Quantcast
Channel: PolitiksiFactTrack ''ARUSHA255''
Viewing all 1899 articles
Browse latest View live

Mapokezi ya Mbunge Nassari KIA yalivyofana

$
0
0

Mbunge wa Arumeru Mashariki amewasili akitokea Marekani na kulakiwa na viongozi mbalimbali wa Chadema na wananchi katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa KIA


Taswira za awali: Mkutano wa Chadema Arusha kutambulisha safu mpya ya Uongozi wa Jimbo la Arusha Mjini

$
0
0
Chadema wamefanya mkitano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Kilombero-Samunge kuwatambulisha viongozi mbalimbali wa Jimbo la Arusha Mjini

RAIS KIKWETE AWAPA ZAWADI FIGO NA WACHEZAJI WA REAL MADRIS

$
0
0
D92A7880[1]

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi ya kinyago mchezaji veterani wa timu Real Madrid Luis Figo wakati wa hafla ya chakula cha jioni aliyowaandalia wachezaji wa timu hiyo na timu ya maveterani ya Taifa Stars ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku baada ya mechi ya kirafiki ambapo Real Madrid illifungaTaifa Stars 3-1 katika uwanja wa Taifa.(picha na Freddy Maro).

CREDIT: VIJANA NA MATUKIO

HABARI PICHA-WATAALAMU WA UMEME WAKIZUNGUMZA NA WANANCHI WAISHIO VIJIJINI JUU YA MPANGO WA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI

$
0
0

SSA51115Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja ,TANESCO Arusha,Benedict Nkini (wakwanza kulia) akifafanua jambo juu ya kifaa cha kujiunganishia umeme bila kusambaza waya kinachofahamika kitaalamu kama Ready Board ,kulia ni Afisa Masoko  wa Tanesco,Adelina Lyakurwa akiwa ameshika kifaa hicho ,pia  walizungumza na wananchi wa Vijiji vya Meserani juu na chini  kuhusu  mpango wa kuwaunganisha wananchi waishio vijijini  na huduma ya umeme kwa unaotekelezwa kwa awamu ya pili katika wilaya za Arumeru,Karatu,Monduli na Longido uliofadhiliwa na REA , lengo ni kuhakikisha wananchi waishio vijijini wanafikiwa na huduma hiyo muhimu.zilizopo mkoani Arusha.


SSA51059Afisa Masoko  wa Tanesco,Adelina Lyakurwa akiwa ameshika kifaa cha kujiunganishia umeme bila kusambaza waya katika nyumba  kinachofahamika kitaalamu kama Ready Board ,wakati akizungumza na wananchi  wa Vijiji vya Meserani juu na chini  kuhusu  mpango wa kuwaunganisha wananchi waishio vijijini  na huduma ya umeme kwa unaotekelezwa kwa awamu ya pili katika wilaya za Arumeru,Karatu,Monduli na Longido unaofadhiliwa na REA  lengo ni kuhakikisha wananchi waishio vijijini wanafikiwa na huduma hiyo muhimu.zilizopo mkoani Arusha.

Picha na Ferdinand Shayo

VIJIJI 120 KUFIKIWA NA UMEME

Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Vijiji 120 vilivyopo mkoa wa Arusha vinatarajia kufikiwa na huduma ya umeme kupitia mpango wa kusambaza umeme vijijini unaofadhiliwa na (REA) na kutekelezwa na shirika la umeme la taifa (TANESCO).

Afisa Uhusiano na Huduma kwa wateja ,TANESCO Arusha,Benedict Nkini amesema kuwa wako katika awamu ya pili ya utekelezaji wa mradi huo wa umeme vijijini na kwasasa wanaelekea katika wilaya za Arumeru,Karatu,Monduli na Longido lengo ni kuhakikisha wananchi waishio vijijini wanafikiwa na huduma hiyo muhimu.

Benedict Nkini akizungumza katika mkutano na Wananchi wa Vijiji vya Meserani juu na chini amesema kuwa kwa sasa wako katika hatua ya kutoa elimu kwa wananchi juu ya mradi huo ili waweze kujiandaa kuunganishwa na huduma hiyo na pia amewataka waepuke vishoka ambao hutumia uelewa mdogo wa wananchi kujinufaisha.

Afisa Masoko wa Tanesco,Adelina Lyakurwa amesema kuwa amewaomba wananchi kutumia fursa hiyo kuunganishiwa umeme huo wa bei nafuu ambao Mtanzania wa hali ya chini anaweza kuumudu ,ambapo Mwanakijiji atatakiwa kuwa na kiasi cha shilingi 32900 ili aweze kuunganishiwa umeme.

“Tunawaunganishia umeme watu wote wenye nyumba za mawe,matofali,mbao kwa hiyo tunawaomba wananchi watoe ushirikiano ili kufanikisha mradi huu,kwa upande wa nyumba za nyasi na makuti kunahitajika ushauri wa kitaalamu kwasababu za kiutaalamu ili kuepuka moto ambao unaweza kutokea kutokana na hitilifu ndogo” Alisema Afisa Masoko

Kaimu Mkurugenzi wa TANESCO wilaya ya Monduli ,Ramadhani Mkayala amewataka wananchi watafute wakandarasi wazuri waliodhinishwa na shirika ili kuepuka vihatarishi vya moto

Kwa upande wao wananchi wa Wilaya ya Monduli Sophia Mligo wa kijiji cha Miserani na Gasper Lengta wamesema kuwa wameupokea mpango huo vizuri na kuwaomba TANESCO wazidi kufanya ushirikishaji zaidi na wananchi ili uweze kufanikiwa bila vikwazo.

“Kuna wakati tulihisi kuwa serikali imetusahau watu wa vijijini lakini sasa tunafarijika kuona hawa REA na TANESCO wanakuja kutuunganishia umeme na tayari wameanza kuchimba mashimo kwenye kijiji chetu shughuli iliyobaki ni kufukia nguzo ,uhakiki ulishafanyika hapo awali” Alisema Parirong’o Sipitieki ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Ingoikumeni.

News Updates: Kinachojiri Mkutano wa Saed Kubenea na Waandishi wa Habari Jijini Dar

$
0
0

Ndugu waandishi wa habari,
Natumaini mna taarifa kwamba tangu Ijumaa iliyopita, nimefungua shauri Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam, kupinga kinachofanywa na Bunge Maalum la Katiba. Shauri hilo, limesajili kwa Na.28 la mwaka 2014.

Katika kesi hiyo, nimeomba Mahakama Kuu itoe tafsiri sahihi juu ya mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba, chini ya kifungu cha 25 (1) na (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ya mwaka 2011.

Aidha, nimewasilisha maombi madogo nikiomba Mahakama kutoa zuio la muda la kusimamisha Bunge Maalum la Katiba, wakati tukisubiri uamuzi wa kesi ya msingi. Maombi ya zuio yamepangwa kutajwa tarehe 4 Septemba na kesi ya msingi itatajwa 15 Septemba 2014.

Ndugu waandishi wa habari,
Tangu kuripotiwa kufunguliwa kwa shauri hili mahakamani, yapo mengi yaliyosemwa. Wapo walionipongeza na kunifariji. Wapo walionitia moyo na kuniomba nisirudi nyuma. Wapo walionidhihaki na kunikatisha tamaa. Wapo walionitisha.

Lakini wapo walioahidi kuniombea kwa Mwenyezi Mungu ili jambo hili kubwa nililolifanya kwa maslahi ya taifa langu, niweze kulifikisha mwisho nikiwa mzima na mwenye amani.

Ninafahamu jukumu hili nililolibeba ni zito sana. Linaweza likasababisha baadhi ya watu kukosa posho ikiwa mahakama itaridhia ombi langu la usitishaji wa Bunge la Katiba. Linaweza kunitenganisha na baadhi ya ndugu na marafiki zangu. Linaweza kuhatarisha hata maisha yangu.
Lakini kwa kuwa maisha yangu hayajawahi kuwa salama kwa zaidi ya miaka tisa sasa; nimesema Mungu ndiye atakayenilinda.

Ninajua kuwa kesi hii, inaweza kusababisha gazeti langu la ----------- ambalo limefungiwa kwa muda usiojulikana na watawala kwa kuitumia sheria katili ya magazeti, linaweza lisifunguliwe kabisa. Hii ni kwa sababu, waliofungia ----------- ndiyo haohao niliowashitaki.
Hata hivyo, nimesema niko tayari kwa lolote. Nitakabaliana nalo kwa kadri Mwenyezi Mungu atakavyoniongoza.

Ndugu waandishi wa habari,
Nimefungua shauri hili kwa kusukumwa na uzalendo wangu na kulinda heshima ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano waliotoa maoni yao mbele ya Tume ya Rais ya Mabadiliko ya Katiba, nami nikiwamo.

Nimefungua shauri hili baada ya kujiridhisha kuwa wananchi waliowengi, kutoka makundi mbalimbali – serikalini hadi chama tawala – wanakiri kuwapo tatizo katika tafsiri ya sheria kuhusu mamlaka ya Bunge Maalum la Katiba.

Baadhi ya walioko bungeni wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samwel Sitta, wanasema wanaweza kufanya lolote katika rasimu. Wanaweza kufuta rasimu; kubandua sura yote na wanaweza kubandika sura mpya.

Siyo hivyo tu: Wanaweza hata kukusanya maoni upya kutoka makundi mbalimbali. Kazi hii, ndiyo inayofanyika sasa bungeni.
Lakini wapo wanaoamini kuwa Bunge Maalum la Katiba, halina mamlaka ya kufanya kazi ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Halina uwezo kukusanya maoni upya.

Bunge Maalum la Katiba, haliwezi kunyofoa moyo wa rasimu ya katiba kama ilivyowasilishwa na mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, waziri mkuu mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba na kuleta kitu kipya ambacho hakikutokana na wananchi; na ambacho kimekusanywa kinyume cha sheria.

