na shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwa ni jitihada za kumkwamua mwanamke kiuchumi. Majiko maalum yanayotumia mkaa uliotokana na makaa ya mawe kwa ajili ya kupikia majumbani. Mtaalam wa Kudhibiti Ubora, Bw. Boscow R. Mabena akitoa maelezo namna ambavyo Coal Briquett Machine (Pichani) hutumika kubadili makaa ya mawe kutoka hali yake ya mwanzo baada ya kuchimbwa na kutengenezwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Picha na: Thomas Nyindo, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango (ORTM), Dkt. Philip I. Mpango, (wa tano kutoka kushoto) akikagua Mradi wa Makaa ya Mawe Ngaka. Wengine ni viongozi na maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na Shirika la Maendeleo la Taifa – NDC pamoja na wataalam wa kampuni ya TANCOAL inayojishughulisha na uchimbaji wa makaa ya mawe. Viongozi na Maofisa kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na NDC wakiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Kampuni ya TANCOAL ndani ya mgodi wa makaa ya mawe. Kampuni ya TANCOAL ndiyo inayohusika nauchimbaji wa makaa ya mawe katika Mradi wa Mkaa ya Mawe Ngaka.

 

Picha na: Thomas Nyindo, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.

BOMU TENA ARUSHA: SHEIKH ALIPULIWA AKILA DAKU NYUMBANI KWAKE

$
0
0

sheikh

 Sheikh wa Msikiti wa Qiblatan,Sood Ally Sood (37) uliopo Kilombero jijini Arusha amejeruhiwa kwa bomu la kurushwa kwa mkono alipokuwa akila daku nyumbani usiku wa kuamkia jana.

Pamoja na Sheikh Sood, mtu mwingine aliyekuwa nyumbani kwake,aliyetajwa kwa jina la Muhaji Kifea (38) mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam pia amejeruhiwa katika tukio hilo na wote wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwa matibabu.

Sheikh alijeruhiwa miguu yake yote na mapajani huku Kifea akipata majeraha makubwa miguuni na kupoteza baadhi ya vidole vya miguu yote.

Akizungumza hospitalini hapo, Sheikh, Sood alisema tukio hilo lilitokea nyumbani kwake eneo la Majengo ya chini, usiku wa kuamkia jana saa 5:00 wakati yeye pamoja na mgeni wake walikuwa wakila chakula sebuleni.

“Nikiwa sijui hili wala lile nilishtushwa na mlipuko ulioambatana na vyuma mbalimbali vilivyokuwa vikiruka hewani ambapo bomu hilo linaelezwa kuwa ni guruneti lililorushwa kupitia dirishani baada ya watu wasiofahamika kufanikiwa kuvunja kioo cha dirisha la chumba tulichokuwamo,” alisema Sheikh Sood.

Alidai anawajua waliotekeleza shambulio hilo kwa sababu amekuwa akipokea vitisho kutoka kwa watu anaowafahamu na tayari alikuwa ametoa taarifa kwa vyombo vya dola.

Alisema kuwa siku tatu kabla ya tukio hilo alikoswakoswa kupigwa risasi na watu wasiofahamika wakati akitoka msikitini na akatoa taarifa Kituo Kikuu cha Polisi jijini Arusha kuhusu tukio hilo. Sood anasema kuna baadhi ya vijana anawatuhumu juu ya matukio hayo.

Sheikh huyo ambaye ni Kiongozi wa dhehebu la Answar sun Kanda ya Kaskazini amekuwa akitofautiana na waumini wenzake kutokana na msimamo wake wa kutokukubaliana na baadhi ya waumini wenye msimamo mkali wa msikiti huo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,  Magesa Mulongo alikemea matukio ya mabomu yanayolitikisa Jiji la Arusha katika siku za karibuni na kuviagiza vyombo dola kufanya uchunguzi wa kina kubaini wahusika wote ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

“Uchunguzi wa awali unaonyesha tukio hili limetekelezwa na watu walio karibu na Sheikh. Polisi wanaendelea na uchunguzi kwa sababu baadhi ya watu wanaotajwa kuhusika kwenye tukio hili pia ni miongoni mwa watuhumiwa kwenye matukio mengine ya milipuko ya bomu Arusha,” alisema Mulongo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatusi Sabasi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa majeruhi wanaendelea vyema huku polisi wakiendelea na uchunguzi wa kina kuwabaini wahusika.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alielezea kusikitishwa na matukio ya milipuko ya mabomu Arusha na kuliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina kuwakamata wahusika bila kujali vyeo, nyadhifa, dini, itikadi wala rangi zao. Kinyaiyas Blog inajiuliza haya mambo ya kulipuana kila kukicha na haswa mkoani Arusha yataisha lini wkt nchi yetu na watu wake hatujazoea hayo mambo jamanii...