Nimekwenda mahakamani baada ya kumuona Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema akishindwa kwenda mahakamani kuomba tafsiri ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Badala yake, Jaji Werema amempotosha rais kuwa hana mamlaka ya kusimamisha mchakato wa Katiba.

Sheria inayosimamia mchakato wa katiba mpya ni sheria tofauti na sheria nyingine katika nchi. Sheria nyingine zote zinasimamiwa na vyombo vya serikali. Hii inasimamiwa moja kwa moja na wananchi.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano inayotumika sasa, haina kifungu chochote kinachoruhusu kutungwa katiba mpya. Wabunge wote wa Bunge la Muungano ambao sasa wamefanywa wajumbe wa Bunge la Katiba, akiwamo Werema, waliapa kulinda katiba iliyopo na kuitetea. Rais wa Jamhuri ya Muungano ameapa kulinda katiba iliyopo.

Lakini kwa kuwa Bunge la Jamhuri liliridhia kutunga katiba mpya kwa kutumwa na wananchi – siyo kwa kutumwa na katiba iliyopo – rais anayo mamlaka mapana ya kusimamisha mchakato huu.

Rais anaposimamia mchakato huu, hafanyi hivyo kama rais binafsi. Anatekeleza matakwa ya wananchi ambao wote kwa umoja wao, wamempa yeye mamlaka yao kusimamia raslimali, ulinzi na usalama wa mali za raia wa Jamhuri ya Muungano.

Kwahiyo, ni ujuha kuacha mabilioni ya shilingi ya wananchi kuteketea, kisha watawala wakadai kuwa “rais hana mamlaka ya kusimamisha mchakato wa katiba mpya.”

Kutokana na mgongano huo, kama mwananchi wa Jamhuri ya Muungano nimewasilisha malalamiko yangu mahakamani kwa nguvu ya Ibara ya 26 (2) ya Katiba inayosema: “Kila mtu ana haki, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria, kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya katiba na Sheria za nchi.”

Suala zima la maoni ya wananchi haliwezi kuachwa mikononi mwa watu wachache. Mamlaka ya kutafsiri sheria za nchi, hawezi kuachwa mikononi mwa Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum la Katiba wala chombo kingine kilichojinyakulia mamlaka hayo kinyemela.
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri, Ibara ya 107 A (1), “mamlaka yenye kauli ya mwisho ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa ni mahakama.”

Kwa msingi huo, iwapo tafsri yangu ni sahihi, kinachofanywa na Bunge la Katiba sasa, ni uvunjaji wa Sheria Na. 83 ya mwaka 2011, inayounda Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kuanisha majukumu yake na Bunge la Katiba.

Kama tafsiri yangu ni sahihi, kinachofanywa na Bunge Maalum la Katiba, ni kuvunja Katiba. Hakikubaliki.
Hivyo basi, kupitia kwenu, nichukue nafasi hii, kuwaomba wananchi wote wanaolitakia mema taifa letu, kusimama pamoja nami katika kusaidia taifa kupata katiba inayoheshimu maoni ya wananchi.

Ninawashukuru wote waliofariji; wanaonitia moyo na walioahidi kuniombea katika hili. Ninawaomba waniunge mkono kwa hali na mali. Nchi hii ni yetu sote.

Saed Kubenea,
Mkuregenzi Mtendaji,
HHP Limited.

MWANAHABARI MACHACHARI SALUM MWALIMU KUWANIA UJUMBE WA KAMATI KUU CHADEMA

$
0
0

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la CHADEMA Zanzibar Bi
Maryam Ahmed Omar akimkabidhi fomu Salum Mwalim fomu ya kugombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya
Chama hicho kundi la Zanzibar katika hafla fupi iliyofanyika ofisi Kuu za Chadema kisiwani humo.

Mmoja wa wachama wa CHADEMA Zanzibar
Bikwao Khamis akitia saini ya fomu ya udhamini wa Salum Mwalim (aliyesimama wa kwanzakushoto) anaegombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho kundi la Zanzibar.Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyo Jumamosi Agosti 30, 2014 katika Ofisi za ChademaZanzibar. (Picha zote na Martin Kabemba)

Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar
Jumbe Idrisa akitia saini ya fomu ya udhamini wa Salum Mwalim (aliyesimama wa kwanza
kushoto) anaegombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho kundi la Zanzibar.
Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyoJumamosiAgosti 30, 2014 katika Ofisi za Chadema
Zanzibar.

Mbunge wa CAHDEMA viti Maalum wa CHADEMA
Mwanamrisho Abama akimdhamini Mgombe Ujumbe wa Kamati Kuu wa Chama
hicho Salum Mwalim katika ofisi za chama Zanzaibar.
Mwalim alichukua na kurudisha fomu hiyo Jumamosi Agosti 30, 2014 katika Ofisiza Chadema
Zanzibar.

Salum Mwalim anaewania nafasi ya ujumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA
kundi la Zanzibar akitia saini kitabu cha
wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi Kuu za chama hicho Zanzibar kwa lengo la
kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo.

……………………………………………..

Na Martin Kabemba, Zanzibar

Mmoja wa wanahabari na mtangazaji
mahiri wa wakati huu Salum Mwalim ameomba kuchaguliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu
wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia nafasi za Zanzibar,Uamuzi huo wa Mwalim ambae kwa sasa ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni ya
Vodacom tayari umeibua mjadala Zanzibar na kwamba unatarajiwa kubadili upepo wa
uchaguzi wa Chadema Visiwani humo kutokana na ushawishi na mvuto alionao
utakaomfanya kukubalika na kuaminika huku akifanya joto la uchaguzi kupanda.

Kwa sasa joto la uchaguzi ndani ya
Chadema linaonekana kuwa juu zaidi Tanzania Bara.

Akichukua fomu ya kuomba kugombea kuingia kwenye chombo hicho kikuu cha maamuzi
ndani ya Chadema, Mwalim amesema baada ya kushawishiwa na watu wa rika na wa
aina mbalimbali kushauriana na makundi mbalimbali amejipima na kuona kuwa
anatosha katika nafasi hiyo.

Mwalim amesema wakati wote wa maisha yake amekuwa akitembea na uzanzibari wake
na kwamba alitambua kuwa siku moja atakuja kuwatumikia wazanzibar na hivyo
kutoa mchango wake katika maendeleo ya visiwa hivyo ambako ndiko asili yake
ilipo.Mwalim amechukulia fomu hiyo mapema leo (Jumamosi Agosti 30) katika ofisi kuu
za Chadema Zanzibar na kuirudisha majira ya mchana ikiwa leo ndio siku ya
mwisho ya uchukuaji wa fomu na urejeshaji kuwania nafasi mbalimbali za uongozi
ndani ya chama hicho,

“Nimechukua fomu na sasa nairudisha, kwa kuwa wakati wa kampeni bado
sitoweza kuzungumza wala kujinadi naomba niheshimu taratibu na miongozo ya
uchaguzi ya chama lakini nataka kuwaambia kuwa Zanzibar na U-zanzibari wangu ni
jambo ninalojivunia kuliko kitu kingine chochote maishani mwangu.”Alisema
Mwalim

“Ni uamuzi mgumu sana kuwahi
kufanya katika maisha yangu lakini nimeufanya kwa kuzingatia masilahi mapana ya
chama ninachokiamini na kwa nchi yangu ya Zanzibar na watanzania kwa
ujumla,ninamuomba Mwenyezi Mungu anisimamie anipe nguvu,afya,hekima,busara,
unyenyekevu na uadilifu katika safari hii ya siasa ninayoianza.” Aliongeza
MwalimAkiongea kwa kujiamini na kwa umakini mkubwa, amesema ana imani kubwa kuwa
ataungwa mkono na kushinda nafasi hiyo kwa kuwa pande zote mbili za Visiwani na
Bara wanamfahamu vizuri sana na wanatambua mchango wake kwa Chadema na kwa nchi
kwa ujumla.

Mwalim ambae ni msomi wa masuala ya uandishi wa habari na
mwenye shahada ya uzamii katika usimamizi wa Biashara ni mmoja wa vijana
waliotokea kujizolea umashuhuri mkubwa nchini kutoka na uwezo wake na uchapaji
kazi wake akiwa mtu mwenye misimamo na kukubalika hasa na vijana nchini.Kamati kuu ya Chadema ndicho chombo kikuu cha maamuzi ndani ya Chama hicho, na
iwapo Mwalim atafanikiwa kushinda na kuingia kwenye chombo hicho anatabiriwa
kuwa atabadili upepo wa Chadema katika siasa za Zanzibar kutokana na
Mwanahabari huyo kukubalika katika jamii na upya wake katika siasa unamfanya
kuingia katika siasa pasi na kuwa na makundi hali itakayomwezesha kupewa ushirikiano
na kila mtu ndani na nje ya Zanzibar.

Akimkabidhi fomu hiyo Makamu
Mwenyekiti wa Zanzibar wa Baraza la Wazee La Chadema Bi Maryam Ahmed Omar
amempongeza Mwalim kwa uamuzi wake huo na kumtakia kila la kheri katika
uchaguzi huo.

Bi Omar amesema Chadema ya sasa
imeimarika kwa kiwango cha juu na kwamba uamuzi wa Mwalim ambae ni kijana
mzaliwa wa visiwani humo wa kuamua kugombea nafasi hiyo utasaidia kuongeza
nguvu ya kukiimarisha chama.

Tukio la uchukuaji wa Fomu wa Mwalim
limehudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Mjini Magharibi Idrisa
Jumbe, mbunge wa wa viti maalum wa chama hicho Mwanamrisho Abama miongoni mwa
viongozi na makada mbalimbali wa chama hicho

Watuhumiwa wa mabomu Arusha wapandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka ya mauaji

$
0
0
 

Watuhumiwa wapatao 19 wanaotuhumiwa kwa milipuko ya mabomu mkoani Arusha leo wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Arusha na kusiomewa mashtaka mbalimbali yanayo wakabili yakiwemo ya mauaji.Watuhumiwa hao ambao wameunganishwa na wenzao zaidi ya 20 waliokwishafikishwa kwenye mahakama hiyo kwa tuhuma hizo wamefikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa polisi ambao haujawahi kuonekana katika siku za hivi karibuni.

Gari ya polisi iliyowabeba watuhumiwa hao


Tofauti na ilivyokuwa hapo awali ulinzi katika mahakama hiyo uliiimarishwa kwa kiasi kikubwa kuanzia mapema alifajiri ambapo watu wote waliokuwa wanaingia kwenye lango la mahakama hiyo walikaguliwa na vifaa maalumu utaratibu ambao ulifuatwa na watu wote bila kujali nyadhifa zao wakiwemo watendaji wa mahakama hiyo.


Baada ya kufikishwa mahakamani hapo mbele ya hakimu Devota Msofe aliyekuwa anasaidiwa na waendeshamashtaka Agustino Kombe, Felexs Kwetukia na Maselina Mwamunyange washtakiwa walisomewa mashtaka yanayowakabili kwa makundi, jinsi wanavyodaiwa kuhusika na madhara yaliyosababishwa na makosa hayo.



Miongoni mwa mashataka waliyosomewa ambayo kila mmoja alihusishwa kwa namna moja ama nyingine huku baadhi yao wakijikuta wakitajwa karibu kwenye makosa yote ni pamoja na shtaka la mauaji, kujihusisha na vitendo vya kigaidi, kukusanya silaha yakiwemo mabomu, kuyasarisha na kisha kuyatumia kuua na pia kufadhili vitendo hivyo kwa kutoa fedha na ushirikiano wa kuvitelekeza.


Mashtaka mengine ni pamoja na kushawishi na kuhamasisha vijana kujiunga na vikundi vya ugaidi, kuhifadhi dhana na silaha za kwa lengo la kufanya ugaidi na kuzitumia kutekeleza vitendo hivyo.


Kesi ya watuhumiwa hao ambao wote wanahusishwa na matukio yote ya milipuko ya mabomu na kuwamwagia viongozi wa dini tindikali vilivyowahi kutokea mkoani Arusha itatajwa tena tarehe 15.08/2014 na washtakiwa wote wamerudishwa rumande ambapo kwa mujibu wa sheria kesi yao haina dhamana.

 

STORI NA PICHA: MATUKIO NA VIJANA .COM

UCHAGUZI CHADEMA BARAZA LA WAZEE @MLIMANI CITY DAR ES SALAAM LEO

$
0
0

Moja kati ya wajumbe wa mkutano huo profesa SAFARI na mh MABERE MARANDO wakiwa hapa katika uchaguzi wa baraza la wazee,uchaguzi huo unafanyiaka jijini Dar es salaam ukumbi wa mlimani city

Chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA leo kimeingia katika siku yake ya kwanza ya chaguizi ndani ya chama hicho ambapo leo watafanya chaguzi ndani ya baraza la wazee la chama hicho uchaguzi unaofanyika jijini Dar es salaam.


Akizungumza na mtandao huu mwenyekiti wa baraza la wazee wa chama hicho nje ya ukumbi wa mkutano MZEE NYANGAKI SHILUNGUSHELA  amesema kuwa muitikio wa wajumbe ndani ya uchaguzi huo ni mzuri ambapo  wajumbe zaidi ya 90 wanatarajiwa kucshiriki katika uchaguzi huo.


  Mtandao huu utakuletea yote yatakatokuwa yanajiri ndani ya chaguzi hizi za ndani za chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA

Picha zikionyesha wajumbe mbalimbali wakiwa katika mkutano huo ambao umeanza leo jijini Dar es salaam


Mwnyekiti wa baraza la wazee la chama cha democrasia na maendeleo CHADEMA MZEE NYANGAKI SHILUNGUSHELA akizungumza na wanahabari muda huu nje ya ukumbi wa mkutano huo wa uchaguzi.UNAWEZA KUPATA HOTUBA YAKE YOTE YA UFUNGUZI WA UCHAGUZI HUO HAPO CHINI


HOTUBA YA MWENYEKITI WA TAIFA WA BARAZA LA WAZEE WA CHADEMA MZEE NYANGAKI SHILUNGUSHELA KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA BARAZA LA WAZEE WA CHADEMA TAREHE 6 SEPTEMBA 2014 KATIKA UKUMBI WA MLIMANI CITY DAR ES SALAAM


Waheshimiwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Wazee wa CHADEMA Taifa,

Waheshimiwa Waasisi wa CHADEMA mliohudhuria mkutano wa leo,

Waheshimiwa Wasimamizi wa Uchaguzi wa Baraza la Wazee wa CHADEMA Taifa,

Waheshimiwa Wawakilishi wa Chama Taifa na Makao Makuu,

Waheshimiwa Wageni  waalikwa; mabibi na mabwana:


Waheshimiwa Wazee;

Niungane nanyi kumshukuru Mwenyezi Mungu  kwa kutukutanisha siku ya leo katika Mkutano Mkuu wa Baraza la Wazee wa CHADEMA Taifa. Niwasalimu kwa kauli mbiu ya Baraza letu: Wazee, Hazina ya Hekima na Busara.

Tumekutana katika Mkutano Mkuu huu tukiongozwa na dhumuni kuu la Baraza la Wazee wa CHADEMA kwa mujibu wa kipengele cha 1.1 cha  kuwa chombo kikuu cha ushauri wa busara na hekima kinachowezesha CHADEMA kufikia na kuendeleza madhumuni ya CHADEMA kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Mkutano huu mara baada ya ufunguzi utajadili ajenda kuu nne: Mosi, Taarifa ya Utendaji wa Baraza la Wazee wa CHADEMA, Pili, Marekebisho ya Mwongozo wa Baraza la Wazee wa CHADEMA, Tatu, Mpango Kazi wa Baraza la Wazee wa CHADEMA kwa mwaka 2014-2016 na Nne, Uchaguzi wa Viongozi wa Taifa wa Baraza la Wazee wa CHADEMA.

Wajibu wangu katika hatua ya sasa ni kufungua mkutano huu rasmi na nimeona nichukue fursa hii kuzungumza machache kabla ya Taarifa ya Sekretariati ya Wazee ambayo itatoa maelezo juu ya Utendaji wa Baraza la Wazee katika kipindi cha kati ya mwaka 2009 mpaka 2014 na ajenda nyingine ambazo zitatoa mwelekeo wa 2014 mpaka 2016.

Kabla ya kuendelea na hatua hiyo, niwaomba tusimame kwa dakika moja ya ukimya kuwakumbuka Wazee wenzetu viongozi na wanachama wa Baraza la Wazee waliotangulia mbele ya haki katika kipindi cha tangu tulipokutana katika Mkutano Mkuu wa Wazee.

Wazee hao ni pamoja na Hayati Mzee Mohamed Bob Makani aliyekuwa muasisi, Katibu Mkuu wa kwanza na Mwenyekiti wa Pili wa CHADEMA, marehemu Wazee Balozi Pastor Ngaiza, Philip Shilembi na Shida Salum waliokuwa wajumbe wa Kamati Kuu ya chama, viongozi na wanachama wengine; Mwenyezi Mungu awalaze mahali pema.

Waheshimiwa Wazee;

Niwapongeze kwa kuchaguliwa kuwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Wazee kwa mujibu Taratibu za Kuongoza Baraza la Wazee wa CHADEMA kipengele 4.7.4.

Nitumie nafasi hii pia kuwaomba mfikishe salamu zangu za pongezi kwa viongozi wote wa Baraza la Wazee wa CHADEMA walioshinda katika ngazi mbalimbali kuanzia misingi, matawi, kata/wadi, wilaya na Mikoa. 

Hakika ushindani katika chaguzi hizo na kiwango cha wagombea waliojitokeza kwenye uchaguzi wa ngazi ya taifa ni ushahidi wa ukuaji wa CHADEMA na namna ambavyo wazee wanazidi kujiunga na CHADEMA na kuwa mstari wa mbele kuwezesha mabadiliko nchini.

Hali hii inapaswa kuendelezwa na viongozi wa kitaifa watakaochaguliwa katika Mkutano Mkuu huu. Hali hii ni matokeo pia ya msukumo ulioongezwa na muundo wa Kanda na Programu ya CHADEMA ni Msingi.

Hivyo, ni muhimu katika maeneo ambayo hayajakamilisha uchaguzi ngazi ya chini, mara baada ya Mkutano huu; nyinyi, viongozi wa kitaifa watakaochaguliwa na kwa kushirikiana na viongozi wa ngazi mbalimbali kwenda kukamilisha chaguzi katika maeneo machache yaliyobaki hususan katika vitongoji, vijiji na mitaa kupitia mwendelezo wa Programu ya CHADEMA ni msingi.

Kwa mafanikio haya ya ujenzi wa CHADEMA, napendekeza kwamba Mkutano Mkuu huu wa Wazee upitishe azimio la kutaka Serikali kutangaza haraka uchaguzi wa Vitongoji, vijiji na Mitaa wa mwaka 2014 kwa kuwa kuchelewa kutangazwa kwa uchaguzi huo mpaka hivi sasa sababu mojawapo ni hofu ya CCM kushindwa katika maeneo mengi nchini.

Aidha, mafanikio haya ni dalili njema ya CHADEMA kwa kushirikiana na  vyama vingine vya upinzani hususan vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) vya kuiondoa CCM madarakani kupitia chaguzi za udiwani, ubunge na urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Katika muktadha huo, katika kujadili Mpango Kazi wa Baraza la Wazee kwa mwaka 2014 mpaka 2016, wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Wazee mtoe mapendekezo yatakayowezesha kukamilisha chaguzi za wazee katika maeneo machache yaliyobaki kwenye ngazi za misingi, matawi, kata/wadi, wilaya na mikoa ili kuwezesha ushindi katika maeneo yote muhimu.