 

STORI NA: BEN KINYAIYA

Sinema la Mchana: Polisi Arusha Waua Watatu Wanaodhaniwa Kuwa Majambazi Waliokuwa Wamejipanga Kupora Mamilioni ya Fedha

$
0
0

JESHI la polisi mkoani hapa limewaua majambazi watatu waliokuwa wamepanga njama ya kwenda kupora mamilioni ya fedha zilizokuwa zinapelekwa benki na kampuni ya Arusha Islamic Centre inayohusika na utengenezaji na uuzaji wa vigae iliyopo eneo la Esso  mjini hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas alisema kuwa,majambazi hao watatu  waliuawa jana tarehe 3 eneo la TBL –Njiro  wakiwa kwenye harakati za kwenda kupora fedha hizo.
Alisema kuwa, majambazi hao walikuwa mahali wanapanga njama majira ya saa 4;20 asubuhi wakisubiria kuteka gari lililokuwa limebeba  fedha zilizokuwa zinapelekwa benki zaidi ya milioni 100  huku wakiwa na gari aina ya Toyota Corola yenye namba za usajili T 762 CWE.
Alisema kuwa, raia wema walitoa taarifa kuhusiana na tukio hilo ndipo  polisi walifika eneo ambalo majambazi hao walikuwa wamejificha katika  eneo la unga ltd relini ambapo majambazi hao walishtuka na kuanza kuirishia gari hiyo ya polisi risasi.

Ambapo majibizano yalianza kati ya majambazi hao na polisi huku wakirushiana risasi hadi eneo la TBL njiro ndipo majambazi walipofika eneo hilo waliamua kutelekeza gari na  kushuka chini  na kumimina risasi kwa askari polisi  hao.
Kamanda Sabas alisema kuwa,hatimaye polisi waliweza kuwauawa majambazi hao  na kufanikiwa kuchukua silaha yao aina ya shortgun yenye namba A 947514 M aina ya  Pumpaction ikiwa na risasi 3 .
Kamanda alisema kuwa, bado majina ya majambazi hayo hayajafahamika ambapo wanakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 30 na miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya mount Meru.
Aidha Kamanda aliwashukuru wananchi kwa juhudi kubwa sana walizoonyesha na ushirikiano hadi kukamatwa kwa majambazi hayo na kuwataka kuendelea kuongeza juhudi hizo zaidi.

 

STORI: LIBENEKE LA KASKAZINI

PICHA:  SERIA

Gari iliyokuwa na majambazi hayo baada ya kushamuliwa kwa risasi na mmoja kuuawa.

Jambazi mmojawapo aliyeuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya gari

Jambazi mwingine aliyeuawa eneo la jirani ba Baclays Bank jijini Arusha

Askari wakilikagua gari hilo.

Ajali Uwanjani: Neymar kukosa mechi zilizosalia za Kombe la Dunia baada ya kuvunjika mgongo

$
0
0

10369968_810642448954422_6734748977862256253_n

 

Nyota wa timu ya soka ya Brazil Neymar hatoshiriki tena katika michuano ya kombe la dunia baada kupata jeraha.

Mfupa wake unaoshikana na uti wa mgongo ilivunjika katika mechi ya ushindi wa mabao mawili dhidi ya Colombia.

Neymar aligongwa upande wake wa nyuma dakika tano tu kabla ya mchuano huo wa robo fainali kukamilika.

Alibebwa na kutolewa nje akiwa katika machela lakini ametolewa hospitalini baada ya kufanyiwa matibabu.

Brazil pia itaendelea kushiriki katika mashindano hayo bila nahodha wake Thiago Silva katika mchuano wa nusu fainali dhidi ya Ujerumani baada ya mchezaji huyo kupewa kadi ya pili ya Njano.

Kabla ya habari hizo za Neymar kutolewa raia wa Brazil walifurika katika barabara za taifa hilo kusherehekea ushindi wa timu yao.

Katika robo fainali ya kwanza Ujerumani iliishinda ufaransa kwa bao moja kwa bila .

 

Chanzo: BBC Swahili

UNAFIKI na USALITI wa Mwigamba dhidi ya tuhuma za ukomo madaraka katiba ya CHADEMA.

$
0
0

UNAFIKI na USALITI wa Mwigamba dhidi ya tuhuma za ukomo madaraka katiba ya CHADEMA.