Pamoja na kazi hii, anzeni kujiandaa kuhamasisha wazee kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura. Napendekeza pia  Mkutano Mkuu huu upitishe azimio la kuitaka Tume ya Uchaguzi (NEC) kutangaza mara moja ratiba ya uandikishaji wa wapiga kura kwa kuwa iliahidi kwamba zoezi hilo lingeanza maeneo mbalimbali nchini kuanzia mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka 2014.

Kampeni za uchaguzi zitakapoanza Mpango Kazi wa Wazee uwezeshwe uwepo wa wazee kwenye kamati za kampeni katika vituo vya kupigia kura kuwezesha ushindi wa CHADEMA na washirika wake katika chaguzi zote zinazofuata.

Waheshimiwa Wazee;

Muongozo wa baraza la Wazee wa CHADEMA kipengele 1.2 (f) unatoa jukumu kwa baraza letu kubuni mipango na mikakati ya kuhusisha kundi la wazee ndani ya jamii kukagua, kusimika na kuchagua viongozi bora kwenye chaguzi za ndani na nje ya chama.

Nimeweka kipaumbele suala la uchaguzi kwa kuwa tupo katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa ndani ya CHADEMA unaofanyika ikiwa ni takribani mwezi mmoja kutoka kuanza kwa kampeni za  uchaguzi wa Vitongoji, Vijiji na Mitaa wa mwaka 2014 na mwaka mmoja kutoka katika kampeni za uchaguzi mkuu wa udiwani, ubunge na urais wa mwaka 2015. Nimeweka kipaumbele suala la uchaguzi kwa kuwa nchi yetu ipo kwenye mkwamo wa mchakato wa mabadiliko ya katiba.

Wakati sisi tunapokutana hapa, Bunge Maalum linaendelea kupokea taarifa za Kamati mbalimbali huku wanaojiita walio wengi katika Bunge hilo wa CCM na vibaraka wao wakiendelea kupuuza maoni ya wananchi na kubomoa misingi ya rasimu iliyowasilishwa na tume ya mabadiliko ya katiba.

Natambua kwamba rasimu ya katiba itayopendekezwa hatimaye itakuja kupigiwa kura ya maoni ambao hao wanaojiita walio wengi wa CCM katika Bunge Maalum watakutana na wananchi walio wengi waliotoa maoni yao.

Hata hivyo, Baraza la Wazee wa CHADEMA ni muhimu kupitia mkutano mkuu huu lipitishe azimio la kulaani hatua ya Wazee wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalum Samuel Sitta na Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete kushindwa kutoa uongozi wa kunusuru fedha za umma kuendelea kutumika huku kukiwa hakuna muafaka wa kitaifa kwenye mchakato.

Kwa upande mwingine, nashauri Mkutano Mkuu wa Baraza la Wazee wa CHADEMA upitishe azimio la kuwapongeza Wazee wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti Jaji (Mstaafu) Joseph Warioba na wajumbe wake akiwemo mzee mwenzetu mteule kupitia CHADEMA Prof. Mwesiga Baregu kwa kuheshimu maoni ya wananchi na kuzingatia sehemu kubwa ya maoni hayo katika rasimu ya pili ya katiba iliyowasilishwa.

Waheshimiwa Wazee;

Muongozo wa Baraza la Wazee kipengele cha 1.2 (a) kimetoa jukumu kwa Baraza la Wazee wa CHADEMA kuwa chombo cha ushauri ngazi mbalimbali za chama. Wajibu huu ni wa baraza na wazee wanachama wa baraza letu. Kwa kuzingatia wajibu huo, nimeshiriki kwa niaba yetu katika vikao vya kamati kuu kwa nyakati mbalimbali na katika vikao vya kupanga mikakati ya chama kwa miaka kadhaa.

Kati ya masuala ambayo vikao hivyo vimekuwa vikiyapa kipaumbele ni mchakato wa mabadiliko ya katiba.

Wazee ni hazina ya hekima na busara. Hivyo, ushauri wangu mara nyingi umekuwa ni kwa CHADEMA kuwezesha maridhiano, usuluhishi na utatuzi wa migogoro inayojitokeza kwenye mchakato wa mabadiliko ya katiba.

Hata hivyo, katika hali ambayo imefikia ya mgogoro baina ya CCM kwa upande mmoja na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na wananchi walio wengi waliotoa maoni yao kwa upande mwingine; na kuvunjika kwa mazungumzo yaliyoongozwa msajili wa vyama vya siasa nashauri viongozi wa CHADEMA na UKAWA nashauri wachukue tahadhari kubwa katika mazungumzo na Rais.

Waheshimiwa Wazee;

Kitendo cha Bunge Maalum kuendelea mpaka hivi sasa hata baada ya kuanza mazungumzo ya Rais na vyama yanayoratibiwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) inaweza kuwa ni mchezo wa CCM na Serikali kuchelewesha maridhiano huku wajumbe wake wakiendelea ‘kuchakachua’ rasimu ya katiba  kinyume na maoni ya wananchi.

Hivyo, tarehe 8 Septemba 2014 iliyotangazwa na Ikulu kuwa ni mwendelezo wa mazungumzo na Rais inapaswa kuwa nafasi ya mwisho iwapo Bunge Maalum halitasitishwa au kuahirishwa ni muhimu viongozi wa taifa wa CHADEMA wakashauriana  wenzao wengine wa UKAWA kufanya maamuzi ya kuwaunganisha wananchi kwa nguvu ya umma kuchukua hatua kwa CCM na Serikali.

Mwelekeo unaonyesha kwamba wazee wa CCM ndani ya chama hicho, Bunge Maalum, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Serikali za pande zote mbili za Muungano wameamua kusaliti maoni ya wananchi na matakwa ya kikatiba kwamba mamlaka na madaraka ni ya wananchi.

Katika muktadha huo, ufumbuzi endelevu ni kuiondoa CCM madarakani na kuweka uongozi bora na chama kitakachokuwa  na dhima ya kuleta sera sahihi, mikakati makini  na oganaizesheni makini katika mchakato wa mabadiliko ya katiba na maendeleo ya nchi.  

Mabadiliko ya Katiba sio  mchakato wa kuchukuliwa kwa mzaha. Ni mchakato unaohusu maisha ya wananchi na mustakabali wa nchi. Pamoja na CCM kukataa maoni ya msingi ya wananchi juu ya muundo wa muungano wa Shirikisho la Serikali tatu, chama hicho kupitia wajumbe wake wanaojiita walio wengi kinapinga maoni ya wananchi yaliyoingizwa kwenye rasimu ya katiba ikiwemo uadilifu, uwazi na uwajibikaji kuwa sehemu ya tunu za taifa.

Kwa kuzingatia maoni hayo, CCM na wajumbe wake wanaojiita walio wengi hawana uadilifu, uwazi na uwajibikaji wa kuweza kusimamia masuala ya msingi yanayohusu wazee katika rasimu ya katiba ikiwemo ya kuhakikisha kwamba hifadhi ya jamii hususan pensheni inatolewa kwa wote (universal social security particularly pension).

Waheshimiwa Wazee;

Masuala na maslahi ya wazee chini ya chama kinachotawala sasa yamekuwa yakipewa kipaumbele kwenye ahadi badala ya kuwekwa katika utekelezaji. Matokeo yake ni migogoro ya wazee kama ambavyo inajitokeza kwa nyakati mbalimbali kwa wazee wanaodai mafao yao.

Taarifa ya utendaji ya sekretariati itaeleza namna ambavyo Baraza la Wazee wa CHADEMA limekaa na wazee wenye madai mbalimbali ikiwemo wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Katika maboresho ya Mpango Kazi 2014 mpaka 2016 natarajia wazee wajumbe wa mkutano huu mtatoa mapendekezo ya namna ya kuwezesha Baraza letu kuongeza msukumo katika kuwawakilisha na kuwatetea wazee nchini.

Kilio cha wazee wengi kimekuwa ni umaskini na hali ngumu ya maisha kutokana na wenye kupata pensheni kupata kiwango kidogo kwa waliokuwa waajiriwa katika sekta rasmi na wengi zaidi kutokuwa kabisa na pensheni baada ya kustaafu kwao hasa wakulima na wazee waliotumikia taifa katika sekta isiyo rasmi.

Kwa nyakati mbalimbali katika siku ya Wazee Duniani Oktoba Mosi kati ya mwaka 2009, 2010, 2011, 2012 na 2013 Serikali imekuwa ikiahidi kutoa pensheni kwa wazee wote nchini; hata hivyo hakuna mwaka mpaka sasa ambao bajeti imetengwa kuwezesha utekelezaji. Wanachama wa Baraza la Wazee wa CHADEMA wamekuwa wakifuatilia suala hili ikiwemo kupitia Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Ahadi za uongo zimekuwa zikitolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda na mawaziri wengine kuhusu suala hili. Nitoe mwito kwa viongozi wa wazee kutoka mikoa mbalimbali mlioshiriki mkutano huu kuanza maandalizi mara baada ya kurejea katika maeneo yenu ili kuziunganisha ngazi zenu na za chini yenu katika maadhimisho ya siku ya wazee kwa mwaka huu Oktoba Mosi, 2014 ujumbe ufike kwa watawala kwamba wazee wamechoka kudanganywa na wako tayari kuunga mkono mabadiliko kuchangua uongozi ambao utatekeleza ahadi kwa vitendo.

Wazee wanaweza kuendelea na mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi wakiwa na mazingira bora.  Hivyo, katika Mkutano huu Taarifa ya Sekretariati ya Baraza la Wazee itawajulisha hatua iliyofikiwa katika mchakato wa kuboresha Sera ya Wazee ya CHADEMA. Nawahimiza kushiriki katika kushiriki michakato yote ya sera mbalimbali zenye kuwagusa wazee kwa namna au nyingine zitakazotekelezwa na CHADEMA kitakapoongoza Serikali.

Waheshimiwa Wazee;

Nimalizie kwa kuwakumbusha majukumu ya msingi ya Baraza la Wazee wa CHADEMA kwa mujibu wa muongozo kipengele 1.2 (b), (c) na (j) ya kuwa chombo cha utatuzi na usuluhishi wa migogoro ndani ya chama ama baina ya viongozi, kuwa chombo cha kupatanisha na kuunganisha viongozi na kushauri viongozi wa CHADEMA katika ngazi mbalimbali.

Katika mkutano huu mtapokea mapendekezo ya maboresho na marekebisho ya muongozo wa Baraza la Wazee wa CHADEMA katika maeneo na masuala mbalimbali. Pendekezo langu jipya ni kuhusu jina la Baraza letu; kumekuwa na changamoto ya kutafuta kifupi cha Baraza hili kuweza kutofautiana na Baraza la Wanawake wa  CHADEMA (BAWACHA). Kumekuwepo pia na ombwe la kutokuwa na Baraza la Wazee katika taifa letu.

Hivyo, pendekezo langu ni kuwa tujitambulishe kama Baraza la Wazee tu. Baraza la Wazee (BAWA) litabeba sura ya utaifa litaendelea kuwa la kitaifa. Jumuiya ya Wazazi ya CCM imeendelea kujitambulisha kama JUWATA ikighilibu wazazi nchini. Umoja wa Wanawake wa CCM, umeendelea kujitambulisha kama UWT ukihadaa wanawake kuwa ni chombo cha wote. Baraza la Wazee (BAWA) sio tu libebe taswira ya wazee nchini, bali lionyeshe kwa vitendo kuwakilisha na kutetea wazee nchini mpaka pale wazee watakapokuwa na chombo chao cha kuwaunganisha wote bila kujadili tofauti mbalimbali.

Katika kujadili mapendekezo hayo, na katika kutekeleza muongozo huo kumbukeni kuwa pamoja na kuwa wanachama na vikao vya kawaida vya ngazi mbalimbali. Mkazo uwekwe katika kuunda “Caucus ya Wazee” katika ngazi zote. Hili ni kundi maalum la kushauri viongozi wa kuanzia ngazi za msingi hadi taifa. Hili ni kundi la wazee wateule wenye busara na hekima lukuki, wanaokubalika na kuheshimika katika jamii  na wenye kupatikana mara kwa mara kutoa ushauri. Kwa kufanya hayo mtakuwa mnatekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya Baraza la Wazee wa CHADEMA: Wazee; Hazina ya Hekima na Busara. Na kwa kauli mbiu hiyo, natangaza kwamba Mkutano Mkuu huu umefunguliwa rasmi.

Mungu ibariki Tanzania,

Mungu ibariki CHADEMA,

Mungu wabariki Wazee.


TASWIRA: MSAFARA WA MAALIM SEIF WAPATA AJALI JIJINI MWANZA

$
0
0

Gari aliyokuwa amepanda MAALIM SEIF ikiwa imeharibika vibaya Na Karoli Vinsent

Habari zilizotufikia mda huu Zinasema MSAFARA wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad umepata Ajali mbaya  Mkoani Mwanza na kupelekea Viongozi mbalimbali wa Chama hicho kuwa na hali mbaya.

Vilevile Mkurugenzi huyo wa Habari wa Chama hicho alisema kwa sasa Majeruhi hawo wamekimbizwa kwenye Hospitali ya Bugando kupatiwa matibabu na hali yao inaendelea vizuri isipokuwa Katibu chama cha Cuf kutoka Wilaya ya Nyamagana Rehema Mwenda hali yake sio Nzuri kutokana na kupoteza Fahamu,

Moja ya gari ambalo lilikuwa kwenye msafara wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu Mkuu wa Cuf, Maalim Seif Sharif Hamadi baada ya kupata ajali, Misungiwi, Mwanza leo.

Hili ni gari lingine ambalo lenye usajili namba T397ANU nalo lilihusika katika ajali hiyo leo.

Keria ya moja ya magari yaliyopata ajali ikiwa chini baada ya kufyatuka baada ya ajali.

Baadhi ya wananchi wakishuhudia msafara wa Maalim Seif, mara baada ya ajali.

Msafara wa Maalim Seif ukijiandaa kuondoka mara baada ya magari mawili kati ya saba yaliyokuwa kwenye msafara kupata ajali.

Mkurugenzi wa habari wilaya'na MH SHIDO Ambae ni mwenyekiti wa serikal ya mtaa uliyopo kata ya miringo,wameumia vibaya wamelazwa hospitali ya BUGANDO

   Akithitisha kutokea kwa Ajali hiyo wakati anaongea na Mwandishi wa Mtandao huu, mda huu kwa njia ya simu kutoka Mkoani Mwanza kwenye Ajali hiyo, Naibu Mkurugenzi wa Habari kutoka Chama cha Wananchi CUF bwana Kambaya alithibitisha kutokea kwa Ajali hiyo na kusema Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Maalim na Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) Seif Sharif Hamad  ajadhurika na yuko salama bali waliodhurika na Ajali hiyo ni viongozi wa chama hicho,

Rehema Mwendaalikuwa kwenye msafara huo aiugulia maumivu

“Ni kweli Msafara wa Makamu wa rais na Katibu mkuu Taifa umepata ajali ila yeye yuko salama,lakini viongozi wetu wa chama akiwemo katibu wa Chama cha Wananchi CUF  Wilaya ya Nyamagana Be Rehema Mwenda Pamoja na Mkuu wa Kitengo cha cha Habari wa chama Chetu wilaya ya nyamagana Hassan Shido  ndio wamepata majeraha kutokana na Ajali hiyo,”alisema Kambaya.


Kambaya alizidi kusema Ajali imetokana na Dereva wa Gari aina Scania kwenda kuligonga  Gari lilokuwa limewabeka viongozi hao,ambapo gari hilo  lilikuwa la nne kutoka gari  lililombeba Maalim Seif  kwenye msafara huo.

 

PICHA NA GLOBAL PUBLISHERS NA MATUKIODAIMA.COM

RAIS KIKWETE ATUNUKU NISHANI ZA MIAKA 50 YA JWTZ

$
0
0

Rais Jakaya Kikwete akimtunuku nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Jeshi la Wanachi wa Tanzania JWTZ, Mkuu wa majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange katika sherehe za kutunuku nishani zilizofanyika kwenye ukumbi wa Jenerali Kiwelu wa Chuo cha Mafunzo ya Maafisa wa Jeshi Tanzania, Monduli, Septemba 6, 2014.

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ baada ya kuwatunuku nishani katika sherehe zilizofanyika kwenye ukumbi wa Jenerali Kiwelu wa Chuo cha Mafunzo ya Maafisa wa Jeshi Tanzania, Monduli, Septemba 6, 2014. Kulia kwake ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jeneral Davis Mwamunyange.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue katika sherehe za kutunuku nishani zilizofanyika kwenye ukumbi wa Jenerali Kiwelu wa Chuo cha Mafunzo ya Maafisa wa Jeshi Tanzania, Monduli, Septemba 6, 2014.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ baada ya Rais Jakaya Kikwete kutunuku nishani katika sherehe zilizofanyika kwenye ukumbi wa Jenerali Kiwelu wa Chuo cha Mafunzo ya Maafisa wa Jeshi Tanzania, Monduli, Septemba 6, 2014. Kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa na wapili kushoto ni waziri Mkuu Mstaafu John Malecela.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

TAARIFA YA KUITWA KWENYE USAILI WA JESHI LA POLISI 2014 KWA VIJANA WA KIDATO CHA IV NA VI WALIOOMBA NAFASI

$
0
0

Kuitwa kwenye Usahili:Orodha ya vijana wa kidato cha Sita na Nne waliochaguliwa

Jeshi la Polisi Tanzania linawaita kwenye usaili vijana waliomaliza kidato cha nne mwaka 2013 na  kidato cha sita mwaka 2014 ambao wamechaguliwa kufanya usaili kabla ya  kujiunga na Jeshi la Polisi.

Usaili utafanyika katika miji ya makao makuu ya mikoa Tanzania Bara Kwa tarehe zilizooneshwa kwenye jedwali hapa chini:

NA
MIKOA
KITUO CHA USAILI
TAREHE ZA USAILI
MUDA WA  USAILI
1
TANGA
OFISI YA RPC TANGA
18-21 /09/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
2
PWANI
OFISI YA RPC PWANI
23-26 /09/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
3
DSM ZONE
OFISI YA RPC  ILALA,KINONDONI,TEMEKE
28-01 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
4
MTWARA
OFISI YA RPC MTWARA
03-06 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
5
LINDI
OFISI YA RPC LINDI
08-11 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
6
SIMIYU
OFISI YA RPC SIMIYU
18-21 /09/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
7
SHINYANGA
OFISI YA RPC SHINYANGA
23-26 /09/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
8
TABORA
OFISI YA RPC  TABORA
28-01 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
9
KATAVI
OFISI YA RPC  KATAVI
03-06 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
10
RUKWA
OFISI YA RPC RUKWA
08-11 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
11
KILIMANJARO
OFISI YA RPC KILIMANJARO
18-21 /09/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
12
ARUSHA
OFISI YA RPC ARUSHA 
23-26 /09/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
13
MANYARA
OFISI YA RPC MANAYARA
28-01 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
14
SINGIDA
OFISI YA RPC SINGIDA
03-06 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
15
DODOMA
OFISI YA RPC DODMA
08-11 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
16
KIGOMA
OFISI YA RPC KIGOMA
18-21 /09/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
17
MWANZA
OFISI YA RPC  MWANZA
23-26 /09/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
18
MARA
OFISI YA RPC  MARA
28-01 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
19
GEITA
OFISI YA RPC GEITA
03-06 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
20
KAGERA
OFISI YA RPC  KAGERA
08-11 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
21
MOROGORO
OFISI YA RPC MOROGORO
18-21 /09/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
22
IRINGA
OFISI YA RPC IRINGA
23-26 /09/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
23
MBEYA
OFISI YA RPC  MBEYA
28-01 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
24
NJOMBE
OFISI YA RPC  NJOMBE
03-06 /10/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
25
RUVUMA
OFISI YA RPC RUVUMA
08-11 /09/2014
08:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
 Muhimu:

(i) Mwombaji anaruhusiwa kufanya usaili kwenye kituo chochote cha usaili kilicho karibu naye kulingana na tarehe zinavyoonesha kwenye jedwali hapo juu ili mradi awe amejiridhisha kuwa ni miongoni mwa walioitwa kwenye usaili. Jeshi la Polisi halitashughulikia usaili wa mtu ambaye hayupo kwenye orodha ya walioitwa kwenye usaili.