Nimeamua kuandika kidogo kikombe kisinipite ili kuanika unafiki wa Mwigamba na marafiki zake (Kitila na Zitto), Mwigamba na maswahiba zake (viruka njia wa usaliti) ambao walisaliti ndani ya CHADEMA na baadae kuibuka na uzushi kuwa kipengele cha 6.3.2 (c) kinacho zungumzia muda wa uongozi kwenye katiba ya chama kuwa kimewekwa kinyemela. Kipengele hicho (6.3.2 (c), kinasema "kiongozi aliye maliza muda wa uongozi ana haki ya kugombea na kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza masharti ya kuchaguliwa kuwa kiongozi"
Mwigamba anasema kipengele hicho kimeongezwa kinyemela huku akijua alishiriki/wameshiriki kwenye kuifanyia mabadiliko katiba ya chama ya 2004 na kuanza kutumika rasmi kwa katiba ya 2006 iliyokuja na kipengele hicho.

Mwigamba pamoja na wajumbe wengine akiwemo rafiki yake (MM) tarehe 13/8/2006 wakiungana na wajumbe wengine wa mkutano mkuu kwa pamoja walisema "...Sisi wajumbe wa mkutano mkuu tumeamua kuifanyia mabadiliko katiba ya 2004 ya chama chetu cha siasa kinachoitwa CHADEMA ili kuipa sura inayoendana na mtazamo na msukumo mpya wa falsafa yetu ya nguvu na mamlaka ya umma na dira na dhamira ya chama kuanzia 2006 na kuendelea. Kuanzia sasa CHADEMA kitaendeshwa kwa mujibu wa katiba hii sambamba na kanuni, taratibu na maadili ya chama...". Mwigamba na Zitto walitamka kwa pamoja maneno hayo wakiwa na wajumbe wengine wa mkutano huo.

Msijiulize kwa nini kwenye hili nawaongelea wote wakati aliyepeleka malalamiko kwa msajili alikuwa Mwigamba peke yake! ukweli ni kwamba utatu huu wa kisaliti nauongelea pamoja kwenye sakata hili kwa kuwa nyendo zote chafu za kisaliti kwa sasa huwezi kuwatenga! Wanaruka pamoja, wanakutana na kupanga pamoja na mawasiliano yao makubwa pamoja na mataniboi wao wa kisiasa ni kuidhoofisha CHADEMA kuliko kuimarisha chama chao kinacho undwa na viongozi walio saliti CHADEMA. Uhakika nilio kuwa nao, watashindwa kama walivyo shindwa kupitia walicho kiita "Mkakati wa mabadiliko 2013".

Mwigamba kupitia gazeti la Mtanzania la tarehe 2/7/2014 alinukuliwa akimshukuru Mungu kwa ofisi ya msajili kwa alicho kiita "..kusimamia na kueleza ukweli wanachama wa CHADEMA kuhusu kuondolewa kinyemela kwa kipengele cha ukomo wa madaraka.." akanukuliwa zaidi akisema "...CHADEMA walinifukuza uwanachama wakiamini kuwa hoja ya kuvunja katiba niliyo iwasilisha kwa msajili itatupwa na hatimaye amejiridhisha kuwa walikuwa wamevunja katiba ya chama chao..."


Maelezo ya Mwigamba yamejaa unafiki na hadaa zilizotawaliwa na dhambi ya usaliti! Usaliti wa kukisaliti CHADEMA na sasa anajisaliti na yeye mwenyewe! Hebu msome katikati ya mstari hapa "...hatimaye msajili amejiridhisha kuwa walikuwa wamevunja katiba ya chama chao..." utadhani marekebisho hayo yamefanyika yeye akiwa tayari kashasaliti na kwenda ACT!
Kuna haja watu wajue, huyu Mwigamba alikuwa nani ndani ya CHADEMA kabla ya kufukuzwa chamani kwa dhambi ya usaliti kupitia mkakati wa mabadiliko na unafiki wa kumsifu mwenyekiti Mbowe kwa kuendesha chama kwa ufanisi na ubunifu kwenye mkutano wa kanda ya kaskazini pale Corridor Spring (Arusha) Novemba 2013 akiwa anawasilisha ripoti ya mkoa wake (Arusha) huku robo saa baadae akimkashifu na kumtukana Mh Mbowe kupitia akaunti yake bandia ya 'Mkulima maskini' kwenye mtandao wa jamiiforums.
Mwigamba alikuwa nani kabla ya kusaliti CHADEMA?


1. Mwigamba aliwahi kuwa mwanachama na kiongozi wa CHADEMA mkoa wa Arusha mpaka alipo vuliwa nafasi zake zote za uongozi Novemba 2013.

2. Aliwahi kuwa mhasibu wa chama makao makuu kuanzia 2011 hadi 2012 alipo simamishwa kazi na makao makuu kutokana na matatizo mbalimbali moja kubwa likiwa kushindwa kuleta ripoti ya matumizi ya fedha alizopewa wakati wa uchaguzi mdogo wa Igunga ambapo zaidi ya milioni 210 zilitumika.


3. Alishiriki kwenye mkutano mkuu wa tarehe 13/08/2006 uliopitisha mabadiliko ya katiba toleo la mwaka 2006 akiwa mjumbe kutoka mkoa wa Arusha (kwa mujibu wa kumbukumbu za mahudhurio).


4. Amekuwa mjumbe wa vikao vya baraza kuu la chama toka 2009 alipo chaguliwa kuwa mwenyekiti wa mkoa wa Arusha na amekuwa akishiriki vikao mpaka Nov 2013 alipo vuliwa nyadhifa zote ndani ya chama.


5. Amekuwa mjumbe wa vikao vya mkutano mkuu wa chama toka 2006 na amekuwa akishiriki kwenye mikutano mikuu mpaka Novemba 2013 alipo vuliwa nyadhifa zote ndani ya chama.
Lakini kubwa la muhimu ni kwamba, yeye na Kitila Mkumbo ndio walikuwa wanamtandao wakubwa na waandaji wa mkakati wa mabadiliko 2013 kinyume na maadili, itifaki, miongozo na katiba ya chama kwa ajili ya rafiki wao anaye kamilisha UTATU wao wa wasaliti. Lakini pia hawaja wahi kulalamika kwenye kikao chochote kuhusiana na kipengele cha ukomo wa ungozi ndani ya kikao chochote cha kikatiba.

Usaliti na hadaa za Samson Mwigamba na utatu wao wa kisaliti ni upi?!
Pamoja na kujua kuwa alishiriki mchakato mzima wa mabadiliko ya katiba ya chama yeye na rafiki yake anajua kuwa:
1.0 wapo viongozi ndani ya CHADEMA ambao waliweza kuwa na haki ya kugombea na walichaguliwa upya kwa zaidi ya vipindi viwili na hakuja wahi kuwa na mgogoro kwani katiba ya chama ilifuatwa kwa ukamilifu wake.

Viongozi hao ni nani na wanatokea mikoa na kanda ipi?
1.1. Alhaji Ramadhani Kasisiko - mwenyekiti wa mkoa wa Kigoma na rafiki mkubwa wa Zito Kabwe. (Inasemekana hata Hijjah alimpeleka yeye).

1.2. Kansa Mbarouk - mwenyekiti wa mkoa Tabora, huyu ni ndugu na Athuman Balozi (Tabora) aliyesoma tamko fake la waliojiita wajumbe wa baraza kuu na mkutano mkuu pale Lamada Hotel na baadae wakaandamana kwenda kwa msajili na CAG.


1.3. Msafiri Wamalwa - Katibu mkoa wa Kigoma.
Viongozi hawa wote watatu hapo juu wanatokea kanda ya Magharibi (Tabora, Kigoma na Katavi) ambako pia ni kanda aliyokuwa anatoka MM na Mzee Said Arfi.
Kwa maana hiyo, kama Mwigamba angekuwa na dhamira safi angemuuliza rafiki yake wa makakati wa mabadiliko aliyempa jina la MM au ange muuliza mzee Said Arfi uhalali wa viongozi hao ambao walichaguliwa zadi ya vipindi viwili.


2.0. Kama dhamira ya Mwigamba ingekuwa haiteswi na dhambi ya usaliti angejiuliza uhalali wa viongozi wengine ambao ni


2.1. Aliyekuwa mwenyekiti wa mkoa wa Singida na rafiki wa MM ambaye anaitwa
Nobert Kitundu japo alikuja kujiuzuru kutoka na sakata la MM (huyu baadae aliomba kurudi kuwa mwanachama wa kawaida baada ya kukiri kuwa alipewa hela ili ajiuzuru kwenye ule upepo wa kujiuzuru ambao baadae ulikwama).

2.2. Mwingine ni Mzee Stephen Massawe wa mkoa wa Dodoma ambaye mpaka sasa ni katibu wa mkoa wa Dodoma na alipasifa za kugombea tena baada ya mabadiliko ya katiba 2006 ambayo Mwigamba naye alishiriki mchakato wa mabadiliko yake.