(ii) Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili aje na vyeti vyote vya masomo [(Academic Certificate(s)/Results slip(s) & Leaving certificate(s)] na nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (Original Birth certificate)]. Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.

(iii) Mwombaji awe na namba ya simu itakayotumika kumjulisha endapo atachaguliwa..

(iv) Kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili. Pia waombaji waje na kalamu za wino kwa ajili ya usaili wa kuandika.

Ni muhimu sana kwa kila mwombaji kuzingatia muda wa kuanza usaili.

PAKUA ORODHA YA MAJINA

1.Orodha ya vijana wa kidato cha Sita waliochaguliwa kufanya usahili

2.Orodha ya vijana wa kidato cha Nne waliochaguliwa kufanya usahili

Katibu wa Lema ajitosa Ukatibu Mkuu BAVICHA!

$
0
0

photo

Katibu wa Mbunge wa Arusha Mjini, Bw Methew Kishili (pichani)  kutoka Arumeru Mashariki amejitokeza kuwanina nafasi ya kuwa Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana Chadema Taifa (BAVICHA) katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Septemba 10 mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam. Ufuatao ni wasifu wake kama ambavyo Blog hii imeupata.

Nakusalimu Kamanda!
Jina langu ni Mathew Kishili, kijana Mtanzania wa kuzaliwa, mpambanaji wa Chadema na kwa sasa Mgombea nafasi ya Katibu wa BAVICHA Taifa. 

Kwanini Nafaa kuwa KATIBU WA BAVICHA!? Zifuatazo ni Dondoo za Wasifu Wangu Kielimu, Kijamii na Kisiasa.

Tarehe ya kuzaliwa kwangu ni  29/07/1984
Nina Elimu ya Shahada ya kwanza ya Maendeleo ya Jamii na Usimamizi wa Miradi kutoka Chuo cha CDTI-Tengeru, Arusha.
Nilijiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo mwaka 2009, tangia wakati huo nimekuwa mtiifu kwa chama nikikua kiuongozi ndani ya chama.

Uongozi Ndani ya Chama

Nimekuwa  Kaimu Katibu wa Chadema Wilaya Arumeru Mashariki kuanzia 2012-2014

Nimekuwa Mwenyekiti wa Vijana (BAVICHA) Arumeru Mashariki kuanzia mwaka 2010 hadi sasa

Nimekuwa Katibu wa Kata wa Chadema Kata ya Nkoaranga

Nimekuwa Katibu wa Tawi la Chadema Chuo Cha CDTI-Tengeru wakati wote nikiwa mwanafunzi.
Nimekuwa Meneja kampeni za Chadema kwa Chaguzi za kuunda Mamlaka ya Mji Mdogo USA River ambapo Chadema ilishinda Mitaa 6 kati ya 9 iliyokuwa inashindaniwa.

Uongozi nje ya Chama
Nimekuwa Katbu wa Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema kuanzia mwaka 2013 hadi sasa.
Nimekuwa Waziri wa Mikopo Chuo cha CDTI-Tengeru mwaka 2010/11.
Nimekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Miradi ya Vijana KKKT Usharika wa Nkoaranga
Malengo yangu na BAVICHA Mpya!!
Malengo yangu ndani Baraza la Vijana Taifa (BAVICHA) ni kuhakikisha Baraza linajitegemea katika uendeshaji wa operation zake na kupunguza utegemezi kwa chama kwa kiwango kikubwa kwa kuhakikisha Baraza la Vijana linakuwa na rasilimali zake zenyewe kama ardhi angalau kila Wilaya.
Kujengea vijana uwezo hasa nyanja za siasa, ujasiriamali, elimu ya sheria nk

Kuhamasisha Vijana kushiriki chaguzi kwa kupiga kura na kupigiwa kura.
Kutumia uzoefu wangu wa kiuongozi ndani na nje ya chama kuwaunganisha vijana nchini kuwa na sauti moja katika kupigania mustakabali wa taifa letu na chama chetu kwa ujumla.

Mkutano wa Maafisa Mipango kufanyika Oktoba

$
0
0

unnamed

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bi Joyce Mkinga (Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akitoa taarifa ya kufanyika kwa Mkutano wa Maafisa Mipango unaotarajiwa kufanyika Mwezi wa Oktoba mwaka huu. Kulia ni Mchumi Mkuu (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bw. Omary Juma.

 

 

clip_image002

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mkutano wa Maafisa Mipango kufanyika Oktoba

Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ipo katika maandalizi ya mkutano wa mwaka wa wachumi na maafisa mipango unatarajiwa kufanyika Oktoba 2014 jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na usimamizi wa uchumi na mipango hapa nchini.

Mkutano huu ambao niwa kitaalamu unawakutanisha wataalamu mbalimbali kutoka tasnia za mipango, uchumi, takwimu na maendeleo, wenye wajibu wa kusimamia uchumi na mipango ambao hukutana kwa ajili ya kujadili na kubadilishana uzoefu juu ya sera, mipango na kujenga mtandao wa masuala ya maendeleo ya kitaaluma.

Mkutano huu unatoa fursa kubwa ya kuwakutanisha kwa pamoja wataalamu hao na kujenga uelewa wa pamoja juu ya uendeshaji wa shughuli mbalimbali za Serikali. Pia hutoa fursa za kujadiliana kwa pamoja juu ya mafanikio na njia za kukabiliana na changamoto kwa kubadilishana uzoefu na ujuzi kwenye masuala hayo. Mkutano huo ni muhimu katika kuimarisha utendaji kazi wa kada hizi kwa minajili ya kusukuma gurudumu la maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.

Kwa kutilia mkazo masuala mbalimbali ya kimaendeleo yanayojitokeza hivi sasa, mkutano wa mwaka huu utajikita katika kujadili masuala yafuatayo;

i) Maendeleo ya Tasnia ya Wapanga Mipango (wachumi, maafisa mipango na watakwimu);

Mkutano utajadili fursa, na changamoto zilizopo katika kuleta maendeleo katika nchi. Huko nyuma kada hizi zilikuwa zinaratibiwa na iliyokuwa Wizara ya Mipango Uchumi na Uwezeshaji. Kwa sasa watakuwa chini ya uratibu wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Hatua hii itarahisisha utekelezaji wa mipango mbalimbali ya nchi.

ii) Maandalizi ya Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2015/16 – 2020/2021);

Utekelezaji wa Mpango wa Kwanza wa Taifa wa Maendeleo 2011/12 – 2015/16) unaendelea na tayari Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango imeanza kufanya mapitio ya utekelezaji wake ili kujua mafanikio na changamoto. Hivyo, katika mkutano huo wapanga mipango wanaandaliwa waweze kuanza kufanya maandalizi kwa ajili ya Mpango wa Pili wa Maendeleo (2015/16 – 2020/21).

iii) Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji katika Sekta ya Umma;

Serikali imeandaa mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji katika sekta ya Umma, lengo likiwa kuimarisha utendaji, ufanisi na uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali za umma zilizotengwa kwa ajili ya miradi na program za maendeleo.

iv) Jinsi ya Kujiandaa na Uchumi wa Gesi

Mkutano utajadili ni kwa jinsi gani Tanzania inajipanga kufaidika na rasilimali ya gesi asilia. Kwa kifupi masuala ya yanayohusu uwekezaji katika gesi asilia, usimamizi na jinsi ya kutumia rasilimali na menejimenti ya mapato yatokanayo na gesi, pamoja na ushiriki wa wananchi katika fursa mbalimbali zinazotokana na ujio wa gesi hiyo. Utayarishaji wa wataalam katika eneo hilo la gesi husani vyuo vya ufundi, vyuo vikuu na kadhalika.

Washiriki wa mkutano huu ni pamoja na wakurugenzi wa sera na mipango, maafisa mipango kutoka kwenye wizara, Serikali za Mitaa, idara na wakala wa Serikali, pamoja na taasisi za kitaaluma na watafiti wanaojishughulisha na masuala ya maendeleo na uchumi.

Mkutano wa mwisho wa mwaka wa maafisa mipango ulifanyika mkoani Morogoro tarehe 12 Machi 2010 ambapo uliandaliwa na Wizara ya Fedha. Mada nne zilizowasilishwa na kujadiliwa zilikuwa ni;

i. Wajibu wa wataalamu wamipango katika Maendeleo ya Uchumi: Mipango ya Kiuchumi, Utekelezaji na Uandaaji wa Taarifa;

ii. Soko la Pamoja la Afrika ya Mashariki;

iii. Ujasiriamali na Usimamizi wa Biashara kwa Wafanyabiashara Wadogo na Wakati; na

iv. Ufanisi wa Uwekezaji kutoka nje katika Uchumi wa Tanzania

MWISHO

Imetolewa na:

Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango

 

Taswira: Matukio ya Awali Kutoka Mkutano Mkuu wa BAVICHA Mlimani City Dar es Salaam

$
0
0

Bavicha5

Bavicha7Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mh Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa Vijana Mh John Heche wakiwasili eneo la Ukumbi Unakofanyikia Mkutano huo ambao utahitimishwa kwa kumchagua Mwenyekiti Mpya wa kuongoza Baraza la Vijana chadema sambamba na Viongozi wengine wa Baraza hilo.