Viongozi wote hapo juu wanatokea kanda ya kati yenye mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida, kanda ambayo anatokea Dr Kitila Mkumbo ambaye ni rafiki mkubwa wa Mwigamba waliye shirikiana kuandaa mkakati wa mabadiliki 2013 na ndio wanaunda utatu wa kisaliti wakishirikiana na MM.
Kama Mwigamba hakuwa na nia ovu, kilicho mzuia asimuulize rafiki yake kwenye utatu wa kisaliti (Dr Kitila) ni nini?!

Itoshe kusema kuwa, pamoja na viongozi hao hapo juu lakini pia wapo viongozi wengine kama marehemu Philiph Magadula Shilembi ambaye naye alishika uongozi kwa kuchaguliwa zaidi ya vipindi viwili, kama mtakumbuka huyu marehemu alisha wahi kuandikiwa makala nzuri sana na MM na Mwigamba mara baada ya kifo chake. Yupo pia mzee Shilungushela kutoka Shinyanga ambaye pia mwenyekiti taifa baraza la wazee ambaye naye alichaguliwa kwa kipindi cha tatu, Shilembi na Shilungushela wanatokea kanda ya ziwa Mashariki yenye mikoa ya Shinyanga, Simiyu, na Mara.


Viongozi wengine walio chaguliwa kwa vipindi zaidi ya viwili ni pamoja na mzee Ndesamburo mwenyekiti wa mkoa wa Kilimanjaro na Mh Conchester Rwamlaza (MB) ambaye ni katibu wa mkoa wa Kagera.
Nabaki najiuliza?!


1. Kwa nini Mwigamba na utatu wake mtakatifu pamoja na mataniboi wao wa kisiasa hoja yao iwe kwa viongozi wa chama taifa wakati kipengele cha ukomo wa madaraka kama kingekuwepo kingehusu viongozi wote mpaka kwenye ngazi ya misingi, matawi, kata, wilaya na hata mikoa na si mwenyekiti na katibu mkuu taifa pekee?!


2. Kwa nini Dr Slaa ahusishwe na kushambuliwa wakati nafasi yake ya ukatibu mkuu na manaibu wake ni nafasi ya uteuzi na si nafasi ya kugombewa na kupigiwa kura?! Nini kimejificha kumuongelea Dr Slaa na wakati huohuo kumuongelea Mh Mbowe wakati mmoja anapigiwa kura na mwingine anateuliwa?! Kumbuka hata rafiki wa Mwigamba kwenye utatu wa usaliti (MM) hakuchaguliwa bali aliteuliwa na mwenyekiti kwenye miongoni mwa majina yaliyo wasilishwa kwake kwa uteuzi na hivyo akawa naibu katibu mkuu bara.

3. Kwa nini rafiki na collegemates wa MM pale udsm ambaye naye ni rafiki na Sisty Nyahoza ambaye ni mhudumu wa ofisi ya msajili waongee lugha moja na kundi lote la utatu wa usaliti kuhusu kipengele cha ukomo wa uongozi?! Lugha moja wanayoongea nikwa bahati mbaya au kuna ka mpango nyuma ya pazia kampango ambako msajili wa vyama jaji Mutungi amejikuta anaingizwa king na ameshtuka akiwa kwenye kilinge cha tope?!


4. Mbona utatu wa usaliti hauongelei mabadiliko ya bendera ya chama pamoja na mabadiliko makubwa yaliyo huisha mfumo wa chama kizima na wamejikita kwenye kipengele kimoja tu ambacho bado ni halali kama vipengele vingine wasivyo taka kuviongelea vilivyo halali?! Nashangaa kwa nini hawaongelei mabadiliko ya bendera, organisation ya chama pamoja na Redbrigade iliyopigiwa kelele na CCM ambayo haikuwemo kwenye katiba ya 2004?!

5. Kama wameamua kusaliti uwepo wao na ushiriki wao kwenye mabadiliko ya chama wakiwa na akili timamu, nani anaweza kusema kuwa watu hawahawa kuwaita kuwa ni wenye kuungana na kuunda utatu wa usaliti na kuanzisha chama chenye kuundwa na viongozi walio saliti CHADEMA hawapaswi kuitwa kwa jina lingine kuwa wao ni Alliance for Cowards and Traitors yaani kwa kifupi ACT?!

IMEANDIKWA NA: MOHAMED MTOI

Viewing all 1899 articles
Browse latest View live