Bavicha8

Bavicha1

Bendi maalumu ikitumbuiza kabla ya hotuba

 

Bavicha4

Bavicha6

Bavicha2

Mh: Freeman A.Mbowe akiwa na Mwenyekiti anaye maliza muda wake Mhe John Heche

Wajumbe wa Bavicha ndani ya ukumbi wa Mliman City

Wanao onekana mstari wa mbele ni dreva boda boda wa mkoa wa Dar es Salaam ambao nao ni wageni waalikwa

Mwakilishi wa Conservative People Party kutoka  Denrmak akitoa salamu kwa wajumbe wa BAVICHA

Live band ikituimbuiza katika ukumbi wa mlimani City

 

WANANCHI ARUMERU WABOMOA NYUMBA NA KUFYEKA MAZAO KWENYE VYANZO VYA MAJI

$
0
0

Vijana wakiwa na mabango kupinga uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji.


Upandaji miti kwaajili ya utunzaji wa mazingira


Ubomoaji wa nyumba ukiendelea


Wananchi wakikagua chanzo kilichogeuzwa shamba


Arumeru.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wa Kata ya Ngarenanyuki,wilayani Arumeru,wamebomoa nyumba moja iliyojengwa kwenye chanzo cha maji  ili kunusuru vyanzo hivyo ambavyo viko hatarini kukauka kutokana na ujenzi usiozingatia utunzaji wa mazingira.

Wananchi waliotekeleza hatua hiyo,Steven John na Frank Nnko walisema kuwa  wamechukua uamuzi huo baada ya serikali kushindwa kuwachukulia hatua za kisheria watuhumiwa wa uvamizi wa vyanzo vya maji .

Nnko alisema mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu kutokana na kuwa wananchi ndio waathirika wakubwa wa kukauka kwa vyanzo vya maji na kwamba  wameamua kujichukulia sheria mkononi na hawatasita kufanya hivyo kwa wananchi wengine watakaokiuka utunzaji wa mazingira.

Alifafanua kuwa kitongoji cha Momela ndicho chanzo kikuu cha maji katika Kata za King'ori,Makiba na Ngarenanyuki hivyo kuendelea kuwaachia wananchi wachache kuharibu mazingira kunaweza kugeuza eneo lote jangwa jambo ambalo linaweza kuhatarisha uhai wa watu na viumbe hai.

Mwenyekiti wa  jumuiya ya Maji bonde dogo  la Ngarenanyuki  ,Aminieli Mungure alisema kuwa vyanzo hivyo vimekua vikiharibiwa kwa  kukosa usimamizi hivyo wakati umefika wa jamii kuamka na kuvilinda kwaajili ya kizazi cha sasa na kijacho.

Aliongeza kuwa Bonde dogo la Ngarenanyuki linahudumia vijiji  vinne ambavyo ni Ngabobo, Olkung’wado,Uvizo na Ngarenanyuki na kuwa wataanza kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kutunza mazingira pamoja na vyanzo vya maji.

 

CHANZO: LIBENEKE LA KASKAZINI


Taarifa Muhimu: Uchaguzi Serikali za Mitaa Kufanyika Desemba 14, 2014

$
0
0

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika Desemba 14, 2014 nchini kote na kampeni zitaanza rasmi Novemba 30, 2014.
Taarifa rasmi kutoka ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa ya jana inafafanua zaidi kuwa uchaguzi huo utafanyika kwa kuzingatia sheria na kanuni za chaguzi za Serikali za Mitaa.

Soma hapa kwa
maelezo zaidi

MBOWE MWENYEKITI TENA CHADEMA, USHINDI WAKE WATIKISA TANZANIA

$
0
0
Hatimaye Mhe Freeman Aikael Mbowe Amechaguliwa Tena kuwa mwenyekiti wa Chadema Taifa,amepata asilimia 97.3 ya kura zote, makamu mwenyekiti Bara ni Profesa Safari na makamu mwenyekiti Zanzibar ni Saidi  Issa  Mohamedi

Kutoka kulia, Makamu Mwenyekiti Taifa, Prof Abdalah Safari, Mwenyekiti Freeman Mbowe , Makamu Mwenyekiti Zanzibar na Dr Slaa

Wajumbe wakishangilia ushindi wa Mhe Freeman Mbowe

habari mchanganyiko za picha katika uchaguzi wa Chadema

Mratibu wa Kanda ya Pwani

Huyu ndiye bwana Frank ambaye alikuwa mgombea mwenza wa Mh Freeman Mbowe

makamanda wa chadema wakifuatilia kwa umakini mchakato mkuu wa uchaguzi wa CHADEMA

Posted by CHADEMA KANDA YA KASKAZINI No comments:

Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest

Heka keka za Uchaguzi wa Mkutano mkuu wa Chadema Taifa

Mhe:Freema Mbowe Akwahutubia wajumbe wa mkutano mkuu kabla ya kujiozulu kupicha zoezi la uchaguzi

Wjumbe walivyo furika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City

Kwa hali hii ukombozi ni lazima

Ulinzi wahimarishwa Nje na Ndani ya ukumbi

‘MRITHI’ WA ZITTO KABWE APATIKANA CHADEMA

$
0
0

Maktibu wa Chadema katika picha ya pamoja.
Uchaguzi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo usiku huu umefikia tamati kwa Kamati Kuu ya chama hicho kupata viongozi wake

KATIBU MKUU --DK WILLBROD SLAA--

NAIBU KATIBU MKUU BARA-- JOHN MNYIKA

NAIBU KATIBU MKUU ZANZIBAR-ALUM MWALIM

viongozi awa waliteuliwa na mwenyekiti wa chama hicho kama katiba inavyosema na hatimaye baraza kuu likawapitisha wote bila kuwapinga

Mh JOHN MNYIKA anateuliwa kushika nafasi ambayo ilikuwa inashikiliwa na Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini mh ZITTO KABWE ambaye aliondolewa katika nafasi hiyo kwa kile ambacho kilisemekana kukos uminifu ndani ya chama hicho.


Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalim (kushoto) akiteta jaambo na Naibu Ktibu Mkuu Tanganyika, John Mnyika

TAZAMA HALI ILIVYOKUWA TETE BAADA YA MBOWE KUWASILI MAKAO MAKUU YA POLISI KUHOJIWA...WANANCHI WAANDISHI WAPEWA KIPIGO

$
0
0

Waandishi wa habari wakirekodi  tukio la kuwasili kwa Mh. Freeman Mbowe (hayuko pichani) Makao Makuu ya Polisi.

Mh. Tundu Lissu akiwasili.Mbuge wa Ubungo, Mh. John Mnyika akiwa ndani ya gari baada ya kukataliwa kuingia. Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Mh.  Wenje (kushoto), Mh. Msigwa na Mh. Joseph Mbilinyi wakiingia katika jengo hilo. Mwandishi wa habari Shamim Ausi mmoja wa wanahabari walioumia na kupoteza fedha na mali nyingine. Wanachama wa Chadema wakiwa wamekalishwa chini na askari. Kina mama ambao ni wanachama wa Chadema waliofika makao makuu ya polisi. Polisi wakiwakimbiza waandishi wa habari (hawako pichani) kwa kutumia mbwa. Wanahabari wakiwa mekusanyika baada ya kutimuliwa na  mbwa. Mmoja wa wanachama wa Chadema, Kamugisha Ngaiza, alivyowekwa chini ya ulinzi na polisi.
Muonekano wa polisi katika tukio hilo. Askari wakiwa hawataki kuwaona wanahabari eneo hilo.
Mwandishi wa habari, Badi, akilia kwa uchungu baada ya kuumizwa na mbwa wa polisi.

MNYIKA, WANASHERIA WAZUIWA KUINGIA NDANI WANAHABARI WAKIMBIZWA NA MBWA, WAUMIA, WAMWAGA MACHOZI

MAMIA  ya watu wamejitokeza leo  kumsindikiza Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, baada ya kuhitajiwa kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini, jijini Dar es Salaam kuhusiana na kauli yake aliyotoa majuzi juu ya kuitisha maandamano nchi nzima kupinga kuendelea kwa Bunge Maalum la Katiba.

Kilichofuata ni polisi kuamuru watu wote waondoke eneo hilo  kwa umbali wa mita 200 ambapo walikimbizwa na mbwa wa polisi na kusababisha wengi wao waumie na kupoteza vitu vyao mbalimbali, hususani wanahabari ambao baadhi yao waliumia na kupoteza zana zao za kazi.

 

TAARIFA NA PICHA KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS LTD

TASWIRA YA TUKIO LA MH FREEMAN MBOWE ALIPOKWENDA KUHOJIWA MAKAO MAKUU YA POLISI

$
0
0

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe akiwasili kwenye makao makuu ya Jeshi la Polisi nchini,Mapema leo asubuhi tayari kwa kwenda kuhojiwa juu kauli aliyoitoa kwenye Mkutano Mkuu wa chama hicho hivi katibuni,kuwa watafanya maandamano nchini nzima bila kikomo.

Makamu Mwenyekiti wa Chadema,Prof. Abdallah Safari na Wakili wa Chama,Wakili Mabele Marando wakiwasili kwenye Makao Makuu wa Jeshi la Polisi mapema leo.

Baadhi ya wapenzi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakishangilia baada ya gari lililokuwa limembeba Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, alipowasili leo Makao Makuu wa Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam, kwa mahojiano.

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika akizungumza na waandishi wa habari waliokuwepo kwenye eneo la makao makuu ya Jeshi la Polisi,juu ya kile kilichokuwa kikiendelea kwenye mahojiani katika ya Mwenyekiti wa Chama hicho na Jeshi la Polisi.

Mwenyekiti wa Chama cha DP, Christopher Mtikila akihojiwa na askari Polisi, alipowasili Makao Makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa bajaji, ambako Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alihojiwa na Polisi.

 

Dar es Salaam. Shughuli za kiserikali katika Wizara ya Mambo ya Ndani na ofisi jirani, jana zilisimama kwa siku nzima kutokana na hekaheka zilizoibuka baina ya polisi na wafuasi wa Chadema pale mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alipojisalimisha polisi.

Hekaheka hizo ziliibuka kuanzia saa 5.10 asubuhi baada ya Mbowe akiongozana na wanasheria wa chama hicho, kufika katika ofisi za Makao Makuu ya Polisi ambako pia zipo ofisi za wizara hiyo kuhojiwa kuhusu kauli yake ya kuitisha maandamano nchi nzima kushinikiza kusitishwa kwa Bunge Maalumu la Katiba.

Kabla ya Mbowe kuwasili, alifika Mkurugenzi wa Oganaizesheni ya Mafunzo na Usimamizi wa Kanda wa Chadema, Benson Kigaira na alipojitambulisha akakataliwa kuingia.

Baadaye waliwasili mawakili, Profesa Abdallah Safari na Mabere Marando ambao waliruhusiwa kuingia, kisha wakafuata Mbowe, John Mnyika na wanasheria wengine akiwamo John Malya na Peter Kibatala.

Wakati huo, Barabara ya Garden inayokatiza mbele ya wizara hiyo ilikuwa imefungwa na wafuasi wa Chadema walikuwa wamezuiliwa kwa mbali. Kila mwananchi aliyefika katika jengo hilo kupatiwa huduma, alijibiwa na askari waliokuwa na mbwa na silaha kuwa, “hakuna shughuli yoyote inayofanyika hadi kesho (leo)”.

Hali hiyo iliendelea hadi saa 9:10 alasiri baada ya Mbowe aliyehojiwa kwa saa mbili kuhusu tuhuma za uchochezi kuachiwa kwa dhamana.

Baada ya kuachiwa, Mbowe alisindikizwa kwa msafara wa magari manne ya polisi akielekea Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, ambako alipanda ndege kwenda Afrika Kusini kwa shughuli za kichama.

 

Ilivyokuwa

Ombi lililotolewa juzi na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John Mnyika kuwataka wanachama wa Chadema kujitokeza kumsindikiza Mbowe polisi, liliitikiwa kwani zaidi ya wanachama 100 walijitokeza katika ofisi hizo.

Walianza kukusanyika mmoja baada ya mwingine nje ya makao mkuu ya jeshi hilo kuanzia saa 4:30 asubuhi na kujichanganya katika kundi la waandishi wa habari, hali iliyosababisha askari polisi waliokuwa na bunduki na mabomu ya machozi kuwataka wanahabari wajitambulishe kwa kuonyesha vitambulisho ili wawatenge na wafuasi hao.

Licha ya juhudi hizo, hawakufanikiwa kuwatawanya wanachama hao ambao awali, walijieleza kuwa walikuwa wamefuata hati zao za kusafiria katika Ofisi za Uhamiaji zilizopo eneo hilo.

Hali ilibadilika baada ya Mbowe kufika katika ofisi hizo akiwa katika msafara wa magari matano huku ukiongozwa na Mnyika na wanachama hao kuanza kuimba nyimbo za chama hicho na kumsifu kiongozi wao.

 

Msafara huo ulizuiwa kwenye lango la ofisi hizo na askari wa FFU waliwazuia viongozi wengine, wakisema anayetakiwa kuingia ndani ni Mbowe na wanasheria wake pekee.

Baada ya gari la Mbowe kuingia, viongozi na baadhi ya wafuasi wa chama hicho nao walipenya kwa nguvu getini na kuingia ndani ya uzio huku wakisema ‘people’s power’ (nguvu ya umma). Kitendo hicho kiliwatibua FFU na kuanza kutumia nguvu kuwatoa nje, hali iliyozua vurugu kubwa.

Kutokana na mvutano huo, askari zaidi wa FFU waliokuwa katika Land Rover mbili wakiwa na mbwa waliongezeka na kuanza kuwashushia kipigo wafuasi hao huku wakiwataka kusimama umbali wa mita 100 kutoka lilipo jengo hilo.

Baada ya kutolewa ndani ya uzio baadhi ya wafuasi wa Chadema walikaa chini wakisema hawatafanya vurugu na wako tayari kuingia ndani wakiwa wamenyoosha mikono juu.

Katika kundi la wafuasi hao walikuwamo pia baadhi ya wabunge wa Chadema, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Mbeya Mjini), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini) na Ezekiel Wenje (Nyamagana).

Wabunge waliofika baadaye na kuruhusiwa kuingia ndani ni Suzan Lyimo (Viti Maalumu) na Halima Mdee (Kawe).

Miongoni mwa walioathirika na hekaheka hizo ni wanahabari ambao pamoja na kuonyesha vitambulisho na kamera, baadhi yao walishushiwa kipigo na askari hao.

Katika kipigo hicho, mwandishi wa Habari wa Gazeti la Tanzania Daima, Josephat Isango na Mwandishi gazeti la Hoja, Shamimu Ausi walijeruhiwa. Isango alijeruhiwa mguuni na Ausi usoni karibu na jicho la kulia.

Wakati Isango alisema alivamiwa na askari wawili wa FFU na kwamba hata alipojitambulisha na kuwaonyesha kitambulisho waliendelea kumpiga, Ausi alisema alipigwa rungu usoni na akashangazwa na nguvu kubwa iliyotumika wakati awali, aliruhusiwa kusimama katika eneo alipokuwa akiendelea na kazi.

Baada ya vurugu hizo waandishi wa habari na wafuasi wa chama hicho walitakiwa kusimama katika makutano ya Barabara ya Ghana na Ohio umbali wa mita 100 kutoka yalipo makao makuu ya jeshi hilo kusubiri mahojiano yaishe.

Ilipofika saa 8.45, Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu alitoka nje ya ofisi hizo na kuzungumza na waandishi wa habari na wafuasi wa chama hicho.

Alisema mahojiano kati ya Mbowe na Jeshi la Polisi yalikwenda vizuri huku akiongozwa na wanasheria na kwamba polisi wamekubali kumpa dhamana lakini kabla hajaondoka, wafuasi wote wanatakiwa kuondoka eneo hilo bila maandamano.

 

“Polisi wanaomba mtawanyike, hawataki maandamano, wao watamsindikiza hadi makao makuu ya chama yaliyopo Kinondoni, mkifanya maandamano watatumia nguvu kuyazuia na hilo hawataki litokee. Nawaomba mtawanyike,” alisema Lissu.

Baada ya tangazo hilo, wafuasi hao kwa shingo upande, walikubali ushauri huo na kuondoka katika eneo hilo saa 9.00 alasiri.

Ilipofika saa 9.20 Mbowe alitoka katika ofisi hizo akisindikizwa na magari ya polisi aina ya Land Rover zilizojaa askari na baadaye ilielezwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa aliyekuwa makao makuu ya chama hicho kuwa mwenyekiti huyo alikwenda moja kwa moja Uwanja wa Ndege kwa safari ya kikazi Afrika Kusini.

 

Mtikila azua gumzo

Wakati hekaheka zikiendelea, Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila alifika katika ofisi hizo saa 7.26 akiwa katika Bajaj lakini alizuiwa kuingia ndani na akaondoka.

Akizungumza na wanahabari, Mtikila alisema, “Ni lazima Watanganyika tuidai Tanganyika yetu kwa gharama yoyote, aluta continua.”

 

Makao Makuu

Baada ya kuondoka eneo hilo, wafuasi wa Chadema walikwenda katika ofisi za makao makuu ya chama hicho, Mtaa wa Ufipa, Kinondoni na kupewa maelekezo na Dk Slaa na Lissu.

Lissu alisema Mbowe anatuhumiwa kwa uchochezi kwa kauli yake kuhusu kufanyika maandamano nchi nzima, huku akisisitiza kuwa tuhuma alizopewa “ni za wizi wa kuku”.

“Mbowe aliposema kufanyika maandamano alikuwa na maana kuwa maandamano hayo yatafanyika baada ya Chadema kutoa taarifa, kauli yake haikuwa ya uchochezi hata kidogo,” alisema Lissu.

Aliongeza, “Kama polisi wakitueleza ni sheria ipi inakataza maandamano, sheria ipi inalazimisha wanaotaka kuandamana lazima wawe na kibali na sheria ipi inakataza watu kugoma, watakuwa na ruksa ya kumfunga Mbowe.”

Kwa upande wake, Dk Slaa alisema, “Mbowe baada ya kutoka polisi ameomba nimwagie kwa wanachama wa Chadema. Amekwenda Afrika Kusini katika mkutano wa chama. Safari yake ilikuwa imepangwa tangu juzi na ingeahirishwa kama angenyimwa dhamana leo.”

Dk Slaa alimwagiza Kigaira kuhakikisha kuwa wanachama wawili wa chama hicho waliokamatwa na polisi wanaachiwa kwa dhamana. Zoezi la kufanya maandamano likifanyika kama hivi Taifa hili litabadilika,” alisema.

Imeandikwa na Fidelis Butahe, Raymond Kaminyoge na Susan Mwillo wa MWANANCHI

 

Viewing all 1899 articles
Browse latest View live




Latest Images